Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Pole sana.

Ukiingia kwenye biashara ya daladala ni lazima kwanza uwe na dakitari wa kuangalia afya yako kwa karibu sana.

Pili ukubali kugawana mapato sawa na dreva na askari.
 
Biashara kama hiyo inahitaji ufuatiliaji wa hali ya juu. Kuchanganyikiwa kupo sana tu mana kila mara unapewa sababu nyingi huku mapato ya siku kama ulivyopangilia hayafiki.

Hilo wazo mbadala la kutafuta tenda kwenye shule ni zuri, jitahidi utembelee shule na kujitangaza pia kuacha mawasiliano yako ili wakihitaji wakuzingatie.

Ila hiyo ya daladala inahitaji upinde kiakili kidogo.
 
Pole sana ndugu yangu. watafute wapenda tena mujahidina kabisa ndo anakufaa kwani wewe unawatafuta vibaka tu. Pia nenda kijijini kwenu tafuta kijana aliyetulia mwambie unampaka zi kisha awe konda kama kuna ujinga atakwambia tena unampamasharti utaona matunda. Ishu ingine wewe usimkabidhi dereva gari mkabidhi konda ndio atafute dereva kwahiyo linakuwa lao sim moja ukiona hivi unapiga chini konda sio dereva waizi ni makonda
Nashukuru kwa mchango wa mawazo!

Original Pastor, hilo la kumweka ndugu kama konda nimelifanya japo sikumtoa kijijini. Kilichotokea ni kuwa mheshimiwa alitafuta dereva kweli lakini hakuishia hapo aliweka na konda pia! Kila wakati yeye yupo chini ya mti akisubiri aletewe hesabu ya kila trip wanayofanya.

Hesabu ndo ilikuwa mbovu zaidi kwa sababu kwanza watu wa kugawana waliongezeka maana ni makonda wawili (Mmoja akiwa bosi-mtoto) Pili nilikuwa na wakati mgumu kumbana kwa kuwa ni ndugu.
 
Best madreva wengi mapanja tu. Pole sana usijekuta huyo dreva wako kashanunua hiace yake kupitia yako.
 
all in all nisingekushauri kufanya biashara ya usafirishaji kuwa biashara ya kwanza (i prefer uzalishaji mali).
Ukipata tenda ya kukodisha itakupunguzia presha

Can someone expound on the idea given by Amoeba? Au amoeba mwenyewe utoe muongozo zaidi. Zingatia unatoa ushauri kwa mwenye mtaji mdogo wa not more than 15M na ambaye mazingira ya kazi yanamuachia masaa machache tuu kwa siku (Km si jumamosi na jumapili tuu)

Maelezo zaidi pse!
 
Hallo Bwire,

Biashara ya Daladala ni Biashara kichaa.

Ukipata pesa Jenga Nyumba inayopanda Thamani kila siku.

Dereva wa Daladala anakwambia tajiri ndiye Mwenye gari na sisi ndiyo wenye pesa.

Utadanganywa mpaka utafilisika.

Ili ufanye Biashara ya Daladala lazima uanze kuendesha wewe mwenyewe iliujue unapata kiasi gani na mabao huwa inakuwaje.

Vinginevyo ni tatizo.
 
Reffering to the bolded part above, inatia uchungu sana hasa nikikumbuka wakati nilioupitia kuzichanga kwa ajili ya hiyo project! These madereva are indeed "heart-less"! Hii ni wiki ya tatu nimeiweka Yard. Najua napata hasara kwa kuiweka yard, but I still consider it as the best thing to do at the moment. At least I have peace of mind. Kila ilipopigwa simu hata kabla sijajua ni nani moyo ulikuwa kama unataka kupasuka.

Wazo la kujenga nyumba kwa ajili ya biashara naliona kama bado ni over-size kwa sasa, hasa ukichukulia ukweli kuwa hata kibanda changu cha kuishi bado kinanipa mtihani wa finishing. Nashukuru kwa ushauri na kwa ku-share experience yako kuhusu biashara ya daladala.
 
Biashara ya daladala ni HEADACHE. Nenda nao taratibu ipo siku utatoka tu. Ila sijui utampata wapi dereva mzuri. wapo lkn ni mia kwa mmoja. mara nyingine wanaelewana na TRAFFIC na wanasema wamepigwa bao. Ukiwapa pesa, wanakutana baadae wanagawana. Kaaazi kwelikweli.

Pole Mkuu.
 
UZOEFU: CHANGAMOTO YA MADEREVA KUTOKUWA WAAMINIFU
Nilipopata vicent nilishauriwa kuchukua daladala (Hiace) ili ifanye kazi kigamboni. kupitia JF nilifaninikiwa kuipata. Lakini kilichofuata hapo ni sawa na ndoto ya kutisha!... ukiamka hutamani usinzie tena.

ne! Sasa naanza kuhisi kuwa they are probably all the same!! Na inanipunguzia concetration yangu kazini.

Baadhi ya watu wanasema ningeweza kuitumia vizuri kama nikitafuta tenda ya kubeba watoto (Nursery) na kuwa hiyo haina longolongo nyingi. Naomba ushauri wenu wakuu! Pse, pse!!
We utakuwa ulilinunua kwa mtu na lilikuwa limeshachoka. Na vile vile hukumpata dereva bali mwizi.
 
Biashara ya daladala ni HEADACHE.. Nenda nao taratibu ipo siku utatoka tu. Ila sijui utampata wapi dereva mzuri. wapo lkn ni mia kwa mmoja. mara nyingine wanaelewana na TRAFFIC na wanasema wamepigwa bao. Ukiwapa pesa, wanakutana baadae wanagawana.. Kaaazi kwelikweli.

Pole Mkuu.
Kila shughuri ina headache zake. Hakuna iliyo mteremko, ni kukaza buti tuuuuu. Umeshawahi kusikia tabu ya kuwa na teksi? Tatizo ni kuwa watz tunapenda sana biashara zenye kukuza majina huko uswazi kwetu; ANA HIACE TISA HUYO, ANA KOROLA SABA HUYO ZOTE TEKSI. Kumbe kila kororla la ulinunua Tsh 8M, na unaletewa 10,000/= kwa siku.siku nyingine longolongo kibao na hatari ya kutekwa kwa gari.

Kuna mtu ana guta 3 na anakula 10,000/= hadi 15,000/- kila guta kila siku. Guta moja alinunua Tshs. 400,000/= hadi 500,000/=

kuna mtu ana mikokoteni ya maji 5. kila mkokoteni alitengeneza kwa 80,000/-, anakua buku kila mkokoteni kila siku.
 
Aisee ukimwambia mtu yeyote anayefanya kazi maofisini akanunue guta atakushangaa sana! Lakini ukiangalia it really make sense.

Hizi biashara za magari ni nuksi sana aisee. hasa kama na wewe tajiri hujui spea za magari. yaani utafilisika.

nakumbuka yalinikumba haya haya ya mkuu hapo juu. nilinunua Hiace 14m baada ya miezi miwili niliuza 8m huku nikiwa nimeshaingia gharama zaidi ya 1.5m. its better ukajenga nyumba kama una mtaji
 
Reffering to the bolded part above, inatia uchungu sana hasa nikikumbuka wakati nilioupitia kuzichanga kwa ajili ya hiyo project! These madereva are indeed "heart-less"! Hii ni wiki ya tatu nimeiweka Yard. Najua napata hasara kwa kuiweka yard, but I still consider it as the best thing to do at the moment... At least I have peace of mind. Kila ilipopigwa simu hata kabla sijajua ni nani moyo ulikuwa kama unataka kupasuka...

