Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Mkuu,
Nakushauri yafuatayo;

Kama una mtaji unaofika 20m, na kuendelea, fungua biashara ya mgahawa wa kisasa, tengeneza chakula kizuri, customer sevice mzuri na usimamizi mzuri. Au kawekeze kwenye ufugaji wa kisasa wa Ng'ombe wa maziwa au mbuzi.

Daladala kwa sasa si biashara salama.
1. Hiace na coater ziko kwenye mchakato wa kuondolewa kwenye ruti nyingi,

2. Faini za barabarani zitakula faida na mtaji

3. Gharama za uendeshaji ni kubwa mno.

4. Risk za kazi ni nyingi sana

5. Madereva watakufanya usiwe na amani katika kipindi chote ambacho unafanya hiyo biashara. Kila simu ikiita moyo utakuwa unaenda mbio.

Nakutakia mafanikio mema ndugu yangu.
 
Sawa mkuu
 
Vipi kuhusu biashara ya trekta (kilimo )?
 
Kifupi hakuna biashara isio na changamoto yaani ya mteremko tu,ni sawa na kuwa na uhusiano ulioshwali siku zote,
 
Kifupi hakuna biashara isio na changamoto yaani ya mteremko tu,ni sawa na kuwa na uhusiano ulioshwali siku zote,
Nikweli, ila kuna ile ambayo unaweza icontrol mwenyewe , risk yake ni ndogo, tofauti na ile inayoendeshwa na mtu.
 
Nikweli, ila kuna ile ambayo unaweza icontrol mwenyewe , risk yake ni ndogo, tofauti na ile inayoendeshwa na mtu.
Ukiwa na mda ukaifanya mwenyewe risk ni ndogo kuliko kumpa MTU akufanyie,
 
Nimetupa Pesa nyingi sana sababu ya kutokuwa na mda wa kusimamia hadi nazijutia,
 
tatizo kubwa la daladala ni wafanyakazi, wengi ni wapumbavu na hawawazi kesho. Utakuta dereva au konda yupo radhi kufukuzwa kwa kukuibia buku 10 . Gari likiharibika anashangilia , kitu kidogo kikiharibika basi hupati hesabu hata kama kifaa ni elfu 5.
 
Hivi biashara ya Hiace ipoje Wakuu ??, Ukiiweka sehemu iwe inasafirisha abiria vipi inalipa ???. Bei ya Hiace mpya ni kiasi gani ??, Je Hadi iruhusiwe kupiga mishe road mchakato gani unapitia ?, Vitu gani vinahitajika ??. Karibuni kwa mawazo.
 

Asante kwa usharui mnono
 
kaka vp?
naweza pata mawasiliano yako
 
Nami nataka kuhama kutoka kwa noah nihamie kwa hiace

Dumelang
 
kila biashar ina changamoto yake, unaposema aiache atafute nyingine atakutana na changamoto pia, je utamshauri aiache atafute nyingine siatakua anatwanga maji kwenye kinu..... chakufanya pambana hizo ni changamoto endelea kutafuta utampata mwaminifu
na mambo yataenda sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…