Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Natamani sana kuifanya hii biashara ya mitumba, kwa wazoefu ni changamoto zipi naweza kumbana nazo pindi nifanyapo hi biashara na nini ushauli wako. Nipo sumbawanga mjini
 
Njoo uuze ilala au machinga complex mkuu(location ya biashara yako matters) na aina ya nguo unazouza(style) bila kusahau jinsia ya unaowauzia,wanaume wengi ni makauzu hawanunui nguo mara kwa mara japo wao ndo wanunuzi wakuu (indirectly) wa Nguo za akina dada
 
Sijawahi kuuza nguo hiyo ni personal experience tu.
 
Tathimini mzunguko wa hela kwanza hapo S'wanga make mtumba hauchelewi kuchuja hasa kama utauexpose juani +vumbi kwa muda mrefu pasipo kununuliwa.
 
Jamani wadau,

Nataka kufanya biashara yakuuza nguo za mitumba kwa jumla(kuuza kwa balo) nataka kujua yafuatayo.ipi Itanilipa kununua mzigo hapa kwa wahindi ambao wao wameitoa nje, yaani na wenyewe wamenunua kwaajili ya kuuza? Au niagize mzigo nje? Pia kama kuna hints zozote zinazohusiana na biashara hii niambieni wadau.pia wapi naweza kupata mitumba mizuri ya ukweli kwa bei poa?
 
Ndugu yangu, wazo lako ni zuri ila nakushauri fanya utafiti wa kutosha katika biashara hizi. kununua apa kwa wahindi si mbaya ila wangine wanachakachua sana. wana weka malonya tu, wengine wanauza kama wanavyo toa nje bia kufungua na kufunga upya. Kitu kingine kama utaamua kununua nje na kuleta mwenyewe, usidhubutu kununua mitumba kutoka india. Mimi nimeishi sana india na nimegundua wahindi kwao ni masikini sana, hivyo hata mitumba ya kutoka uko inakuwa imechoka sana. nunua kutoka nchi kama canada, thailand, usa, Austrelia n,k. Pia ulizia sheria za sasa hivi zikoje usije ukaleta mitumba yako kumbe watu wa tbs wakaja kuichoma moto. nguo zingine hazitakiwi kuingizwa nchini. Jambo la mwisho mitumba ambayo inaweza kukulipa zaidi ni nguo za watoto ua zinaenda sana. ndo hayo tu na Mungu akubariki
 
Asante ndugu japo si mimi muuliza swali
 
Wakuu habari zenu

Nina wazo la kufanya biashara ya kuuza nguo za mitumba kwa mfumo wa kununua Mabaro then kuyapeleka kwenye masoko mbalimbali, natafuta vijana wanazipiga mnada then mzunguko unajirudia kama kawa.

Mtaji nilionao mpaka sasa ni 5Million Tshs, sina uzoefu wowote wa biashara, hivyo kwa yeyote mwenye kuielewa hii biashara please tupeane uzoefu.

Kwasasa bado nipo kwenye ajira, ila natamani sana kuanza kuwa mjasiriamali maana siko happy kabisa na suala zima la kuajiriwa, niliingia humo kwa lengo la kukusanya mtaji then nikafanye yangu

Naomba kuwasilisha, napokea pia mawazo mapya....
 
Biashara ya mitumba ni nzuri ila kwa sababu ndo unaanza usitumie kiasi chote kufanya hiyo biashara kwa sababu huwezi jua kama itakulipa au lahh..Kwa kuanzia tumia angalau hata 1mil kwa kuanza kuchagua baadhi ya nguo kwenye masoko then unauza kwa staili yako kama ni kutafuta frame yote ni juu yako

Nakwambia hivo kwa sababu na mimi ni muajiriwa kama wewe na nimeshafanya sana mambo ya biashara, yana challenge zake. Usitoe kwanza kiasi chote angalia mwelekeo wa iyo biashara yako mana najua utapata ushauri mzuri tu kutoka kwa wafanyabiashara wa mitumba ila nakushauri usiingie kichwa kichwa.
 
Jaman karibu tupeane uzoefu, +ve contributions pls

Ni biashara nzuri sana mkuu na hasa kama ulivyosema unataka kuuza kwa njia ya mnada Mimi mwenyewe naifanya iyo shughuri nilianza just mwezi 1 uliopita na baro moja na sasa ninauwezo wa kuagizia baro 5 na malengo yangu niwe nauza kwa jumla na lengo hilo litafanikiwa kwani msimu wa korosho ndo unaanza huku kusini. Kwa Maelezo zaidi ni PM namba zako tuone kama tunaweza kushirikana kwa hilo.
 
Ahsante sana bwana Mtimbo, yap nashukuru kwa kunipa courage kuwa issue inawezekana na wewe umeweza bila shaka nami nitaweza tena maradufu sababu nguvu na nia ninayo, wadau wengine mnakaribishwa tufanye hii kitu kwa level zingine..
 
Nimeiona mkuu text yako!
Ila biashara ipo hivi:

Kila baro inavyotoka nje inakua na mchanganyiko wa nguo zote yaani grade A, B,C na zinginezo na haswa kwa zile mixture kinachosumbua kuna aina fulani ya baro huwa wabongo huzifungua na kuchukua nguo nzuri then huzipack tena
sasa hukikumbana nazo hizo zilizofunguliwa unaweza ukakata mtaji

Kuna aina kama tatu hivi za baro ambazo ni nzuri kwa mnada kwani zenyewe ni mixture

Aina ya kwanza ambazo zenyewe hutoa nguo nyingi ambazo ni grade one ni Australia ambazo zinapatikana ktika uzito wa kg 100 na bei yake ina range Tsh 450000 hadi 500000, hizi ni nzuri na ndio ninazoziuza Mimi nawe nakushauri uzipate hizo kwani si rahisi kukata pesa yako, umeanguka sana unarudisha pesa yako.

