Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Ni kweli sema wakati mwingine unakuta kitu hakiulizwi ila ukikileta kinapata mvuto na kinachukuliwa.mfano juice ya ukwaju azam ilikua haiuliziwi lakini baada ya kuileta inachukuliwa.mawazo ya wadau ni muhimu sana
Chukua huu ushauri mkuu.

Huwezi kuchukua assumptions za watu tu, angalia kitu gani kinauliziwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya vyoote lakini KAULI NZURI kwa wateja ni msingi. Maneno kama 'Asante', 'Karibu tena' ni madogo lakini yana maana kubwa sana kwa mteja.
 
ni kweli sema wakati mwingine unakuta kitu hakiulizwi ila ukikileta kinapata mvuto na kinachukuliwa.mfano juice ya ukwaju azam ilikua haiuliziwi lakini baada ya kuileta inachukuliwa.mawazo yawadau ni muhimu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Ntaandika gazeti mkuu [emoji23][emoji23][emoji23]

Ni kweli unachosema ila at least kwa kuanza sio mbaya na kingine unaweza angalia ni huduma gani ambayo wao huifuata sehemu nyingine au la haipatikani kwa ile standard inayohitajika. Ni fursa nzuri pia

Ulisema unaweka shop hivyo nikaunga mkono hoja ya kuangalia nini kinachouliziwa katika shop ili kujua ni nini wateja wanahitaji au kutaraji katika "DUKA"..
 
Weka tigo pesa . M pesa. Mix makava ya simu protector chaja. Utafanikiwa

IMG_20191010_104824.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ni wazo zuri, just ucuze kwakuwa tu wanakuja wa mwaka wa kwanza katika duka lako hkikisha hela haikupiti. Weka kila kitu. Hat kama uknunua kwa uchache lkn hakikisha kiwepo.

Nakumbuka wakat naanza nlkuw nna nia ya kuhakikisha kuwa kila kitu kipo

Yan nkienda mjini hata kama sina pesa nilichukua hata nusu, walau kiwepo!

Hiyo unawawekea imani kuwa hawatakosa kitu kwako.

Leo hii mtu akitafta kitu ambcho wengne hawana, wanamuelekeza kwangu

Ngoja nami nikupe ushauri wangu kwa kipindi ambacho wanaingia wanachuo wa mwaka wa Kwanza (wapya) basi hapo mbele ya duka lako weka meza na uuze vitu vya electronic kama charge, USB, flash drive, Bluetooth speaker, memory card, earphones, cover za simu n.k
Note: Ni kwa kipindi tu ambacho first year wanaingia (biashara ya msimu).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umefungua duka, hongera sana

Ina maana tayari wateja wanakuja na kununua/kuulizia bidhaa mbalimbali

Uwe na daftari pembeni, orodhesha bidhaa zinazouliziwa na wateja wako (kila inapouliziwa weka kumbukumbu)

Baada ya mwezi utafahamu ni bidhaa gani za kuweka au kuongeza hapo dukani kwako hayolae,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok, hebu tusaidiane kufikiri hapa, umesema 90% ya wateja wako ni wanachuo right? sasa ndugu mfanyabiashara wanapokua wamefunga chuo (that's means also 90% ya mapato au mauzo yako yata drop) umejipangaje na kipindi hiko cha mpito wakati wanafunzi hawako chuo ili "ku- balance" mambo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kila siku ni jumapili ila matairi ya gari ndo hayana rangi nyingine zaidi ya nyeusi. Duka siuzi mwenyewe anauza mdogo wangu na kwa miezi miwili na sasa watatu tutaumaliza soon mambo yanaenda kama nilivyosema hapo juu. Bora kuwa positive kwa kutoa changamoto na suluhisho lake. Yes tunajua kama ukiajiri mtu hasa kwa maduka haya anaweza kukuulia mtaji, na si wote wanaweza kufanya hivyo. Mazingira unayoyaweka mwenyewe kwenye duka, na jinsi ulivyo mgroom huyo muuzaji ndo yatakuwa maamuzi wa mwendelezo wa biashara yako.
Aisee I am impressed with your spirit of positivism. Kiukweli watanzania wengi wetu tuna negativity sana hata kwenye masuala ya msingi. Nakupongeza sana na nitakutafuta kwa ushauri zaidi maana na miminiko mbioni kufungua biashara hii ya duka la reja reja.
 
yello masai,

Ni kweli mkuu pole pole tu mambo yanaenda, siku za mwanzo ni issue ila nilipata imani sana kuuza bidhaa za 10,000 kwa siku na kuna siku mauzo yanafika 200,000 kwa siku. Hapo toa tigo pesa na mpesa ambazo commision ya kwanza nilipata jumla 160,000 kwa mwezi.

Mimi bwana naliangalia hili duka kwa mbali sana, nimekula amini sitoi chochote dukani kwa miaka miwili. Faida yote naidumbukiza dukani kununua vinavyohitajika na inayobaki naiweka bank.

Baada ya miaka miwili nitafanya tathmini kuona mwenendo wake ulikuwaje for those two years. Ila so far so good.
Bro salaam na heri ya mwaka 2020. Natumai unaendelea vema na biashara ya duka na kwa sasa umeshaizoea na yenyewe imekuzoea tayari.

Vipi, tathmini inasemaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu faida ya duka la rejareja ni kati ya 10% hadi 18%. Na hilo ni duka gani uuze 300,000 kwa mwezi? Mi nina duka la mtaji 2 mil nauza kati ya elfu 40 hadi 60 kwa siku pia nina genge nauza elfu 25 hadi 40 kwa siku. Na trend ya msuzo inakuwa positively

Kuuza laki 3 kwa mwezi maana yake unauza elfu 10 kwa siku. Hapo unakuwa ulifungua duka bila kupata ushauri au kupiga hesabu zako vizuri
Unaposema nauza let say 50,000 kwa siku. Hiyo ndiyo inakuwa faida au faida ipo ndani humo humo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom