Habari za jioni wakuu
Ninaombeni mawazo yenu. Niko kwenye mchakato wa kuanzisha kiwanda rasmi cha kusaga na kufungangasha unga wa nafaka mbalimbali. Nina mashine ya kusaga mahindi mkoani Dodoma na nilikua nafunga na kuuza unga kienyeji vijijini. Sasa nimeamua kuifanya iwe rasmi kabisa na Mungu akisaidia January 2016 bidhaa zangu zitakua sokoni. Niliyofanya mpaka sasa?
1. Mashine ya kukoboa na kusaga
Tayari ninayo na inatoa huduma
2. Mashine ya kupima, kufungasha na kufunga niliagiza kutoka China na iko kwenye hatua za mwisho za kuwa installed
3.Nimeshaanza mchakato wa kupata vifungashio kwenye kiwanda kimoja Bagamoyo. Mifuko ya kilo 5, 10 na 25 yenye nembo.
4.Stock ya mahindi ninayo karibia tani 10
5.Niko kwenye hatua za mwisho za kupata kibali cha tbs.
Kwa wazoefu wa biashara hii naomba kama kuna mwenye mchango wa ziada tushauriane mpaka hapo nilipofikia. Na kama kuna kitu kingine chochote kinahitajika.Tunaweza wasiliana hapa kwa michango au anymore business ideas/patnership na masoko zaidi.Au hata kwa PM
Shukran.
Mjasiriamali