Wazo la kujenga nyumba kwa ajili ya biashara naliona kama bado ni over-size kwa sasa, hasa ukichukulia ukweli kuwa hata kibanda changu cha kuishi bado kinanipa mtihani wa finishing. Nashukuru kwa ushauri na kwa ku-share experience yako kuhusu biashara ya daladala.
UZOEFU: SUALA LA UAMINIFU WA DEREVA NA KONDAKTA

Pole sana ndugu. Kwa mtu aliyewahi fanya hiyo biashara anaweza kukuelewa kiurahisi sana ni magumu mangapi unayapitia. Believe me, madereva wengi wa daladala hawana shukrani, me nina hiace na nimewapa hesabu ndogo tu walete 30,000 kwa siku na mara zote siku za sikukuu yoyote ile iwe ni Idd, Pasaka au Krismas. Huwa nawaachia siku moja ili wapate hela ya sikukuu, lkn ndugu yangu ni kama kosa. Kila siku ni visa, mara majembe, mara tairi lina pancha, mara pump wakati siku ukiwa free na ukiwakomalia unakuta hamna ugonjwa wowote wa gari na gari bado iko safi kabisa!

Hao jamaa ni wezi hawana mfano! Utakuja filisika and then watakucheka! Inabidi tu utafute tender ya shule, hoteli ... au utafute dereva mwingine mzuri (sijui utamtoa wapi manake kigamboni madereva wote wanajuana pale na ndio tabia yao).

Believe me, njia za kule zina hela sana, si Tungi, Kisiwani, Vijibweni, wala Kibada. Hesabu wanapata ila mtakuwa mnagawana nusu kwa nusu!

Ningekushauri utafute dogo mmoja wa kitaa unayemuamini then asimamie gari yako na yeye ndo akuletee hesabu na uwe unampoza ... me i did the same and it worked out mpaka huyo dogo alipoenda shule then wakaanza upumbavu wao tena. Now nimewatishia kuwatimua ndo kidogo wamejirekebisha lkn ni presha tupu!

pole sana!
 
Vp mkuu sasa umeishia wapi umesha pata tender?

Kama kuna kijana mtaani hana kazi mweke awe konda mambo yataenda sawia sio konda atafutwe na dereva wewe weka mtu wako unae mjua asimamie mauzo huna hata wapambe?
 
Hiyo ni biashara nzuri tu kama ukikomaa!

Hawa madereva ndivyo walivyo, hawaishi sababu ila unatakiwa kuwa mkali. Kama umeshazoeana na hao madereva badilisha ruti kisha tafuta dereva mwingine na usimchekee, inaelelekea wewe mpole sana, hutapata hela ukiwa mpole na ndo maana wenye madaladala wengi ni wanaume kwani ndo wenye roho ngumu, komaa baba, kama ukishindwa mpe mtu akusaidie kusimamia, hata mimi naweza ila ukibadili ruti,
 
Kila shughuri ina headache zake. Hakuna iliyo mteremko, ni kukaza buti tuuuuu. Umeshawahi kusikia tabu ya kuwa na teksi? Tatizo ni kuwa watz tunapenda sana biashara zenye kukuza majina huko uswazi kwetu; ANA HIACE TISA HUYO, ANA KOROLA SABA HUYO ZOTE TEKSI. Kumbe kila kororla la ulinunua Tsh 8M, na unaletewa 10,000/= kwa siku.siku nyingine longolongo kibao na hatari ya kutekwa kwa gari.

Kuna mtu ana guta 3 na anakula 10,000/= hadi 15,000/- kila guta kila siku. Guta moja alinunua Tshs. 400,000/= hadi 500,000/=

kuna mtu ana mikokoteni ya maji 5. kila mkokoteni alitengeneza kwa 80,000/-, anakua buku kila mkokoteni kila siku.

Thanks Ngalikihinja,

Nimepokea challenge ya what matters is not how much you are investing, but the returns!Kwa mtazamo huo guta linaweza kuwa na faida kuliko biashara iliyoku-cost hela nyingi tuu.

