granitized
JF-Expert Member
- Jul 5, 2016
- 3,249
- 7,948
Usemalo ni kweli ila utafiti wa madini ni gharama kubwa sana mkuu, ndo maana wachimbaji wadogo wanachimba kimungu mungu tu boss.Wachimbaji wadogo wengi wanafanya kwa kubahatisha, hawafanyi utafiti.
Madini siyo maharage ambayo unapanda sehemu na kuyaona yanavyokua. Kwenye madini, unatafuta kitu ambacho hukuweka wewe wala rafiki yako. Hivyo hatua ya kwanza ni kufanya utafiti, siyo kuchimba. Unachimba baada ya kufanya utafiti, na kujua yako wapi,, kwa kiwango gani.