Biashara ya movies za nje ni πŸ”₯ sana Kkoo, ni nini kiliua soko la filamu za Tanzania?

Nimeangalia moja mtandaoni jana inaitwa Chumba cha Msukule, safi sana na imafikirisha mno.....ila ndiyo hivyo wapumbavu wamesha haribu njia kiasi kwamba wengine wanashindwa kupita.
Uliiangalia wapi mkuu
 
I second you mkuu, hamna muvi za kidwanzi kama bongomuvi. Kwanza Ni low budget muviz na wahusika wanashindwa kuvaa uhusika kweli, story ukiangalia dk.5 unajua kabisa mwisho wake ukoje. Quality mbovu, yaan ukishoot na ProMax ngoma inaweza ikawa Kali zaidi.
 
Sijui ata wanapata wapi hela hawa wabongo movie. Maana hakuna raia anaenunua kazi zao.

Kuna siku nimetoka Mlimani city, nakutana na mshikaji kanisalimia. Nikajua ananifahamu. Nakuta ananionesha CD yeye ni msanii sasa wanauza yaani anauza kama pipi eti nimsapoti. Mi nikamwambia ata CD player sina naangalia Netflix.
 
Yale maandamano na Dr. Bashite hayakusaidia?
 
Uko sahihi 100%.
 
Tatzo sio mabando tatzo ubora wa movies za bongo haujakizi ili kuwekawa Netflix
 
Mm niliacha toka Kanumba alivyokufa
 
Tatzo sio mabando tatzo ubora wa movies za bongo haujakizi ili kuwekawa Netflix
Sikumaanishe waweke movie zao Netflix, ubora uko chini bali watengeneze streaming platform kama Netflix maana shida kubwa ya Bongomovie kwa sasa ni kukosa platform ya kuuza kazi zao.
 
😁😁😁
 
Sikumaanishe waweke movie zao Netflix, ubora uko chini bali watengeneze streaming platform kama Netflix maana shida kubwa ya Bongomovie kwa sasa ni kukosa platform ya kuuza kazi zao.
Yan una bidhaa mbaya alaf et usingizie sokon unabaguliwa kwaiyo unataka utengenze genge lako peke yako kwel? Kwanza waboreshe movie zao waendane na soko ndio waanzishe platform yao
 
Comedy pia bado bado ukiangalia za Kenya ndio utajua sisi bado
 
Yan una bidhaa mbaya alaf et usingizie sokon unabaguliwa kwaiyo unataka utengenze genge lako peke yako kwel? Kwanza waboreshe movie zao waendane na soko ndio waanzishe platform yao
Huwezi kutoa movie nzuri au bora kwa bajeti kubwa kama huna sehemu ya kuuzia. Shida kubwa ya bongo movie kwa sasa ni namna ya kuuza na kukabiliana na uharamia. Hapo miaka kadhaa watu wengi walitumia CD, bongo movie walipata hela na pengine hadi sasa wangekuwa wameimprove sana. Ghafla CD zikawa ishu za kizamani na watu wakaanza kupirate kazi zao, ikawa hailipi tena. Ndiyo sababu za kutengeneza movie mbovu kwa bajeti za laki nane.

Na pia hata kama wanatoa kitu quality hawataweza uza netflix sababu ya watanzania na kumudu gharama za bando.

Ndiyo maana nimeshauri labda waanzishe streaming service isiyotumia bando, waanzishe channel ya tv ya kulipia.
Watu wanawekeza pesa ndefu kwenye movie na kutia vitu bora kwa sababu zinalipa na wana uhakika wa soko, bongomuvie imekosa hicho kitu, pamoja na mambo mengine, hili nalo ni chanzo kikubwa cha kutoa movie za kijinga.
 
Hakika, wanachojua ni kugombania madem tu
 
  • Ubunifu hafifu
  • Umaskini (kukoswa mbinu za kutafta wazamini)
  • Kupeana nafas kwa kuangalia umaarufu na sio ubora wa mtu kwenye nafas husika.
  • Matumiz madogo/ kitokuwa na matumiz ya technology katika kupendezesha movie zao.
  • Kufeli kuchagua location nzuri kwaajir ya scenes za movie zao
  • Kufanya kaz kwa mazoea.
Kwa dunia ya sasa lazma ujitaid kufanya movie nzur na yakuvutia kuanzia story, characters, location na ubunifu wa hali ya juu na matumiz ya technology pia ni mhimu, wenzetu wanatumia teknolojia kuanzia kwenye kutengeneza location, kutengeneza characters, kutengeneza na kurekebisha actions zote zinazotokea kwenye movie(hapa kwetu sasa ndio panatia kinyaa et mtu kafa lakin unaona anapumua kifua kinapanda juu na kushuka) ushauri wangu waanze kujifunza /ama watafte wataalam wa VFX pia itawasaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…