Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

hadi project kukamilika inaeza gharimu kiasi gani?

-Tv zisiwe chini ya mbili
-Dstv' set + dekoda ya extra view + Bando lao + 27,500 charges ya extra view
-Azam set +Fundi + Bundle
-Viti/Mabenchi
-Gharama ya kujenga ukumbi au kuukodisha
-Jenereta + wiring yake
-Fundi wa welding na nondo za kuchomelea tv ukutani ili isiwe rahisi sana kumtamanisha mwizi.
-Mlinzi wa eneo
 
Tabora Hiyo Biashara huwezi fanikiwa kuna zile cable wanazotumia Kuangalia Kila Nyumba wanaangalia EPL
 
-Tv zisiwe chini ya mbili
-Dstv' set + dekoda ya extra view + Bando lao + 27,500 charges ya extra view
-Azam set +Fundi + Bundle
-Viti/Mabenchi
-Gharama ya kujenga ukumbi au kuukodisha
-Jenereta + wiring yake
-Fundi wa welding na nondo za kuchomelea tv ukutani ili isiwe rahisi sana kumtamanisha mwizi.
-Mlinzi wa eneo
bando la extra view ni sawa na bando zingine mfano compact plus?
 
wale wadau wa biashara hii tukutane hapa,tupeane uzoefu na maarifa zaidi,

mm nahitaji kujua kwa wadau wabobezi wa biashara hii,je huwa mnatumia projector kuonesha mechi zile za mchana?????? tuanzie hapo

naombea uzi ukawe msaada kwetu sote,nawashukuru sana wachangiaji,

karibuni sana
 
Hongereni kwa michango. Nami Naomba kujua je naweza unganisha decoder na laptop (computer) . Vifaa na Namna ya kuunga. Help me
 
Ni biashara inayolipa sana na sana ila make sure unasimamia wewe mwenyewe na si kumpa rafiki au ndugu. Unatakiwa uwe na vyote Azam for VPL na DSTV na Projector ili iwe rahisi kwa watazamaji kuona + viti vya mbao au mabenchi then umemaliza
mkuu,nipe uzoefu wa kutumia projector wkt wa mechi za mchana.
 
Mimi ilinishinda kwa kukosa msimamizi.
 
mkuu...wewe unatumia projector aina gan? nipe model yake?
Binafsi sina projector ila mimi ni mwanafunzi wa chuo hapa UDOM tunasomea projector mchana kabisa na inadisplay vizuri sana hata ukiwa back bencher .... lakini pia nilikuwa naangalia mechi za saa nane mpaka ikaja saa kumi na moja za WORLD CUP
Ndo maana nikasema unaweza kuangalia mchana ila mazingira yawe ya giza maana hata tukiwa class lazima tufunge milango na mapazia kwenye madirisha yazibwe
 
Back
Top Bottom