Mkuu hongera kwa kuwaza jambo kama hili. kwa miaka ya hivi karibuni washabiki wa masuala ya soka wameongezeka sana hivyo kufanya hii biashara kuwa nzuri kiasi. Niliwahi kufanya kipindi cha nyuma ila naweza kukushauri kulingana na wakati huo ilivyokua. kama una uwezo mzuri anza na projector zipo za bei nafuu sana hadi 850k unaweza kupata, ukiweka hii itavutia watazamaji wengi zaidi kuja kwako kwakua wanamuona mchezaji kwa ukubwa wake halisi na pia itakuasaidia hata anayekaa nyuma kabisa anaweza kuona bila wasi wasi wowote. swala lingine kuwa na decoder zaidi ya moja kwakuwa mara nyingi game za uefa zinapigwa wakati mmoja hivyo usiwanyime wateja wako burudani. Pia zingatia sana sehemu za kukaa ikiwa n viti vya plastic au bench basi liwe confortable kwa mtu kuweza kukaa hapo kwa zaidi ya 2hrs isiwe mteja anakaa kwa shida kesho hatorudi. nashauri utumie bench sababu viti vta plastic vinatumia sehemu kubwa mahali pakuingia bench la watu 15 vitaingia viti 10 tu so ushapoteza watu 5 hapo(utaangalia na ww mwenyewe).
Pia n vizuri mahali hapo ukaweka na biashara zingine ndgo ndgo mfano. kama upo maeneo yenye baridi unaweza kuuza vitu kama gahawa,tangawizi,uji,chai na vitu vingine vya moto moto na kama ni eneo lenye joto unaweza kuuza ice cream,soda na vinywaji vingine baridi visivyo na vileo. kwa kufanya hivi utaweza kuwafanya wateja wako kukaa hapo kwa muda mwingi kipind cha weekend au kila siku jioni.
Ukiwa na muda wa kutosha tembelea moja ya banda ambalo unadhani ndo bora kabisa la mpira na ujaribu kuona jinsi wanavyofanya kazi na tafuta mapungufu yao yawe kama kipaumbele kwako ili kuweza kuwapiku wao na kuwapora wateja. Baadh ya mambo niliyowahi kufanya n kuonesha game za timu ndogo ndgo zile zinazoanza mapema bila kucharge hela ili kuwaacha wajione unawajali. pia lazima uweke mtu anayejua soka la mdomoni kweli kweli akianza ubishi unatrend wiki nzima, na awe anajua historia mbili tatu za kuwafanya wateja waamini wapo old trafod kweli kweli. fanyia kazi hayo kwanza ikitokea unaswali unaeza niuliza hapa hapa tu.