Ukiona mtu anaendesha biashara ya duka rejareja(nadhani vyakula Kama mtoa mada amekusudia hivyo) kwa muda wa miaka 3 na linaendelea vizuri mpe heshima yake.
Hii biashara watu wanaweza sema ni rahisi ila ni biashara ngumu Sana inayohitaji akili maana ukicheza kidogo tu unafunga.
Wengi imewashinda kwasababu hajui njisi ya kuiendesha, kwenye mauzo atataka ale hapo hapo atachota sukari, hapo hapo atachukua sabuni ,chumvi, unga n.k kwa matumizi ya nyumbani ila haesabu , yeye anahesabu alizouza tu na tatizo linaanzia hapo.