Biashara niliyofungua Aprili 2022 nimeifunga Agosti 2024

Nimejifunza kitu kizuri sana kwako.. inatakiwa nijifunze kuwa mfuatiliaji kwenye biashara.
Kwasasa nipo Mkoa wa Pwani, ila kikazi ntahamia Nyanda za juu kusini(Greencity) next year Mwenyezi mungu akijalia, Kama unampango wakunishauri anzia Greencity ndugu yangu.
 
Sasa dunia ya Leo ndiyo kumpata mwanamke wa hivi imekuwa mtihani sana .

Ewe dada niliyekopa ili ufungue biashara ukakimbilia Tabora kuolewa na mlina asali ,yangu macho na roho Ila ipo siku .

God nipe mwanamke wa hivi sio hawa mashangingi wa kwenye vilabu vya ulanzi.
 
Kwani huwezi kuifanya kwa kupitia utaratibu halali ? Au kuni zimepigwa marufuku huko Chugastan ?
 
Mnawatoaga wapi hao wanawake wanaowapigia simu wateja wenu kuwatukana?

Aisee kuna vitu kama mwanaume hautakiwi kumchekea mwanamke akifanya hata mara moja.
 
Mi niliacha kazi
Nikajikita sehemu moja
Sijutii na namshukuru Mungu kwa uamuzi niliouchukua mapema japo sio mapema sana
Haya mambo ni chemistry flan hivi,ukiwa na kimeo flan kiko katika maisha yako kila kitu kinakuwaa namna flan hivi,codes ni vitu mhimu
 
2yrs umejitahidi mkuu hapo usimamizi hafifu ndo changamoto kuu.
 
Dah ila nashangaa sisi ambao tunapenda kuendesha biashara za wenzetu kama za kwetu huwa hatudhaminiki tunawaingizia pesa maboss lakini kukulipa hadi msumbuane lakini ambao wale ambao hawajali kazi za watu ndo wanapata fursa nzuri hadi na kupewa mda mzuri wa wiki nzima kuwapiga maboss zao yaan inasikitisha kiongozi nikusihi mda mwingine biashara kueindesha inafaa sana uwe na mda wa kuiangalia tunasemaga mtu yeyote huwa anadili sana na kile kinacho mpa faida hivyo basi kama utatumia mda mwingi kwenye kazi fulan huku kazi nyingine ukashinda kuzifatilia ipasavyo basi hiyo unayoitumia mda mwingi kuzifatilia ndo yenye masilai zaidi kuliko hiyo nyingine
 
Binadamu hatujawahi kueleweka....cha ajabu utampata wa hivi utaanza kulia lia tena ooh mke yupo bize hana muda wa kunipikia, hanifulii boxa bla bla bla 😁
 
Mambo machache niliyojifunza kuhusu biashara....

1: Biashara ni usimamizi.
Mwajiriwa kama unavoamka asubuhi mapema unaoga na kuwahi kazini ndivyo hivyo biashara inakutaka, amka mapema oga wahi katika biashara yako.

2: Hakuna mtu atakaefanya kazi ya kukutafutia pesa wewe.
Yani ufungue biashara umpe mtu achakarike, kama ni juani azunguke, kama ni shambani apige kazi kisha akukusanyie pesa wewe akuletee, huyu mtu hayupo, hii biashara haipo.

3: Usifanye biashara ya kuambiwa.
Usifanye biashara za kuambiwa na kusikia kuwa phoneaccessories zinalipa, nawe utimbe huko, duka la mangi lnalipa nawe huyoo, kilimo kinalipa nawe huyooo. Biashara utakayoifanya kwa moyo na ikaleta mafanikio ni inayoanzia kwako, yani idea ianzie kwako.

4: Mwajiriwa angalia biashara ambazo zinahitaji walau minimal supervision walauu....nasisitiza walau kwasababu najua zote zinahitaji usimamizi tena haswaa ila kuna utofauti wa biashara na biashara.
Mfano biashara ya kukodisha vitu hii nii bora zaidi kwa waajiriwa, au biashara ya vitu vinavyohesabika mf duka pampers unajua kabisa kuna carton ngapi zikiuzika unajua, tofauti na biashara ya mchele unamuachia mtu gunia la kg 100 akiuza 10 akasema kauza kg 3 unahakiki vipi? Utahakiki magunia yote?

Itaendelea......
 
