Biashara ya mifugo (ng'ombe, mbuzi, kondoo n.k)

Mkuu commoro na Syshells kuna soko zuri la wanyama hai hasa ng'ombe. Hata hivyo kufanya biashara hiyo huhitaji vibali kadhaa vya serikali, mtaji mkubwa kidogo pamoja na usimamizi mathubuti ya biashasha ili kuepuka uwezekano wa kutapeliwa au wanyama kuathirika kabla ya kufika sokoni au kufika wakiwa wamepungua ubora. Kama unataka kufanya biashara hiyo nicheki PM
 
weka hapa na wengine tunufaike mdau maana wazo zuri sana hili aise
 
Asante mkuu, nakukuta huko PM.
 
Pm za nini sasa wekeni darasa tufaidike wote hapa
 
Pm za nini sasa wekeni darasa tufaidike wote hapa
Mkuu si kila kitu kinafaa kumwambia kila mtu na wala si kila mtu anahitaji kujua kila kitu, pia si kila kitu kinafaa kusema kila mahali na ndio maana kukawa na PM. Hata hivyo kama kuna kitu unataka kukijua specifically, unaweza kuuliza na kama kuna ninachojua nitakufahamisha.
 
Nahitaji elimu juu ya biashara ya mbuzi kutoka kwa watu wenye experience na biashara hiyo.
1.ununuaji wa mbuzi Mikoani na kuleta dar es salaam.
2.Mikoa yenye mbuzi wengi.
3.Masoko ya mbuzi dar es salaam na nje ya Tanzania.
4.usafirishaji wa mbuzi
 
Mwenye elimu ya hii kitu atujuze tafadhali
 
Ununuzi wa mbuzi unategemeana na wapi unanunulia kwa mfano handeni kipindi cha kulima wanauzwa mpka 25000 kwa mbuzi, Soko la mbuzi kubwa sanaa dodoma kuna kiwanda kinanunua nyama ya mbuzi, kwa dar ni pugu mnadani na vingunguti
 
na kuwasafirisha ni usaniii mkubwa
 
Mnachozungumza ni kweli kuhusu kununua ng'ombe kwenye minada na kuwanenepesha kasha kuwauza sehemu kwenye soko kubwa kama Dar. Ninarafiki yangu aliwahi kunishirikisha hii biashara ila sikuifanya kutokana na kutingwa..ila ninaeneo la kama eka 20 ambazo niko mbioni kuongeza zifike angalau 50 kwa ajili ya shughuli hizi za kilimo na ufugaji..sasa naanza kupata wazo la kunenepesha ng'ombe pia maana kuna wasukuma na warundi kibao kupata ng'ombe sio ishu tena sometimes wanakupa hadi ng'ombe wa zawadi. Ni fursa kubwa hii
 
1. Biashara ya mazao sio lazima ufanye usanii ndio upate faida..mazao yana faida sana tu
2. Sio lazima watu wote wafanye biashara ya kuongezea bidhaa thamani...kwani watu wanavoenda kuleta nguo kutoka China na kuziuza kariakoo wanaongeza nn...lakn faida wanapata
 
Sasa wote wakifanya biashara ya kuchinja nani atanunua ng'ombe na kuleta machinjioni...kuna watu ambao wao wamespecialize kununua hapa hataki hassles za kusafiri kwenda kutafuta ng'ombe huko maporini...ndo mana kuna specialization...na hapo sasa unauliza kama hao wanaochinja wanatilia maanani hyo mikia au ngozi au manyoya...mtu anaspecialize kwenye kile kitu ambacho anaona atakiweza na kitampa faida...sasa wewe udeal na nyama...kongoro mkia ulimi pembe...huwezi kuwa expert wa kutafuta masoko yote hayo..muuliza swali anataka kuspecialize kununua na kuuza ng'ombe kama walivyo kinachoongeza thamani hapo ni kuwatoa sehemu yenye more supply na kuwapeleka sehemu ambayo kuna more demand. Hyo ya kuchinja siyo mbaya ila ni option nyingine na siyo usanii.
 
Umenichekesha sana eti NG'OMBE WA KUSWAGWA...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…