Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Mkuu Mimi hii ni moja wapo ya biashara zangu
Ingawa kwa sasa natumia dish mbili tu

Dstv natumia extra view malipo laki moja na nusu
Na kingine hizi za ndani decoder ya Azam

TV ninazo flat mbili na projector moja
Na jenerator plus sabufa mbili basi

Bei star x mbili nilinunua laki Tisa kila moja 450000
Sabyfa mbili

Moja 200000
Nyingine 90000
Ving'amuzi Azam 145000+ ufundi 30000+malipo ya mwezi 15000

Dstv nilinunua 80000 + ufundi 30000
Kifurushi 150000 kwa mwezi

Ila kabla ya Dstv nilikuwa natumia receiver ya alphabox hii nilinunua 250000 pamoja na Vifaa + ufundi
Dish 200000
Basi
Na banda laki saba tu kulijenga

ILa usiogope anza na ulivyo navyo

Samahan mkuu na mm nipo kwenye maandalizi ya kufungua banda la mpira soon tv unazotumia ni inch ngap?,projector unatumia aina gani na specifications zake zipoje?ulinunua bei gan?na jenerator?
 
Biashara inalipa ila inahitaji usimamizi wa kutosha na ni better usimamie wewe kuliko umuweke rafiki au ndugu mana it costs me a lot pindi nlipomuweka rafiki bali kwa kipindi nlichokua nasimamia mimi as mimi nlikua naiona hela
 
Mkuu hongera kwa kuwaza jambo kama hili. kwa miaka ya hivi karibuni washabiki wa masuala ya soka wameongezeka sana hivyo kufanya hii biashara kuwa nzuri kiasi. Niliwahi kufanya kipindi cha nyuma ila naweza kukushauri kulingana na wakati huo ilivyokua. kama una uwezo mzuri anza na projector zipo za bei nafuu sana hadi 850k unaweza kupata, ukiweka hii itavutia watazamaji wengi zaidi kuja kwako kwakua wanamuona mchezaji kwa ukubwa wake halisi na pia itakuasaidia hata anayekaa nyuma kabisa anaweza kuona bila wasi wasi wowote. swala lingine kuwa na decoder zaidi ya moja kwakuwa mara nyingi game za uefa zinapigwa wakati mmoja hivyo usiwanyime wateja wako burudani. Pia zingatia sana sehemu za kukaa ikiwa n viti vya plastic au bench basi liwe confortable kwa mtu kuweza kukaa hapo kwa zaidi ya 2hrs isiwe mteja anakaa kwa shida kesho hatorudi. nashauri utumie bench sababu viti vta plastic vinatumia sehemu kubwa mahali pakuingia bench la watu 15 vitaingia viti 10 tu so ushapoteza watu 5 hapo(utaangalia na ww mwenyewe).

Pia n vizuri mahali hapo ukaweka na biashara zingine ndgo ndgo mfano. kama upo maeneo yenye baridi unaweza kuuza vitu kama gahawa,tangawizi,uji,chai na vitu vingine vya moto moto na kama ni eneo lenye joto unaweza kuuza ice cream,soda na vinywaji vingine baridi visivyo na vileo. kwa kufanya hivi utaweza kuwafanya wateja wako kukaa hapo kwa muda mwingi kipind cha weekend au kila siku jioni.
Ukiwa na muda wa kutosha tembelea moja ya banda ambalo unadhani ndo bora kabisa la mpira na ujaribu kuona jinsi wanavyofanya kazi na tafuta mapungufu yao yawe kama kipaumbele kwako ili kuweza kuwapiku wao na kuwapora wateja. Baadh ya mambo niliyowahi kufanya n kuonesha game za timu ndogo ndgo zile zinazoanza mapema bila kucharge hela ili kuwaacha wajione unawajali. pia lazima uweke mtu anayejua soka la mdomoni kweli kweli akianza ubishi unatrend wiki nzima, na awe anajua historia mbili tatu za kuwafanya wateja waamini wapo old trafod kweli kweli. fanyia kazi hayo kwanza ikitokea unaswali unaeza niuliza hapa hapa tu.
 
Huu ushaur ni mzur sana watu wanasema sana kwamba uchum umebana but opportunity are there is matter of grabbing them
 
Mkuu biashara hii inalipa sana cha msingi sehemu iwe na mkusanyiko wa watu, nunua dstv dish na decoder yake na unakuwa unalipia kila mwezi kama tsh.80000/-
Pia tafuta wanachama wa kudumu wanakuwa wanalipa tsh.10000/- kwa mwezi, wakiwa 50 sawa na tsh.500000/- achilia mbali wale wa rejareja watatoa 500/- au 1000/- kila mechi.
Huwezi pata mwanachama wa kudumu kwa 10000/= mechi kubwa hazizidi kumi kwa mwezi. 500*10=5000 sasa nan mjinga ivi?? Unless upo kinondoni mpira buku ila sehemu nyingi mpira jero tu.
 
