Biashara ya mifugo (ng'ombe, mbuzi, kondoo n.k)

Kwa hyo unashauri nn wa mfano hatuna viwanda au teknolojia ya kubadirisha pamba kuwa nguo ile pamba wanayolima wakulima tuwaachie wakae nayo au tununue na ku export hata kwa faida kidogo? Maana unavyoongea ni kama hatuwezi kuyaongezea thamani basi tusifanye hyo biashara...issue ya kuongeza thamani siyo ngeni tunaijua lakini kama huna uwezo huo kwa sasa pamba isiuzwe?
 
Aseee nakushukuru kwa kuandika kwa ufasaha nikichokifiria
 
Mkuu hii ya Dubai siyo kweli! Masharti uliyoorodhesha hapo ni ya watu wa EU hawa ndo wana masharti ya kufa mtu. Hao Waarabu wako wanabugia nyama ya kutoka Tanzania kama hawana akili nzuri. Unajua wale jamaa wanaochinja pale Dodoma wanachukua mbuzi kutoka Usukumani na kuwachinja kisha kuwasafirisha kwenda Uarabuni? Hata nyama ya ng'ombe niliwahi kuongea nao wakanipa utaratibu kabisa wa ku-supply nyama kwao ili waunganishe na order yao ya kupeleka Uarabuni. Walisema soko wanalo kubwa sana lakini wameshindwa kulitimizia matakwa kutokana na kuwa na supply ya ng'ombe. Hivyo hata kama unanenepesha huku Usukumani unaweza kuwauzia!
 
Mi nna jamaa yangu ananunua ng,ombe usukumani kipindi cha ukame hadi ng,ombe mmoja kwa laki anawanenepesha kwa miezi mitatu then anawapeleka visiwani kuanzia zanzibar,comoro na kwingineko yeye ana protection ya wakubwa so huwa ananenepeshea huku rufiji kwenye mbuga ya serous anapiga pesa balaa na wakubwa wana ng,ombe zao humo humo na anasema ng,ombe comoro anauzwa milioni nne mmoja
 
Umenipa somo,mkuu!
 
Nimejifunza kitu hapa juu ya biashara ya mifugo ,
 
Nyie mnataka kuingilia mabizines ya wakubwa. Tip; KUNA SOKO ZURI DUBAI, QATAR NA HATA SAUDIA. Lkini kumbuka kuna wakubwa ambao ndiyo wameshilia mabiz hayo.
Who's mkubwa bwana? Mkubwa kwake Kwa mke wake hivi haya mambo ya kuuoga ya kizamani yapo?
 
Nahitaji taarifa za kusafirisha nyama ya mbuzi from Tanzania to Dubai.
0758216498
 
kuwapata hao wacomoro mpaka uwe na connection na wafanyabiashara wanaouza ng'ombe pale pugu.

Kuna kipindi nilikua nafanya nao kazi,nafahamiana nao wengi ngoja nikipata mda nntawacheki wanipe update.
Mkuu bado una hizo connections?
 
Nipigie 0786 272120
 
Biashara ni ngumu, nilikuwa mbioni kuifanya, nikafatilia sana vibali na process zote, mwishoni nilinyanyua mikono.
Kifupi fanya mambo mengine.
1) wizara ya mifugo - ukaguzi ,viwango, chanjo ,
2) wizara viwanda na biashara - leseni , vibali.
3)meli za wanyama - sehemu maalumu ya kuwapakilia.
4) oder ya huko unakopeleka - import permit, -viwango wanavyotaka na chanjo.

Mkuu. Ni pasua kichwa.
 

Hongera sana mkuu.

At least umethubutu kiongozi ni wachache sana wenye moyo wa kuthubutu.

Safi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…