Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Mkuu ahsante sana kwa maelezo matamu, nimechelewa kujibu nilikuwa pori mtandao nii shida. Tafadhali niunganishe hap watu.
Watu wasikukatishe tamaa ndg, tena mimi si kwa rafiki wala jirani, nilianza mtumba, kwa kununua bero moja tu pale mnazi mmoja, faida ikatoka karibu sawa na bei ya baro nikarudia.

Nguo za kike zinalipa, mashuka na viatu, za kiume suruali na mashati ila wanaume wanakamatika kiurahs ukiwafikishia maeneo yao ya kazi au kwa kufuatwa.

Nimewai kwenda Uganda, najua vizur pia huko, anzia nyumbani uimarike kibiashara, japo mimi nimeajiriwa serikalini lakn nafanya sana mtumba. Na ivi sasa naanza likizo june, nitaendelea na mtumba kama kawa.

Mil 3 ni nyingi, suala la kununua bero na au za kuotea za kutundika/mnada ni wewe tu na upendo wako, za bero lazima ukute na marapurapu ndani, ingawa huwa tunauza cheap, na hazikosi wavaaji au wanunuzi, za kuotea utauza zote bila kuacha rapurapu lkn je? Unauzoefu wa kuotea nguo? Yani ukiiona tu unapoint? Maana mnakuwa wengi kayika ku point na wwngi ni wazoefu.

Hapo inahtaji mtu anaeona nguo tu nakujua hii ni sumu la sivo utaotea zote takataka au zinazokuvutia wewe binafs alafu zisivutie wateja

Sehemu ya kupoint nguo ni ilala Boma, alifajir saa kumi na moja, baadae hakuna soko asbh meza ni za wanaouza kawaida kwa wapita njia.

Uliza swali kwa kile sikuandika nitakujibu

Dresses za kike bero ya bei ya juu ni 380000/= kwa zile za kg 45, lakn unakuta bero ya top hadi 170000/= zinatofautiana kuanzia 150000/= mpk 400000/= hapo ndio juu sana kwa beri ya kilogram 45 na ukienda utaonesha hapa grade B hapa 1
Note: bero zinauzwa kwa kilogram, bei nilioweka ni. Kwa kg 45 ambazo mara nyingu utakuta nguo hadi 200

Bero za mil 1 ni kilograms 100 nk

Kuna maduka wana nguo uhakika. Naweza kukupa namba private nikakuunganisha.

Jaribu usikatishwe tamaa
 
Tupe japo maelezo kias tuelewe we upo wap, na unataka utaratibu gan kabla ya kusema tunafanya au hapana.
 
mkuu pcs 205 ,

chukua mtaji tsh 3,000,000/205 = tsh14,7000

turn over tsh 6,000,000/205 = tsh 30,000

ili kupata turn over ya 6,000,000 kila pc auze kwa avarage price ya 30,000 ,
na hapo ujatoa usafirishaji, kodi ya banda, gharama ndogo ndogo

hapo :smash:

Nijuavyo mie viatu vya mitumba huuzwa hadi 150,000/= kwa pair. Si vema sana kufanya generalization
 
Aiseee kama ana info ya bei za jumla atuwekee inaweza kuwa nafasi kwa wengine kujifunza.
 
Tupo wengi jamani hasa hii biashara ya mtumba nguo za watoto. Mwenye uelewa atujuze. Asanteni
 
Naomba wadau waje hapa pia ntaka kujua mabaro first quality ya mashuka ya mtumba ntapata wapi.
 
Habari wanajukwaa!! Awali ya yote naomba nikiri wazi kuwa sijawahi wala sina uzoefu wowote na hili. Nahitaji kufanya biashara ya kuingiza mitumba (ya nguo) kutoka Ujerumani kupitia bandari ya DSM.

Naomba mwenye ufahamu mzuri anifahamishe ni taratibu gani zitakazonihusu, kampuni gani ya clearing & forwarding niitume, na kwa kila furushi moja la mzigo ( la 100kg kwa mfano) nachajiwa ushuru kiasi gani hapo bandarini?

Heshima kwenu ma expert!!
 
Pamoja na hayo.Kumbuka vile vile Mjini fitina nyingi kila mtu anajua anavyoingiza mzigo wake na kuutoa.Maswala ya uzoefu ni mbwembwe tu .Ushauri wangu kama uko serious mtafute mtu aliye karibu yako anayeingiza mizigo upitishie mizigo yako kwenye mizigo yake.
 
Pamoja na hayo.Kumbuka vile vile Mjini fitina nyingi kila mtu anajua anavyoingiza mzigo wake na kuutoa.Maswala ya uzoefu ni mbwembwe tu .Ushauri wangu kama uko serious mtafute mtu aliye karibu yako anayeingiza mizigo upitishie mizigo yako kwenye mizigo yake.
Sawa mkuu ila nilitaka japo nipate ABC kidogo zinifute tongotongo.
 
Nipo mkoan naitaji kufanya biashara hii, msaada. Nahitaji mzigo mzuri. Hasa kwa mabelo. Pia nahitaji mtu mwaminifu wa kuniongoja na kunipa ushauri mzuri. Wengi wamekuwa wakidanganya, nina mtoto mdogo sijaanza kusafiri.
 
Habari Mamytrifo, nafikiri biashara hii ya mitumba inahitaji kufanya utafiti wa kujua mzigo (mabelo) unapatikana wapi, nauli ya kuusafirisha mpaka sehemu unapofanyia biashara na changamoto zingine, tafuta wafanya biashara wa mitumba walio karibu yako na upate ushauri wa kujua jinsi ya kuanza na kuendesha biashara hii.
 
Back
Top Bottom