Mkuu hongera kwa kuwaza jambo kama hili. kwa miaka ya hivi karibuni washabiki wa masuala ya soka wameongezeka sana hivyo kufanya hii biashara kuwa nzuri kiasi. Niliwahi kufanya kipindi cha nyuma ila naweza kukushauri kulingana na wakati huo ilivyokua. kama una uwezo mzuri anza na projector zipo za bei nafuu sana hadi 850k unaweza kupata, ukiweka hii itavutia watazamaji wengi zaidi kuja kwako kwakua wanamuona mchezaji kwa ukubwa wake halisi na pia itakuasaidia hata anayekaa nyuma kabisa anaweza kuona bila wasi wasi wowote. swala lingine kuwa na decoder zaidi ya moja kwakuwa mara nyingi game za uefa zinapigwa wakati mmoja hivyo usiwanyime wateja wako burudani. Pia zingatia sana sehemu za kukaa ikiwa n viti vya plastic au bench basi liwe confortable kwa mtu kuweza kukaa hapo kwa zaidi ya 2hrs isiwe mteja anakaa kwa shida kesho hatorudi. nashauri utumie bench sababu viti vta plastic vinatumia sehemu kubwa mahali pakuingia bench la watu 15 vitaingia viti 10 tu so ushapoteza watu 5 hapo(utaangalia na ww mwenyewe).

Pia n vizuri mahali hapo ukaweka na biashara zingine ndgo ndgo mfano. kama upo maeneo yenye baridi unaweza kuuza vitu kama gahawa,tangawizi,uji,chai na vitu vingine vya moto moto na kama ni eneo lenye joto unaweza kuuza ice cream,soda na vinywaji vingine baridi visivyo na vileo. kwa kufanya hivi utaweza kuwafanya wateja wako kukaa hapo kwa muda mwingi kipind cha weekend au kila siku jioni.
Ukiwa na muda wa kutosha tembelea moja ya banda ambalo unadhani ndo bora kabisa la mpira na ujaribu kuona jinsi wanavyofanya kazi na tafuta mapungufu yao yawe kama kipaumbele kwako ili kuweza kuwapiku wao na kuwapora wateja. Baadh ya mambo niliyowahi kufanya n kuonesha game za timu ndogo ndgo zile zinazoanza mapema bila kucharge hela ili kuwaacha wajione unawajali. pia lazima uweke mtu anayejua soka la mdomoni kweli kweli akianza ubishi unatrend wiki nzima, na awe anajua historia mbili tatu za kuwafanya wateja waamini wapo old trafod kweli kweli. fanyia kazi hayo kwanza ikitokea unaswali unaeza niuliza hapa hapa tu.
Nimekuelewa mkuu BT unawez kunisaidia bei ya kulipia dstv na bei ake kukinunua kam hautajal mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hii 80000 haitoshi kama kweli unataka kufanya biashara. Unahitaji tsh 130000 hivi kwa mwezi ili kupata premium bouquet. Aidha decoder 1 huenda ickutoshe, unaweza kutafuta ya pili ambayo ikiunganishwa na ya kwanza itakufanya upate chnl 2 kwa wakati m1. Itakugharimu tsh 150000.
Premium ni TSH 184,000/= kwa sasa
 
Boss bila M4 hutoboi hii kitu Just ione hivyo tu ni shida [emoji23][emoji23][emoji23]
Kweli boss nmepiga hesab sana nkaona costs zinatua hapa... sasa swali ni kwamba itaweza rudi kweli.. ndani ya mda gani..?

Agro Business Iringa
 
Kweli boss nmepiga hesab sana nkaona costs zinatua hapa... sasa swali ni kwamba itaweza rudi kweli.. ndani ya mda gani..?

Agro Business Iringa
unaweza kuirudisha within 2 months mkuu

check this out:
kama una bench 30 za kukaa watu 10, that means 30 x 10 = watu 300

una uhakika wa kupata idadi hiyo ya wateja ktk mechi kubwa kubwa, so nitachukua mechi kubwa za mwezi december 2017;
EPL
december 2
i. chelsea vs newcastle
ii. brighton vs liverpool
iii. arsenal vs man utd

december 9
i. west ham vs chelsea

december 10
i. southampton vs arsenal
ii. liverpool vs everton
iii. man utd vs man city

mechi 1 = watu 300 x tsh. 1000 = tsh 300,000
tsh 300,000 x mechi 7 = tsh 2,100,000

hayo ni mahesabu ya ligi moja tu bado kuna UEFA champions league, la liga (mechi zinazowakutanisha madrid, atletico na barcelona), ligi yetu hapa bongo vodacom premier league, mechi za kirafiki na za kimataifa

ukiwa eneo lenye wateja wengi wa mpira, na mwez wenye mechi nyingi hupungui 3 milion
 
usiogope kuanzisha biashara mkuu itafuatana nawe Tv zako na decoder basi mengine ndani ya mchezo kama hapa tunavyojuzana kuzikwepa baadhi gharama maana dstv anaumiza huyo

boss......nami piua nina idea km hio ; tayari nina samsung inch32 projector sony na band la kuonesha;

vilivobaki naomba muongozo na ushauri niko arusha
 
mm Nina ukumbi wangu Nina wateja wengi tu naonyeshaga kwa jero tu
ukumbi wangu unachukua watu 250, na unajaa sana maana nilianza cku nyingi kwahiyo ninajulikana sana napata faida nzuri tu Nina screen 2
 
boss

hongera ....vp unanishaurije mtu anayeanza kuhusu namna bora ya management vifaa na wateja
 
Back
Top Bottom