I should admit pia kuwa JF ni mahali ambapo napatumia kujifunza mambo mengi sana. Na it was JF that made me set my foot into this bussiness, ambayo honestly I do not think it is that bad. Issue ni management hasa kwa mtu amabaye unafanya monitoring kwa simu.

Mkuu I have been moved by your analyisis on biashara ya guta na mkokoteni! Tunachomiss ni knowledge or rather awareness kuhusu biashara kama hizo ambazo unaweza ku invest less na kupata return ya kueleweka tuu. Maana kupata mtu anayejihusisha na biashara ya guta/mkokoteni ili ujifunze, hilo tuu ni mtihani tosha. Mfano mdogo tuu, si rahisi ukapata thread ndani ya JF inayoongelea kitu kama hicho. May be we are underestimating them kwa sababu unachosema status ya mtaani.

So far, mchango wako wa mawazo na changamoto imepokelewa! Thanks!!
 
yaani sina hamu kabisa na Teksi wala hiace; ni afadhali nikalime miwa tu! nilikuwa na taaksi 2 moja imegongwa dereva akasepa na nyingine kwa kukosa usimamizi nimeiuza kwa hasara; afadhali nimgempeleka mama yangu atembeleaa kwani huenda mpaka leo ingekuwepo! Kibaya ni kuwa inakubidi uache kazi zako ufuatilie hizo gari; sasa huo ni mtadi wa aina gani! Aarrrgh!😡
 
Thanks Ngalikihinja,

Nimepokea challenge ya what matters is not how much you are investing, but the returns!Kwa mtazamo huo guta linaweza kuwa na faida kuliko biashara iliyoku-cost hela nyingi tuu.

I should admit pia kuwa JF ni mahali ambapo napatumia kujifunza mambo mengi sana. Na it was JF that made me set my foot into this bussiness, ambayo honestly I do not think it is that bad. Issue ni management hasa kwa mtu amabaye unafanya monitoring kwa simu.

Mkuu I have been moved by your analyisis on biashara ya guta na mkokoteni! Tunachomiss ni knowledge or rather awareness kuhusu biashara kama hizo ambazo unaweza ku invest less na kupata return ya kueleweka tuu. Maana kupata mtu anayejihusisha na biashara ya guta/mkokoteni ili ujifunze, hilo tuu ni mtihani tosha. Mfano mdogo tuu, si rahisi ukapata thread ndani ya JF inayoongelea kitu kama hicho. May be we are underestimating them kwa sababu unachosema status ya mtaani.

So far, mchango wako wa mawazo na changamoto imepokelewa! Thanks!!

Mkuu ukisoma kati ya mistari katika ujumbe wa Ngali, uandikishaji na utunzaji wa takwimu ndio mhimili mkubwa hasa wa biashara yeyote ile maana ndio inayokuwezesha kujua kipi kilichotoka, ingia, kodishwa, uzwa, kopwa, masaa yaliyotumika n.k . Utakapokuwa na msingi mzuri wa takwimu au rekodi zako ndiyo utaweza kujua kama biashara unayoifanya ina tija au la.
 
pole sana mkuu,
madereva wa daladala ndiyo tabia yao. pole sana!
tafuta tu dereva mwaminifu!

Ushauri:
Wewe mkabidhi gari. Mwambie hii nakukabidhi wewe. Mpunguzie hesabu mpaka labda 35. Kisha mwambie aihudumie kila kitu, Na wewe hutaki kusikia longolongo lolote. Mwambie akupe hesabu ya wiki nzima!

Hayo mambo ya bao, sijui nini ni juu yake, wewe hayakuhusu!

Hapo lazima uwe na roho ya paka la sivyo utakuwa unafanya biashara ya kuuza ubuyu na visheti kila siku!
si utakuwa umemfungia fisi buchani? ndio ataikongoroa kabisa kwa mwezi mmoja tu.Sababu hana uchungu nayo.
 
Back
Top Bottom