Biashara ya mifugo (ng'ombe, mbuzi, kondoo n.k)

Biashara ya mifugo (ng'ombe, mbuzi, kondoo n.k)

Mkuu Biashara zote ni ghalama, na kuongeza thamani ndo mpango mzima, Ukinunua MCHELE KUTOKA MBEYA UKALETA DAR, ili upate faida ni lazima ufanye usanii wa kuchakachua MCHELE wa mbeya unachanganywa na wa Morogoro na hata saa zingine unachanganywa na MCHELE WA NJE YA NCHI KUTOKA PAKSATAN NA THAILAND,

Bila kuongeza thamani huwezi fanya Biashara yenye Tija hata siku moja, na si lazima uanze na mitaji mikubwa mkuu, hii ya kuuza mchele au mahindi kama yalivyo ni unyonyaji na hakuna faida inayo patikana,

Chukulia mfano Kahawa Ya Tanzania au Pamba, PAMBA INAPELEKWA NJE INATENGENEZA NGUO THEN TUNARUDISHIWA KUUZIWA KWA BEI GHALI,

Ni uvivu wetu tu lakini hakuna kisicho wezekana ni kuweka mikakati
Kwa hyo unashauri nn wa mfano hatuna viwanda au teknolojia ya kubadirisha pamba kuwa nguo ile pamba wanayolima wakulima tuwaachie wakae nayo au tununue na ku export hata kwa faida kidogo? Maana unavyoongea ni kama hatuwezi kuyaongezea thamani basi tusifanye hyo biashara...issue ya kuongeza thamani siyo ngeni tunaijua lakini kama huna uwezo huo kwa sasa pamba isiuzwe?
 
Sasa wote wakifanya biashara ya kuchinja nani atanunua ng'ombe na kuleta machinjioni...kuna watu ambao wao wamespecialize kununua hapa hataki hassles za kusafiri kwenda kutafuta ng'ombe huko maporini...ndo mana kuna specialization...na hapo sasa unauliza kama hao wanaochinja wanatilia maanani hyo mikia au ngozi au manyoya...mtu anaspecialize kwenye kile kitu ambacho anaona atakiweza na kitampa faida...sasa wewe udeal na nyama...kongoro mkia ulimi pembe...huwezi kuwa expert wa kutafuta masoko yote hayo..muuliza swali anataka kuspecialize kununua na kuuza ng'ombe kama walivyo kinachoongeza thamani hapo ni kuwatoa sehemu yenye more supply na kuwapeleka sehemu ambayo kuna more demand. Hyo ya kuchinja siyo mbaya ila ni option nyingine na siyo usanii.
Aseee nakushukuru kwa kuandika kwa ufasaha nikichokifiria
 
Mkuu kwani sisi hatuwezi kuwauzia Nyama? ni mpaka tuwauzi ng'ombe mzima? au tunawauzia ng'ombe wachinje wachukue ngozi theni watengeneze viatu waje kutuuzi kwa bei ya ng'ombe?

Masoko ya ng'ombe yako mengi sana hapo kenya tu kuna soko la kufa mtu,

Ila kule kenya wao wanafaidi zaidi kwenye ngozo na product zingine.


HILI LA DUBAI NA QATAR SI LA MCHEZO WAKUU SI RAHISI KAMA MNAVYO FIKILIA, SI SWALA LA KUPAKIA NG'OMBE KWENYE MELI NA KUPELEKA KULE.

HAWA MPAKA WAKUPE KIBALI CHA KUINGIZA NG'OMBE KWAO SI SWALA LA KITOTO NA SI SWALA LA MWAKA MMOJA
WANAANGALIA VITU VINGI SANA, WANAJARI AFYA ZA WATU WAO SI HUKU BONGO TUNALETEWA SAMAKI WA NYUKILIA THEN TUNAAMBIWA NI SALAMA

BAADHI YA VITU WANAVYO CHEKI

1. MAHALI NG'OMBE WANAKO TOKA/SHAMBA/RUNCH
2. UTUNZWAJI WAO
3. MADAWA WANAYO PEWA/ AINA YA MADAWA WANAO TIBIWA NAYO KAMA HAYANA MADHARA
4. CHAKULA WANACHO PEWA

HUWEZI OKOTELEZA NG'OMBE KWENYE MINADA YA SHINYANGA HALAFU UTARAJIE KUWAPELEKA DUBAI, NI NDOTO MKUU, HAPA LAZIMA UWE NA SHAMBA LAKO NA UNAKUWA UNAWATUNZA MWENYEWE NA HAPO NDO UNAWEZA KU EXPORT
NA KIBALI WANATOA WAO SI KWAMBA UNACHUKULIA HAPA DAR KIBALI

WALE WANAANGALIA SANA QUALITY YA NG'OMBE, NA SANA SANA WENYE RUNCH NDO WANAO WEZA KU EPORT HUKO NA SI HAWA NG'OMBE WA KUSWAGA NA KUPIGWA NA FIMBO

- HUWEZI BEBA NG'OMBE KUTOKA SHINYANGA NA TREN AU MALORI AU KWA KUWASWAGA UFIKISHE DAR UTARAJIE KUWAPAAKIA MELI UWAPELEKE DUBAI, UTARUDI NAO
Mkuu hii ya Dubai siyo kweli! Masharti uliyoorodhesha hapo ni ya watu wa EU hawa ndo wana masharti ya kufa mtu. Hao Waarabu wako wanabugia nyama ya kutoka Tanzania kama hawana akili nzuri. Unajua wale jamaa wanaochinja pale Dodoma wanachukua mbuzi kutoka Usukumani na kuwachinja kisha kuwasafirisha kwenda Uarabuni? Hata nyama ya ng'ombe niliwahi kuongea nao wakanipa utaratibu kabisa wa ku-supply nyama kwao ili waunganishe na order yao ya kupeleka Uarabuni. Walisema soko wanalo kubwa sana lakini wameshindwa kulitimizia matakwa kutokana na kuwa na supply ya ng'ombe. Hivyo hata kama unanenepesha huku Usukumani unaweza kuwauzia!
 
Mi nna jamaa yangu ananunua ng,ombe usukumani kipindi cha ukame hadi ng,ombe mmoja kwa laki anawanenepesha kwa miezi mitatu then anawapeleka visiwani kuanzia zanzibar,comoro na kwingineko yeye ana protection ya wakubwa so huwa ananenepeshea huku rufiji kwenye mbuga ya serous anapiga pesa balaa na wakubwa wana ng,ombe zao humo humo na anasema ng,ombe comoro anauzwa milioni nne mmoja
 
Mi nna jamaa yangu ananunua ng,ombe usukumani kipindi cha ukame hadi ng,ombe mmoja kwa laki anawanenepesha kwa miezi mitatu then anawapeleka visiwani kuanzia zanzibar,comoro na kwingineko yeye ana protection ya wakubwa so huwa ananenepeshea huku rufiji kwenye mbuga ya serous anapiga pesa balaa na wakubwa wana ng,ombe zao humo humo na anasema ng,ombe comoro anauzwa milioni nne mmoja
Umenipa somo,mkuu!
 
Nimejifunza kitu hapa juu ya biashara ya mifugo ,
 
Nyie mnataka kuingilia mabizines ya wakubwa. Tip; KUNA SOKO ZURI DUBAI, QATAR NA HATA SAUDIA. Lkini kumbuka kuna wakubwa ambao ndiyo wameshilia mabiz hayo.
Who's mkubwa bwana? Mkubwa kwake Kwa mke wake hivi haya mambo ya kuuoga ya kizamani yapo?
 
Nahitaji taarifa za kusafirisha nyama ya mbuzi from Tanzania to Dubai.
0758216498
 
kuwapata hao wacomoro mpaka uwe na connection na wafanyabiashara wanaouza ng'ombe pale pugu.

Kuna kipindi nilikua nafanya nao kazi,nafahamiana nao wengi ngoja nikipata mda nntawacheki wanipe update.
Mkuu bado una hizo connections?
 
Habari ndugu, marafiki na jamaa!!, naomben ushauri juu ya biashara hii ya ng'ombe, mbuzi au kondoo kuhusu soko na gharama za usafiri kutoka Ruvu(pwani) hadi sokoni!!, lakin si mbaya kama kuna mfanyabiashara hiyo akashirkiana nami!!!. huwa mm nanunua kwa wafugaji na kuuza kwenye masoko ya huku porini ambayo hayana bei!!.
Nipigie 0786 272120
 
Biashara ni ngumu, nilikuwa mbioni kuifanya, nikafatilia sana vibali na process zote, mwishoni nilinyanyua mikono.
Kifupi fanya mambo mengine.
1) wizara ya mifugo - ukaguzi ,viwango, chanjo ,
2) wizara viwanda na biashara - leseni , vibali.
3)meli za wanyama - sehemu maalumu ya kuwapakilia.
4) oder ya huko unakopeleka - import permit, -viwango wanavyotaka na chanjo.

Mkuu. Ni pasua kichwa.
 
Biashara ni ngumu, nilikuwa mbioni kuifanya, nikafatilia sana vibali na process zote, mwishoni nilinyanyua mikono.
Kifupi fanya mambo mengine.
1) wizara ya mifugo - ukaguzi ,viwango, chanjo ,
2) wizara viwanda na biashara - leseni , vibali.
3)meli za wanyama - sehemu maalumu ya kuwapakilia.
4) oder ya huko unakopeleka - import permit, -viwango wanavyotaka na chanjo.

Mkuu. Ni pasua kichwa.

Hongera sana mkuu.

At least umethubutu kiongozi ni wachache sana wenye moyo wa kuthubutu.

Safi sana.
 
Back
Top Bottom