Biashara ya madini ni kichaa. Kaka yangu kapoteza milioni 120 mwezi huu nimemkuta ameshaanza kudata

Usemalo ni kweli ila utafiti wa madini ni gharama kubwa sana mkuu, ndo maana wachimbaji wadogo wanachimba kimungu mungu tu boss.
 
Wazungu wanawekeza mabilioni kwenye exploration msifikiri ni kitu kidogo,

Imagine kampuni kama Barrick imeajiri kampuni 3 zote za drilling kwaajili ya exploration na development, uchimbaji madini sio uchimbaji wa choo
Kwa hiyo asilie Jamaa,hizo ni kampuni mkuu,na huyu ni mtu wa kawaida tuu!
 
Ya madini nimeivulia kofia aisee kuanzia leo

Wengi wanaingia with unrealistic expectations wanadhani wataenda leo na kuwa matajiri overnight. Never happening.

120M kwenye madini ni hela ndogo sana itakua alisikiliza wachimbaji wadogo wakamjaza matumaini hewa. Hiyo haikutoi hata kwenye level ya uchimbaji mdogo.

Angeuliza wachimbaji wakongwe hapo Chunya wanafanyaje kazi kabla ya kuingiza hela zake.

 
Kuna Mpambanaji Huku,Alikuwa Na Duka kubwa La Madawa,nyumba,na Gari akauza vyote akaenda Mgodini Bahati Mbaya Mtaji wote ukakata Mgodini Saivi yupo tu Anajipanga upya
 
Bro wako sio mvumilivu kwenye haya maisha. Nilishawahi poteza 270m, ni kweli iliniuma sana. Nilitulia kiume nikaendelea na maisha.

Nilishasahau na kutengeneza zaidi ya hiyo
Pole,mioyo hutofautiana, wataalamu wa Tabia wanajua hayo kwa ufupi kuna sanguine, melancholy,nk ukizujua Tabia hizi hutosumbuka, Wewe utakuwa sanguine Hawa kwa ufupi hawajali matokeo!
 
hatare sana ndo mambo ya kuchukua risk hayo, kuna kupata na kukosa, ukiwaza kupata tu kisha ukakosa lazima dishi licheze kidogo.

Kuna raia alipoteza mil30 kwenye dhahabu akajifungia ndani miezi sita, huyu wa mil120 simpatii picha
Kapotezaje

Ova
 
Kwahiyo Geita Gold na Barrick nao utumia ulozi??
Bro Biashara ya Madini Matambiko ni lazima Alafu usichokijua Wazungu na Wahindi Ni watu noma Sana Kwenye Hizo mambo".

Ndio maana Hata uwe kigagula kiasi gani Huwezi kuiba benki,au kuiba Madini Mgodini".
 
Akirudia tena atapata mzigo wa maana, dhahabu ndio ilivyo..Ukiwa na moyo mwepesi unafirisika jumla.
 
Tatizo kukosa mahesabu ya elimu ya uchimbaji wa madini pamoja na kuchimba kwa kutegemea mikono ya binadamu!
 
Ni bora kubet m 120 angekuwa naweka m1 mechi za Simba au yanga asingekuwa chizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…