Biashara nzuri ya uzalishaji isiyo ya umachinga

happyxxx

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2020
Posts
604
Reaction score
1,970
Wataalam wa business naombeni ushauri wenu kwa hapa Dar es Salaam ni biashara gani nzuri ya uzalishaji naweza ifanya yani niwe mzalishaji bidhaa sio kuchuuza.

Niliwaza kutenengeza pedi lakini naona mtaji wake utanishinda inabidi mzigo kuagiza utengenezwe China pia nikisema nizalishe hapa hapa production cost ni kubwa.

Naombeni mawazo yenu ni kitu gani naweza fanya cha uzalishaji just any idea nitashukuru sna.
 
Ni bidhaa gani bongo zinaweza kuzalishwa? Zalisha vifungashio visivyo boksi
 
Tanzania tuna maligafi nyingi za kuzalisha bidhaa nyingi ila inaweza kuwa changamoto vitendea kazi au mitambo, ujuzi,wataamu, mitaji , vibali nk.

-Unaweza kuzalisha mkaa mbadala
-unaweza kuzalisha vyakula vya mifugo
-unaweza kuzalisha dawa za kudhibidi wadudu wasumbufu kwenye makazi ya binadamu, wanyama na mimea
-unaweza ukazalisha mbengu za mazao mbali mbali ya muda mrefu na mfupi
-unaweza ukazalisha samani mbali mbali za ofisi na makazi ya watu

Na vingi ambavyo vinamzunguko mkubwa katika maisha yetu ya kawaida, pia nakupingeza kwa kuja na mbadala maana kila mmoja wetu huwa linatujia wazo la kununua na kuuza na wala sio kuzalisha na kuuza .

Mwenye kuzalisha na kuuza huanza kwa mtaji mkubwa lakini humchuka muda mfupi kama kukiwa hakuna changamoto kubwa kupata faida kubwa.
 
Juice ya miwa
 
Tafta maziwa ya kutosha uanze uzalishaji wa yoghurt ns ice cream
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…