Big points,

Pia biashara ni maisha means unatakiwa kuiishi biashara usifanye kama kuna ukomo ukifikia utaacha fanya biashara kuwa ndio maisha yako wekeza nguvu na akili zako zote kwenye biashara uliyochagua kuiishi hapo ndio utaona faida ya unachokifanya
 
Madini ya wasoma vitabu🔥🔥
 
Hongera Kwa kuanza, ila kwenye kupumzika mwaka mmoja hapo nakupinga. Maisha hayana mambo ya kupumzika anza Tena hata Kwa udogo ukiendelea kuzoeleka kwenye mfumo Hadi hapo utakapo tia pesa ya maana.
 
Inaendelea.....

5: Kabla ya kuamua kufanya biashara flani ifnyie utafiti wa kutosha.
utafiti wa kutosha yani....sio tu thread wakuu nataka biashara ya mama lishe vipi, majibu yanakuja nunua sahani nunua sufuria na mwiko anza kazi inalipa😹, maana yake nenda kwa mama lishe kakae hapo huku ukipiga story na kula angalia namna wanavofanya kazi zao, najua wanasambaza chakula na kukusanya hela jioni uliza changamoto zao tembelea wengi wa kutosha na biashara nyingine hivyo hivyo.

Experience yangu katika hili: nilivagaa biashara ya kukopesha nilienda kariakoo beba mapochi beba nguo biashara siijui nikakopesha watu.....mmmh nilibaki na majuto heri ningevaa tu hizo nguo na pochi nkabeba.

Experience yangu nyingine: nilifungua duka la vyakula mchele, unga, maharage nk nikamuweka housegirl nliekaa nae nyumbani miaka 7 nikiamini namjua ni mwaminifu, home nikaweka mwingine daaaah kumbe pesa haina uaminifu, alikua anakula hela zangu kama hana akili na kwakua nlimuamini nlifanya mahesabu kizembe hata mwezi unakata sijapiga hesabu.

Kosa lingine kubwa sana nilifanya kutokujua mi mwajiriwa naamka asubuhi naenda kazini yeye anaenda dukani, anauza ila anasema hajauza nitajuaje??? Hii biashara sikupaswa kuifanya kabisa make inahitaji uwepo muda wote namie kuwepo muda wote haiwezekani ila wala sijutiii sasa nisingefanya ningejifunza vipi.

Pia ilikua mbali na nyumbani mbali na kazini gharama za nauli daily nk mwisho nilichukua vyakula nkaweka nyumbani tukala.

Nmeamua kufanya biashara nyingine inayoendana na kazi yangu, nilianza kwa utafiti nimezunguka sana, nashukuru kuna jamaa anaifanya na sio mchoyo wa maarifa amenipa sio tu abc....yani ni abc hazi z ana roho nyeupe, nimepitia nyuzi sana, na ninaisimamia vema naamka mapema naanzia kwenye biashara kwanza saa mbili ndo naenda kazini, nikitoka chaaap narudi kijiwe,
naiona mwelekeo mzuri.....hii haifi yani ntakufa mie hii haifi 😹

waajiriwa tuchague biashara walau yenye usimamizi wa kueleweka, isiokuhitaji hapo 100% yani inaweza kuendelea vema na haupo mfano biashara za kukodisha vitu mbalimbali, vyombo, maturubai, viti, nk nk vya kukodi ni vingi, au biashara inayohesabika unajua vilikua vitano kimeuzwa kimoja vimebaki vinne....

Kama ni biashara ya chakula, mfano mi nikitaka kuifanya nitauza ugali, nyama choma/mishkaki na kachumbari tuuuuu au ndizi kaanga/choma pia.....hii ina urahisi kusimamia nmeacha ugali 30 nikija nataka hesabu ya ugali 30 kama umebaki nitaona, ila ukianza na wali na michuzi mambo yatapandiana.
 
Katika biashara kuna siri ambazo pia watu hawasemi na ndio siri za mafanikio mixa ujanja ujanja.....

Ndugu yangu anauza mchele ananunua mchele wa aina moja mfano ni mchele wa 1200, anaugawa, anaweka kwenye mashine unapakwa mafuta wanajua wenyewe huu unakua na bei yake imechangamka, mwingine haupakwi mafuta ila anatoa chenga huu una bei yake pia, na mwingine anauacha kama ulivyo na huu una bei yake......mchele huo huo wa bei moja ila una bei tatu tofauti 😹 #siri za biashara

Kwenye stationery kuna mahali wameandika copy sh 40 maana yake huku na huku sh 80, sasa utalipa sh 80? Obvious utalipa 100 na ndio bei halisi....lugha ya biashara #siri za biashara
 
Umetoa madini yamesimama kwelikweli...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…