Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Fatilia Uzi wa jamaa anaitwa nani sijui ila search mada zake “Biashara ya utumbo” ana avatar ya akwirima.
 
uzi mzuri sana huu, weka projector na flat screen moja kubwa, weka vinywaji, weka zawadi,piga kazi masaa yote siku zote,weka sehemu ya wazi ambapo ni center ya watu wengi,viti viwepo vya kutosha, hii ni biashara nzuri na endelevu, matajiri wakubwa wanawekeza kwenye mpira.
 
Umefafanua vizuri sana.Ila kila biashara ina changamoto zake.Upande huu wa pili hujauelezea kinagaubaga.Je, ni changamoto zipi zinaikumba biashara hii?
 
Biashara nzuri kwanza unatakiwa uwe na banda kubwa lenye hewa pia ufunge mafeni (mapangaboi) pia mabenchi ya kutosha kwa mbele unaweza utandika maturubai tv unatakiwa uwe nazo kuanzia mbili mimi ninazo inch 43 na vinga'muzi unatakiwa uwe navyo kuanzia vinne vya DSTV viwili utamtafuta fundi atakuungia mfumo wa extra view yaani utaonesha mechi mbili kwa wakati mmoja pia unatakiwa uwe na kinga'muzi cha startimes kwa ajili ya mechi za uefa ndogo na cha azam kwa ajili ya mechi za ligi kuu tanzania bara na mechi nyingine mbalimbali.

Mtaji kwa biashara hii unaweza ukaanza na sh m5 ujenzi wa banda milioni 2 tv za flatscreen mbili milioni 1.4 vinga'muzi vinne I mean vya dstv viwili cha startimes 1 na cha azam 1 vitakucost kama laki 7 plus na vifurushi vyake fedha itakayobaki kuna vitu vingine mafeni ya mtumba moja linauzwa sh40,000/*3 itakuwa sh 120,000/ kwa ajili kupunguza joto bila kusahau generator kubwa sh 400,000/ fedha iliyobaki utalipa kodi eneo ulilokodi.
 
Biashara nzuri kwanza unatakiwa uwe na banda kubwa lenye hewa pia ufunge mafeni (mapangaboi) pia mabenchi ya kutosha kwa mbele unaweza utandika maturubai tv unatakiwa uwe nazo kuanzia mbili mimi ninazo inch 43 na vinga'muzi unatakiwa uwe navyo kuanzia vinne vya dstv viwili utamtafuta fundi atakuungia mfumo wa extra view yaani utaonesha mechi mbili kwa wakati mmoja pia unatakiwa uwe na kinga'muzi cha startimes kwa ajili ya mechi za uefa ndogo na cha azam kwa ajili ya mechi za ligi kuu tanzania bara na mechi nyingine mbalimbali
Tuwekee mapato na matumizi.
 
Moja kati ya michezo pendwa sana kwa vijana na hata wazee na watoto kwa ujumla ni mchezo wa miguu, mpira (Football). Ligi nyingi sana zimeanza na zinatarajiwa kuanza ndani ya mwezi huu, huku tayari ligi pendwa ya EPL imeanza kutimua vumbi huku ligi ya Tanzania soon kuanza nayo.

Napenda kuanza biashara hii ya kuonyesha mpira hasa kwa ving'amuzi vya DSTV na AZAM ikiwa kuonyesha mechi za nje ya nchi na ndani hasa timu pendwa za watani wa jadi (Simba na Yanga).

Huu ndo uchambuzi wangu ambao nategemea kufanya makadirio kabla ya kuanza ujenzi na biashara kwa ujumla:
  • Ujenzi wa Banda kwa kutumia Mabati pamoja na umeme hasa kutokana na sehemu niliyopo ni ya kijijini (sio sana) itanigharimu Tshs 900,000.
  • TV ya Kisasa (LED Inch 43) itanigharimu Tshs 900,000.
  • Manunuzi ya Ving'amuzi vyote viwili (AZAM - Tshs 135,000 & DSTV - Tshs 109,000)
  • Jumla = Tshs 244,000.
  • Vifurushi Vya Kujiunga Ndani husika (AZAM PLUS - Tshs 23,000 & DSTV Compact - Tshs 69,000)
  • Jumla = Tshs 92,000.
  • Kabati kwa ajili ya kuwekea/kuhifadhi TV itanigharimu Tshs 85,000.
  • Matumizi mengine ya dharura (Emergency) ndani ya ujenzi ni Tshs 200,000.
Jumla ya Mahitaji na Gharama kwa Ujumla Itanigharimu Kiasi Cha Tshs 2,421,000

Nakaribisha maoni na mapendekezo yenu yaweze kunisaidia mimi pamoja na wanajukwaa wengine wenye malengo kama yangu ya kuanzisha biashara hii.

Asanteni[emoji120]
 
Usisahau feni kama kuna joto, Pia kama utaweka viti vizuri ikawa kama V.I.P.. Nakulotelea mfano;-
Kuna Banda niliwahi kuliona sehemu jamaa ameweka benchi nzuri kama za kanisani kwa kiingilio cha 500 then akaweka mbele kabisa makochi 4 yale ya watu 3 ikawa kama V.I.P kwa kiingilio cha 1500 + free soda.

kuwa na lugha nzuri kwa wateja usisahu Spika kubwa au subwoofer kubwa.


Vinywaji usisahau.
 
Back
Top Bottom