Za pili ni baro za kichina nazo ni nzuri na hata bei yake ni affordable kg 100 @ Tsh 370000 hadi Tsh 420000

Na za tatu ni za kimarekani maarufa kama SUMMER, zinapatikana katika uzito wa kg 50 na 80 na bei zake Tsh 250000 hadi Tsh280000 kwa za kg 50 na Tsh 320000 hadi Tsh370000

Ndio hivyo mkuu, jipange kachukue mzigo huo.
 
Ok haina kwere mkuu, ila design umesema unafanya biashara yako Mtwara au sikukuelewa, mimi nataraj mchakato kuufanyia dar, ila kwenye soko bado sija-decide kama itakuwa ilala, karume, tandika, manzese au sehemu nyingine, vp hizo baro za grade A toka Australia zinapatikana wapi? Kuhusu bei hakuna shida so long as nanunua mzigo classic na nina uwakika wa kupata faida nzuri.

Vp kwa uzoefu wako faida yake kwa baro moja imekaa vp kama biashara ikienda poa, nipe tu profit range...
 
Ok haina kwere mkuu, ila design umesema unafanya biashara yako Mtwara au sikukuelewa, mimi nataraj mchakato kuufanyia dar, ila kwenye soko bado sija-decide kama itakuwa ilala, karume, tandika, manzese au sehemu nyingine, vp hizo baro za grade A toka Australia zinapatikana wapi? Kuhusu bei hakuna shida so long as nanunua mzigo classic na nina uwakika wa kupata faida nzuri...
Vp kwa uzoefu wako faida yake kwa baro moja imekaa vp kama biashara ikienda poa, nipe tu profit range...

Sijajua Dar biashara ya mnada ipoje/ inalipaje lakini kwa huku kusini mtwara/ lindi biashara ni nzuri sana na kama nilivyokudokezea pale awali sasa hivi no msimu wa korosho so wakulima wanakua na pesa na biashara hufanyika poa tu.

Kuhusu faida, biashara ikiwa nzuri baro 1 hununua baro lezange na kwa upande wangu imenisaidia sana kuinuka haraka haraka name ndio maana naanza kua hats name kiburi cha kutaka kuanza na mimi kuanza kuuza kwa jumla.
 
Shukrani wana JF maana nimepata ufahamu kwa kiasi kuhusu hii biashara. Hivi hayo mabaro yanauzwa wapi hapa Dar
 
nimeiona mkuu text yako!
ila biashara ipo hivi:

Kila baro inavyotoka nje inakua na mchanganyiko wa nguo zote yaani grade A, B,C na zinginezo na haswa kwa zile mixture kinachosumbua kuna aina fulani ya baro huwa wabongo huzifungua na kuchukua nguo nzuri then huzipack tena
sasa hukikumbana nazo hizo zilizofunguliwa unaweza ukakata mtaji

Kuna aina kama tatu hivi za baro ambazo ni nzuri kwa mnada kwani zenyewe ni mixture

Aina ya kwanza ambazo zenyewe hutoa nguo nyingi ambazo ni grade one ni Australia ambazo zinapatikana ktika uzito wa kg 100 na bei yake ina range Tsh 450000 hadi 500000,hizi ni nzuri na ndio ninazoziuza Mimi nawe nakushauri uzipate hizo kwani si rahisi kukata pesa yako ,umeanguka sana unarudisha pesa yako

Za pili ni baro za kichina nazo ni nzuri na hata bei yake ni affordable kg 100 @ Tsh 370000 hadi Tsh 420000

Na za tatu ni za kimarekani maarufa kama SUMMER, zinapatikana katika uzito wa kg 50 na 80 na bei zake Tsh 250000 hadi Tsh280000 kwa za kg 50 na Tsh 320000 hadi Tsh370000
ndio hivyo mkuu jipange kachukue mzigo huo

Mkuu hua unachukulia wapi kwa bei hii? Na pia za aina gan? Za watoto, kike au kiume au hiyo bei ni constant kwa mabaro ya nguo ya aina yeyote?
 
Owk Mr. Mtimbo hongera kwa hapo ulipofikia, tuendelee hiyo biashara ya jumla ya mabaro imekaa vp? Na kwa upande wa mnada ilikuwa inakuchukua mda gani kumaliza baro moja na kutia sokoni lingine. Big up sana mkuu kwa kututiaa moyo wajasiriamali wenzako nasi pia tutaleta mrejesho hapa hapa jamvini ili wengine pia waendelee kujifunza hii fursa.
 
mkuu hua unachukulia wapi kwa bei hii? Na pia za aina gan? Za watoto, kike au kiume au hiyo bei ni constant kwa mabaro ya nguo ya aina yeyote?

Mkuu bei hizo ni kwa baro

ambazo ni mchanganyiko yaani unazipata za watu wote, wake kwa waume, watoto kwa wa kubwa,aidha Jessy, mashuka taulo hadi mapanzia yanapatikana pia.

Aina hizi za baro ni nzuri na haswa kwa biashara ya mnada kwani lengo huwa kuakikisha kila aina ya mteja na mahitaji yake yanatimizwa kikamilifu

Aidha kuhusiana na swala bei hazitofautiani sana kati ya hizi baro mchanganyiko na zile aina moja ya nguo,

Bei nilizoItaja hapo juu unaweza ukazichukua kama standard price tu na zenyewe ziko specific kwa baro za mchnganyiko
 
Back
Top Bottom