Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndugu yangu, wazo lako ni zuri ila nakushauri fanya utafiti wa kutosha katika biashara hizi. kununua apa kwa wahindi si mbaya ila wangine wanachakachua sana. wana weka malonya tu, wengine wanauza kama wanavyo toa nje bia kufungua na kufunga upya. Kitu kingine kama utaamua kununua nje na kuleta mwenyewe, usidhubutu kununua mitumba kutoka india. Mimi nimeishi sana india na nimegundua wahindi kwao ni masikini sana, hivyo hata mitumba ya kutoka uko inakuwa imechoka sana. nunua kutoka nchi kama canada, thailand, usa, Austrelia n,k. Pia ulizia sheria za sasa hivi zikoje usije ukaleta mitumba yako kumbe watu wa tbs wakaja kuichoma moto. nguo zingine hazitakiwi kuingizwa nchini. Jambo la mwisho mitumba ambayo inaweza kukulipa zaidi ni nguo za watoto ua zinaenda sana. ndo hayo tu na Mungu akubariki
Jaman karibu tupeane uzoefu, +ve contributions pls
Ahsante sana bwana Mtimbo, yap nashukuru kwa kunipa courage kuwa issue inawezekana na wewe umeweza bila shaka nami nitaweza tena maradufu sababu nguvu na nia ninayo, wadau wengine mnakaribishwa tufanye hii kitu kwa level zingine..
Ok haina kwere mkuu, ila design umesema unafanya biashara yako Mtwara au sikukuelewa, mimi nataraj mchakato kuufanyia dar, ila kwenye soko bado sija-decide kama itakuwa ilala, karume, tandika, manzese au sehemu nyingine, vp hizo baro za grade A toka Australia zinapatikana wapi? Kuhusu bei hakuna shida so long as nanunua mzigo classic na nina uwakika wa kupata faida nzuri...
Vp kwa uzoefu wako faida yake kwa baro moja imekaa vp kama biashara ikienda poa, nipe tu profit range...
nimeiona mkuu text yako!
ila biashara ipo hivi:
Kila baro inavyotoka nje inakua na mchanganyiko wa nguo zote yaani grade A, B,C na zinginezo na haswa kwa zile mixture kinachosumbua kuna aina fulani ya baro huwa wabongo huzifungua na kuchukua nguo nzuri then huzipack tena
sasa hukikumbana nazo hizo zilizofunguliwa unaweza ukakata mtaji
Kuna aina kama tatu hivi za baro ambazo ni nzuri kwa mnada kwani zenyewe ni mixture
Aina ya kwanza ambazo zenyewe hutoa nguo nyingi ambazo ni grade one ni Australia ambazo zinapatikana ktika uzito wa kg 100 na bei yake ina range Tsh 450000 hadi 500000,hizi ni nzuri na ndio ninazoziuza Mimi nawe nakushauri uzipate hizo kwani si rahisi kukata pesa yako ,umeanguka sana unarudisha pesa yako
Za pili ni baro za kichina nazo ni nzuri na hata bei yake ni affordable kg 100 @ Tsh 370000 hadi Tsh 420000
Na za tatu ni za kimarekani maarufa kama SUMMER, zinapatikana katika uzito wa kg 50 na 80 na bei zake Tsh 250000 hadi Tsh280000 kwa za kg 50 na Tsh 320000 hadi Tsh370000
ndio hivyo mkuu jipange kachukue mzigo huo
mkuu hua unachukulia wapi kwa bei hii? Na pia za aina gan? Za watoto, kike au kiume au hiyo bei ni constant kwa mabaro ya nguo ya aina yeyote?