Biashara ya mashine ya kusaga na kukoboa nafaka- Fahamu bei zake, uendeshaji wa biashara hii pamoja na faida na hasara zake


Ndio kuitumia kwa muundo niliwekwa Mimi unafanya one thing at a time lakini kumbuka mota ya kusaga ni kubwa kuliko ile ya kukoboa

Bei hizo ziko juu sana lakini haswa tumia za Sido kwa vinu mota ndo uingoe Dukani

sijajua unataka gharama za mashine yenye nini na nini. Kuna umeme hapo? 3Phase? Ongezea nyama nikuelewe mkuu
 


Asante mkuu. Kwa sasa ntaanza na sembe na Dona. Ila business plan yangu ya kukuza nataka niwe natengeneza dona sembe na muhogo ndani ya 3years.Kuna masoko flani nafukuzia nchini India ya muhogo. Tuombeane
 
mkuu siku nyingine, kabla y kuweka uzi, jaribu kutafuta kwanza nyuz za nyuma, utapata watu wameshajadili hayo mambo. so usiwe na akiri kama za ccm

kwi!kwi!kwi!kwi!kwi!!,Wewe inaonyesha ni Mh.Ukawa.Mbona unaichukia hivyo CCM?,Vipi walikuchikulia demu nini???.
 

Mkuu hyo mashine ya VFFS inauwezo wa kufunga mifuko mingapi kwa siku, (kufunga,kujaza, na kupima inafanya kazi kwa wakati Mmoja?
 


oh asnte mkuu ngoja nitalifanyia kazi USISITE KUTUVUMILIA TUNAPOKUULIZA MASWALI ZAIDI
 

KUHUSU VINU NIMEKUELEWA ASANTE MKUU MIMI NILITAKA HAPO KWENYE MOTA mfano ya 20hpdukani ni 1.2million je nikiwa na vinu vya kukoboa na kusaga utatumia mota moja au mpaka ziwe mbili na ikiwa moja utakuwa unasubiri kusagisha kwanza ndipo uanze kukoboa au unaweza fanya vyote kwa pamoja PIA JE KUSUKA UMEME INAWEZA COST BEI GANI HASA gharama za nyaya
 
Mi nakushauri tembelea hata kiwanda cha kusaga unga cha bakhresa(azam) kuna vitu utapata.

Hili wazo zuri lakini kabla hujafika kwa hao wakubwa fuata kwanza wazalishaji wa mkoani mwako au kwa dar mmoja yupo pale bunju chapa ya unga ni bora nadhani
 
Kama nijuavyo unapoweka unga kwenye mifuko huwa inachukua miezi michache kuharibika tofauti na makampuni makubwa ambapo unga unakaa hata mwaka bila kuharibika
Sasa we utatumia nini kukausha huo unga ili usiwe na moisture?
 
Mimi kwa kuongezea, ningeshauri ufikirie yafuatayo pia kadri biashara itakavyokuwa:
1. Kupata mashine / teknolojia nyepesi ya kukausha pumba. Uzalishaji ukiwa mkubwa ni dhahiri ukaushaji pumba huenda ukakusumbua kutokana na ufinyu wa nafasi ya kuanika au vipindi vya mvua. Hivyo, kuwa na njia ya kukausha pumba kutasaidia pumba kutokuoza au kuungua. Kumbuka, mauzo ya pumba yanasaidia sana kucover gharama za uendeshaji mfano umeme, vibarua, kodi (kama zipo) n.k

2. Fikiria pia kuwa na product ya dona (iliyofungashwa) ili kupata soko la walaji wa dona.

3. Pia, fikiria kuanzisha uongezaji wa virutubishi (zinc, vitamin A, B12 nk) kwenye unga wako wa sembe ili kuufanya kuwa wenye lishe zaidi. Hii kuna kipindi TFDA walitaka kuifanya iwe lazima (sijui iliendaje). Pia, kwa wazalishaji wakubwa wa unga wa ngano nafikiri ni lazima sasa kuongeza virutubishi (tazama mifuko yao utaona "fortified". Kumbuka, utapiamlo ni janga la kitaifa.

Embu ngoja nipate kahawa kidogo labda nitapata vingine vya kuongeza.
 
endelea.mimi niko dodoma nafanya ufugaji.washindani ni wachache ivyo soko linaruhusu ila zingatia zaidi ubora wa bidhaa na huduma na muda.Taasisi za kukopesha pia ni nyingi hata hapa dodoma zipo.mimi pia ninampango wakuamia kwenye kilimo cha biashara soon.
-- ushauri usibase kwenye huduma 1 au biashara 1 tu na hasa kwa mikoa yenye uchumi mdogo na unaoibukia.kimbia na muda tafuta mikopo anza kukamua ba alizeti au wekeza na kwenye biashara nyingine.mikoa kama hii ndo rahisi sana kutusua kwa uwekezaji wakati na mkubwa.
 
Hongera sana, Kuna mtu ameshauri hapo kuhusu kuwa na mtu wa Marketing. Napenda pia kushauri kuwa na watu wa marketing kwa kila mkoa kwa kuanzia angalau DSM, PWANI, sijajua kwa huko mikoani..

Ambao kila kwanza utawapa jukumu la kutengeneza Market Plan iliyoshiba kwa kuelezea na vitendo kuanza haraka juu ya vyanzo vya masoko. Kwa DSM waanze negotiations na shule ya Private, Cafterias za vyuoni mf. DUCE, UDSM, ARDHI, IFM, CBE, DIT, ST JOSEPH, TIA, ST MARK'S, MNMU nk.

Pia kufungua ofisi mbalimbali kwa kila maeneo yenye hizo nafaka. mf. Mbagala, Tabata, Buguruni, Gongolamboto, Temeke, Kigamboni, Mbezi, Kimara, Mwenge, Makumbusho, Magomeni, n.k. Promotion katika vyombo vya habari, kutafuta airtime za mahojiano na TV's au Redio.

Lakini mwisho wa siku kumbuka kutembelea VITUO VYA WATOTO YATIMA angalau kuwapa hizo nafaka. Kumbuka pia promotion nyakati za sikukuu. ALL THE BEST.
 
Kaka Hiyo n hatua moja nzur sana ktk maendeleo mm nlikua na idea Hiyo nlikua cjui naanzia wap Leo nmepata mwelekeo itakua vzur kama Nkipata mawasiliano yako
 
Hi mwana ifm naomba nije kwako unipe mwongozo mi nimemaliza banda na machine zipo ila sijui pa kununua mahindi lakin pi a na Fundi wa umeme.. 0784800989
 
Fundi wa kuja kuzifunga hizo machine
 
Tunashukiru kwa kutujuza wengine tunajifunza biashara ya nafaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…