Biashara ya Kuuza Mkaa: Uzoefu, Vibali vya kuchoma, Changamoto na Ushauri

Biashara ya Kuuza Mkaa: Uzoefu, Vibali vya kuchoma, Changamoto na Ushauri

Ndio tunavogawana shilingi yetu.Tutakomaa kama nyie wakulima hamtauza bei za tamaa kubwa,ukishapanga bei za gunia utuguze
 
ni pm ndugu nitakuelekeza vzr2, maana naona watu wanakukatisha moyo mm ndio biashara yangu
 
ndugu tafuta sh@40,000 kwa gunia la kg100 nikuletee mpk nyumbani kwako(jumla)
 
.
Aksante. kwa hiyo hicho kibali cha kuuza mkaa wilayani mwako tunachukulia kwenye ofisi za manispaa mfano temeke pale uwanja wa mpira wa taifa au ofisi za maliasili wilaya?(mimi natarajia kufungua wilaya ya temeke)
Asante kwa mshindonyuma! Fanya kazi usitishiwe, hakuna kazi isiyokuwa na kadhia!
 
Habarini?

Ninaomba kuifaham hii biashara nina mpango wa kufungua stoo ya mkaa nimuweke mtu aniuzie kwa jumla na rejareja.

Naomba kufahamishwa kwa mwenye ujuzi na hili itanigharimu shilingi ngapi hadi kufanikisha hili?

Na je zipi changamoto kubwa nitakazo kabiliana nazo?

Nawasilisha.

Asanteni.

ni pm 2zungumze kiundani
 
Mkuu hebu ni pm picha ya hilo gunia likiwalimesimama nilione tunaweza fanya biashara hapa.

kaka bahati mbaya nimemaliza ila nipo katika maandalizi ya kuleta mzingo ukifika nitakujulisha wala ucjali
 
ndugu tafuta sh@40,000 kwa gunia la kg100 nikuletee mpk nyumbani kwako(jumla)

Nitawezaje kuona hilo gunia?mi nipo dar na ninanunua mengi,niagizie ilipo ofisi nije kuziona hizo gunia?Au ni Pm namba yako ilitupeane maelekezo.
 
du Mimi nipo Nachingwea.... kumbe ninaweza kuwa nawatumia ukawa unauza ......check me mkuu
 
TARATIBU ZA VIBALI KWA MAZAO YA MISITU-MKAA.


1,Hati ya usajili ambayo ni 261000 kwa mwaka hutolewa na ofisi ya misitu wilaya ambayo utafanyia biashara.
2,Hati ya kusafirisha mkaa ni 6500 kwa fuso na 13000 kwa semi ,hii ni kwa kila safari hii hutolewa kula unapochukulia mkaa(shambani).
3,Leseni ya kuvuna mkaa/ushuru wa serikali kuu ambayo ni 8700 kwa gunia la kawaida na 14700 kwa gunia lumbesa,hii ni sawa na 160 kwa kilo 1
4,Ushuru wa serikali ya mtaa ni kati ya 1000 hadi 2000 kwa gunia
5,Leseni ya biashara na tin
6,Uwe na daftari la mauzo kwa ajili ya ukaguzi ukitokea
7,Mwisho wa kusafirisha mkaa ni sa 12 jioni

NAWAKILISHA

masharti ni mengi kuliko baishara ya mbao...!!
 
Juzi nilisikia mkuu wa mkoa wa Pwani akifuta vibali vyote vya kutengeneza mkaa kwa mkoa mzima wa Pwani sasa kama unataka kuuchukulia Pwani lazima uliangalie na hili.
 
1.usajili(meneja misitu wilaya au ofisi ya tfs iliyokaribu nawe 256000+na maombi 5000=261000)
2.ushuru(serikali kuu168/kg(km gunia lina lebo ya kg 90 zidisha )na halmashauri(1000-2000(dfo(au wakala wa halmashauri aliyeteuliwa\idhinishwa) na dfm(kituo kilicho idhinishwa))
3.kibali cha kusafirishia(gari lisilozid tani saba 6500 na linalozid 13500)
4.leseni ya uvunaji(kutokana na eneo la uvunaji mf forest on general land,forest reserve etc)
5.leseni ya biashara(afisa biashara w au manispaa\jiji)
6.TIN(TRA)
 
Back
Top Bottom