Cha kwanza na kianze, niliwadharau wasanii wa bongo movie kwa sababu waliamini na wanaamini tuliojiajiri kwa kuuza seasons zilizotafsiriwa tunawaharibia soko lao.
Anyway, nimeshaangalia filamu nzuri zilizozalishwa hapa Tz.
Nimeangalia Shamba Kubwa, The Witness, Girlfriend, Fungu la Kukosa, Nsyuka, In The House, Bongo Kung Fu (ni komedi hii) Mzee Toboa Tobo, Siri ya Kijiji na Kigodoro ni filamu za kizazi cha karibuni ambazo niliweza kuziangalia.
Tulikua na Sultan Tamba na Musa Banzi, Tamba alikua amewekeza kwenye horror movies Tamba alikua ndiyo Jason Blum wetu Banzi alikua mzuri katika drama. Unaiangalia Fungu la Kukosa unampenda Riyama, unampenda lead xcter wa kiume na la msingi zaidi unapenda script.
Nakubaliana na
Lizzy ya kwamba bajeti ni finyu lakini filamu zetu nyingi hua zinafeli mno katika script na casting. Kanumba na Kigosi wakafanya ya kwamba ni lazima mtu ambaye ni 'mrembo' awe muigizaji, ni lazima mlinzi awe kituko, ni lazima ukiwa unaigiza upige kelele, ikawa ya kwamba kwakua wewe ni director basi wewe lazima uwe lead xcter, ikawa lazima wapaka wave na super black wawe lead xcter wa kiume.
Una kipaji? Ndiyo.
Unahisi wewe ni handsome/ mzuri kwa viwango vyetu? Hapana.
Utakua housegirl/ mlinzi. And make sure unaonekana huna akili sawasawa.
Una kipaji? Hapana.
Ila wewe ni Hemedy PHD? Ndiyo.
Can you just hang around, look important and keep on saying "Na still bado ..." ? Yes.
Wewe ndiye lead xcter.
Anyway, Tamba akaja akakaa kushoto, Banzi akaanza kuigiza, jamaa ni mzuri kudirect na kuandika script kuliko kuigiza, ilikua ni upuuzi ambao hakutaka kuuacha mpaka akatemana na career yenyewe (nafikiri)
At one point nikawa siangalii filamu zozote za Tz zaidi ya za vichekesho, nikawa nakutana na swala lile lile script na casting ni hovyo. Kuna filamu moja mimi nilishuhudia utengenezwaji wake muongozaji alikua mchekeshaji anaitwa Mkono Mkonole, wale jamaa walikua wanadevelop script hapo hapo kwenye set as in Mkono anamuambia cast wake "Ukifika pale wewe sasa simama halafu anza kumlazimisha akulipe deni lako, yaani ongea tu onyesha umekasirika" ilikua si mchezo.
Kisha kuna zile filamu za Al Riyamy, kuna zile zinaitwa Inye, ilikua ni kutoa filamu zinazohusu matako sehemu ya kwanza mpaka ya nne hivi. Na swala ni moja, mtu ataona matako atashangaa atajikwaa kisha hakuna kinachofuata yaani vipande hivyo hivyo vinaungwa na kuungwa kisha inakua filamu na hawa walitarajia wasogee kimataifa? Kweli?
Kisha zikaja hizi seasons zilizotafsiriwa script ya kawaida ila inaeleweka Ray + Wasanii wakamtrick Nape kwamba zile zinaharibu soko lao, Nape akatuita baada ya kueleweshana akasema haoni sababu ya kuzifungia kwakua hawajaprove ni kivipi zinaharibu soko lao. Wakamgeukia Makonda na Siro vifaa vikakamatwa (PC na kila watakachokukuta nacho) mwisho Msama na Makonda na Siro wakasema hizi filamu hazilipi kodi so tufanye moango zilipe kodi.
As in ile series ya 24 uliyoidownload na kuitafsiri unailipia kodi ili kuiburn na kuiuza kwa wananchi. Tukauliza hii kodi tunayolipa hapa itawafikia hawa tunaodownload muvi zao? Wameshindwa ona kwanini hizo series zilisurvive hata hicho kimbunga?
Script & Casting ni jibu. Filamu zingine zina worse editing ila hamu ya kutaka kujua nini kitafuata inafanya wateja wasiache kuifuatilia. Katikati ya kuvutana na Makonda na Siro Kigosi akatoa filamu inaitwa Watchman (Sina uhakika na jina) ilikua inahusu Kigosi kua mlinzi. Kaka yangu akasema "Waweza kuta humo jamaa anakua mlinzi halafu anamega familia nzima" guess what? Niliambiwa hicho ndicho kilichokuemo.
Kwa upande wangu naamini bajeti kama factor kuna namna unaweza ukaiignore mfano kuna filamu nyingi zimezalishwa kwa bajeti ndogo Rocky, The Clerk n.k. na hizi zilibebwa na script na casting. Kuna filamu zimezalishwa na kamera ya mkononi lakini script yake ni lazima utaimalizia hiyo filamu utake usitake (The Blair Witch Project).
Ni hatari.