Mkuu Biashara zote ni ghalama, na kuongeza thamani ndo mpango mzima, Ukinunua MCHELE KUTOKA MBEYA UKALETA DAR, ili upate faida ni lazima ufanye usanii wa kuchakachua MCHELE wa mbeya unachanganywa na wa Morogoro na hata saa zingine unachanganywa na MCHELE WA NJE YA NCHI KUTOKA PAKSATAN NA THAILAND,
Bila kuongeza thamani huwezi fanya Biashara yenye Tija hata siku moja, na si lazima uanze na mitaji mikubwa mkuu, hii ya kuuza mchele au mahindi kama yalivyo ni unyonyaji na hakuna faida inayo patikana,
Chukulia mfano Kahawa Ya Tanzania au Pamba, PAMBA INAPELEKWA NJE INATENGENEZA NGUO THEN TUNARUDISHIWA KUUZIWA KWA BEI GHALI,
Ni uvivu wetu tu lakini hakuna kisicho wezekana ni kuweka mikakati