Biashara ya Bodaboda

Ndio maana tunashindwa kushindana na wahindi na wachina. Wenzetu hiyo faida ya 3000 kwa siku ni nyingi mno na kwa kuwa wana nidhamu ya biashara wanafanikiwa sana.
Wenzetu wana Pambana, kuwa na vitega uchumi vingi vyenye kuwaletea hizo 3000 tatu za kutosha
 
Binafsi niko njiani kuianza hii biashara ndani ya mwezi mmoja. Sioni faida kuiweka 2.3M banki na mitozo yote hii kuliko kuikosa 3000 ya siku, nani atanipa bure?
Mkataba kwa siku 10k wengine hadi 12k ndani ya mwezi unaingiza 300k hadi 360k

Ukiwa nazo mbili 600k hadi 720k kwa mwezi

Tuseme zote ulinunua used kwa 1.3m + 1.3m= 2.6m

Ndani ya miezi 4 umerudisha hela yako yote uliyonunulia unaanza kutengeneza faida

NB: Nidhamu ya matumizi, usimamizi mzuri wa chombo, usicheke na dereva kuwa kauzu
 
Kumbe mwanafunzi una nielewa vyema.
👉Msisahau na bajaji. Ntawapa dark secret kuhusu hivi vyombo vya moto
 
"Ni Biashara nzuri Kwa maana FEKON Moja inauzwa 2.3M Kwa Faida wewe Utapata sio chini ya 1M Kwa miezi 11 au 1.3M Kwa miezi 12. Ambayo ni sawa na faida ya 100,000/= Kwa Kila mwezi Kwa Pikipiki Moja"

Miss allocation of money. Asante kwa mchanganuo, biashara hii hainifai
 
Biashara ya bodaboda ni nzuri sana na inalipa haswa endapo tu dereva utakua wewe mwenyewe, otherwise utakua unamfaidisha mtu. Imagine dereva anaingiza zaidi ya 30k then ya bosi ni 10k, tena hapo kashajaza mafuta na other expenses kasha clear.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…