DOKEZO Biashara kufanyika karibu kabisa na Barabara, Mbezi Mwisho karibu na Kituo cha Daladala ni hatari kwa usalama

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
photo_2024-06-04_16-21-12.jpg
Hapa Mbezi Luis Stendi barabara ya kwenda Kinyerezi ilivyojaa msongamano wa machinga na bidhaa zao ambazo ziko kando ya barabara na kusababisha barabara kuzidi kuwa finyu licha ya wembamba wake tangu kutengenezwa, siku dereva yoyote akishindwa kulimudu gari likaenda pembeni litaua watu wengi sana.

Tena si machinga pekee bali hata wapita njia na wanunuzi, maana hali ilivyo ni msongamano wa watu barabarani kutokana na kukosa njia ya kupita maana njia zote za watembea kwa miguu zimezibwa na machinga na kulazimika watu kupita barabara kuu kama magari ivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kugonjwa na gari, bajaji, bodaboda na wao wenyewe kugongana kwa kuwa wanapita kwa kulazimisha huku wakikwepa magari.

Wafanyabiashara wa hapa wamejimilikisha eneo la barabara na la watembea kwa miguu huku wakiwa hawana wasiwasi wa kuwa wanahatarisha maisha yao kwa kukaa barabara, wengine wameweka ndoo na kuzikalia huku wakiipa mgongo barabara hali ya kuwa wapo pembezoni mwa barabara na magari na vyombo vingine vya usafiri vikipita na wala hawajali wao huendelea kuuza bidhaa zao ambazo wameziweka kwenye kinjia kilichokuwa kimeachwa kwa ajili ya watembea kwa miguu.

Sijui mamlaka ziko usingizini au eneo hili hakuna viongozi wanaoweza kuona hatari kabla haijatokea na wakachukua hatua ya kudhibiti kabla ya majanga husika. Narudia tena siku ikitokea gari ikachochora hapo ni balaa tutabaki kulaumu wakati tungeweza kuzuia hali hiyo.

Hao machinga kama wameshindikana kuondolewa kama ambavyo mwanzo walikuwa wakitolewa basi wawekewe namna nzuri ya kukaa, wasikae barabarani, wasizuie njia za watembea kwa miguu ili kuepuka hatari ambayo inaweza kuepukika.

Machinga kwenye eneo hilo licha ya kuwa sababu au chanzo kero lakini wanahatarisha sana usalama wao na wateja wao ambao muda mwingi usimama kwenye eneo la barabara ili kuhudumiwa.

Lakini nimekuwa nikibakia kujiuliza hivi Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeshindwa kubaini changamoto hiyo na kuipatia suluhu kwa kuwaondoa wamachinga walioko kwenye maeneo hatarishi na yanayochangia kero au tunasubiri mpaka majanga makubwa yatokee ndio tuanze kuwajibika.

Viongozi wenye maono wanatakiwa kutatua changamoto kabla madhara makubwa hayajatokea tusijifungie, katika hili Viongozi wenye mamlaka ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo au ngazi ya Mkoa ni vyema mkaliona hili kwa uharaka mimi nimewadokeza, naamini wengi waliopitia njia hiyo mtaungana na mimi.

photo_2024-06-04_16-23-35.jpg

photo_2024-06-04_16-21-50.jpg
 
Hapo Mbezi watembea kwa miguu hawana haki wafanyabiashara wanaweka bidhaa mpaka wapita njia mnakosa eneo mnabaki kubanana na ole wako uguse biashara zao kwa bahati mbaya matusi mapya utayasikia hiyo siku.
 
Bwana DC yeye anakimbizana na madada poa riverside haoni hili janga mkabara na ofisi yake!
Pengine atokee mtu na fuso au mende afanye kweli hapo utaona serikali nzima itakavyotoa rambirambi na kugharamia mazishi na kulaani saana na kisha kupiga marufuku msongamano huo!

Serikali ya majanga!!
Wanashindwa nini kutangaza tenda ya kuboresaha barabara hiyo kwa kuifunga na kuhamisha wachuuzi wote kuwapeleka maeneo salama na kisha kusimamia wasirudi tena baada ya kuimprove barabara hiyo?!
 
Hapa Mbezi Luis Stendi barabara ya kwenda Kinyerezi ilivyojaa msongamano wa machinga na bidhaa zao ambazo ziko kando ya barabara na kusababisha barabara kuzidi kuwa finyu licha ya wembamba wake tangu kutengenezwa, siku dereva yoyote akishindwa kulimudu gari likaenda pembeni litaua watu wengi sana.

Tena si machinga pekee bali hata wapita njia na wanunuzi, maana hali ilivyo ni msongamano wa watu barabarani kutokana na kukosa njia ya kupita maana njia zote za watembea kwa miguu zimezibwa na machinga na kulazimika watu kupita barabara kuu kama magari ivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kugonjwa na gari, bajaji, bodaboda na wao wenyewe kugongana kwa kuwa wanapita kwa kulazimisha huku wakikwepa magari.

Wafanyabiashara wa hapa wamejimilikisha eneo la barabara na la watembea kwa miguu huku wakiwa hawana wasiwasi wa kuwa wanahatarisha maisha yao kwa kukaa barabara, wengine wameweka ndoo na kuzikalia huku wakiipa mgongo barabara hali ya kuwa wapo pembezoni mwa barabara na magari na vyombo vingine vya usafiri vikipita na wala hawajali wao huendelea kuuza bidhaa zao ambazo wameziweka kwenye kinjia kilichokuwa kimeachwa kwa ajili ya watembea kwa miguu.

Sijui mamlaka ziko usingizini au eneo hili hakuna viongozi wanaoweza kuona hatari kabla haijatokea na wakachukua hatua ya kudhibiti kabla ya majanga husika. Narudia tena siku ikitokea gari ikachochora hapo ni balaa tutabaki kulaumu wakati tungeweza kuzuia hali hiyo.

Hao machinga kama wameshindikana kuondolewa kama ambavyo mwanzo walikuwa wakitolewa basi wawekewe namna nzuri ya kukaa, wasikae barabarani, wasizuie njia za watembea kwa miguu ili kuepuka hatari ambayo inaweza kuepukika.

Machinga kwenye eneo hilo licha ya kuwa sababu au chanzo kero lakini wanahatarisha sana usalama wao na wateja wao ambao muda mwingi usimama kwenye eneo la barabara ili kuhudumiwa.

Lakini nimekuwa nikibakia kujiuliza hivi Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeshindwa kubaini changamoto hiyo na kuipatia suluhu kwa kuwaondoa wamachinga walioko kwenye maeneo hatarishi na yanayochangia kero au tunasubiri mpaka majanga makubwa yatokee ndio tuanze kuwajibika.

Viongozi wenye maono wanatakiwa kutatua changamoto kabla madhara makubwa hayajatokea tusijifungie, katika hili Viongozi wenye mamlaka ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo au ngazi ya Mkoa ni vyema mkaliona hili kwa uharaka mimi nimewadokeza, naamini wengi waliopitia njia hiyo mtaungana na mimi.

wapiga kura hawa waacheni, ila siku likifeli lori utaskia sijui nani kawapenda zaidi
 
Inatakiwa ujue kuwa, biashara ndogo ndogo ni asilimia 90 ya biashara Tanzania, ungesema tu wafanyevipi mfano waweke reflectors kwenye vibanda au gari zipite kwa mwendo wa 10KPH eneo husika.
Siyo Mbezi Luis tu, Mbagala, Tandika hata Kariakoo wana challenge hiyohiyo
 
Back
Top Bottom