Scorpio Me
JF-Expert Member
- Aug 2, 2016
- 6,119
- 7,934
ushapata jibu?Wakubwa naomba mwongozi wa kupata mitumba bora kwa Dar ! Nineshauriwa nisinunue bales Bali nikachague
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ushapata jibu?Wakubwa naomba mwongozi wa kupata mitumba bora kwa Dar ! Nineshauriwa nisinunue bales Bali nikachague
Ulicho eleza ni 100% ukweli mtupu, kuna braza angu anauza METRESS COVER (nyumba za godoro) Tandika. huwa anavunja ma ballore, show huwa ina anza mida 4 mpaka saa 6 anakua amemaliza ballore zake5 ballore kipindi chanyuma lilikua linanunuliwa bei chee kidogo ila kwa sasa halikamatiki linauzwa laki mbili na 80 alafu bei zilizopo mnadani ni zilezile 3,500, 4000,5000,6000,7000,8000,9000, 10000 N.k,Ushauri wangu, lete hiyo mitumba tz 70% iwe ya kiume na 60% ya kike! na kwakua unaanza lete grade 1, ili ujenge good will na wateja! wahindi wanacho kifanya wanaleta grade tofauti kisha wanachanganya ili kupata super profit! Uzuri mmoja ni kuwa, ukileta mali nzuri. Mteja mmoja akifungua na kuona ni mzuri, huwaambia wenzake na wote huja kwako.
Kizuri kingine ni kuwa, kuna watu wana hela zao chini..Wao wanasubiri wasikie fulani kafungua mali nzuri na inakimbia, yeye anakufuata, kisha anakupa hela ya belo zote ulizonazo store kisha yeye anauza rejareja kama wewe ila anakuwa kaongeza elfu kumi au ishirini kwa belo! kwenye hii biashara, umakini mkubwa ni ubora wa hizo nguo na jinzi sio jinzi tu ziwe za kisasa, sio chupa (juu pana, chini inabana, hutouza)! nilishwahi kuingiza nguo frm tz zamani from usa via charlestone port via s.carolina, zilinikata kwakweli!
Hakikisha kwenye huo mtumba, hakuna sox wala chupi. TBS watakupa shida bandarini!
Kama unaweza, mkuu badala ya nguo za mitumba weka mitumba ya viatu vya kiume, au changanya nguo za mtumba na viatu vya mtumba ili upime biashara! open shoes, canvas, mukasin, sendoz raba n.k! Kikweli biashara ya viatu vya mtumba inakimbia kupita maelezo.
Huna haja ya kuwa na duka au stoo kariakoo...wewe ukitangaza tu una viatu vya mtumba hasa vya kiume na kama utaweka kidogo vya kike visiwe kokoko, watu wananunua mali yote kwa siku moja! Ukiwa mvivu, utawauzia kontena lote, faida utaiona lakini ni kidogo sana ukilinganisha na watakachoenda kupata wao!
Kila siku asubuhi saa kumi uwe ushafika kariaokoo (mchikichini) na baloo tatu au nne hivi na kuhakikishia mpaka inafika kwenye saa moja asubuhi, unakuwa umemaliza mali yoote na unarudi home na furushi la kimango! Kule unakodisha meza kwa huo muda ni shilingi 5,000/- na vijana waaminifu wapo wa kukusaidia kulinda na kupiga debe, wewe kazi yako ni kupokea hela!
Kinachofanyika ni kuwa a day before upeleke hizo balo za viatu kariaokoo, unaita vijana wanatenganisha viatu vya kushoto na kulia, kwahiyo ukifika mchikichini asbuh unamwaga eiza vya kulia unabaki na vya kushoto and vice vser! Akikipenda kiatu unamtajia bei, bkoz kila kiatu kina bei yake, anakupa hela huku ameshika kimoja alicholipia! wakati wakufunga biashara, unampa mguu uliobakia.
Ofkoz, hadi mida hiyo lazima kuna pea kadhaa zinakuwa hazijapata wanunuzi, good news ni kuwa pembeni kuna watu kibao wanasubiri muhesabiane in a flat rate vyote vilivyobaki...ana ku'cash wewe unarudi na hela home saa moja asbh, na kuandaa mazingira ya kesho!
You can send mtu wako pale mchikichini, mida hiyo asbuhi akathibitishe nilio kwambia!
tnx Mnada unakuwaga juna ngapi kwa week?Tandika mnadani
Monday to Sundaytnx Mnada unakuwaga juna ngapi kwa week?
shukrani mkuu ,kazi kaziMonday to Sunday
Boss me natafta ya kuuza, afu hapo shekilango nna mpango Wa kuweka Bizness yangu, ,ila cjajua nafata utaratibu gan ili kupata eneo au banda kabisa.Njoo ubungo hapa shekilango
Asante sana mkuu kwa ushauri mzuri,nitafanyia kazi ushauri wako.Tatizo muhindi amepandisha bei ya balo
Ila siyo mbaya, Faida ipo binafsi nafahamu Kwenye upande wa shuka, nguo za watoto na za wanawake.
Changamoto ni kukosa wateja wa aina fulani ya nguo
Kukuta ballo bovu na nyuki kibao
Issue siyo brand issue ni kueleweka kwa muhindi akupe mzigo mzuri
VP ulifanikuwa kuanza hii biashara ,naomba unipe experience yko coz na Mimi nataka kuifanya hiyo hiyoHabari zenu wanajamvi wote humu nawasalimu, heshima zenu nyote pia mnaostahili heshima hii.
kama kichwa kinavyoeleza,mimi nimekuwa nikijihusisha na vibiashara vidogo vidogo kutokana na mtaji wangu niliokuwa nao na walau umeongezeka kufikia kiasi Fulani.Nafikiria kuingia kwenye biashara ya kuuza nguo za mitumba,maana baadhi ya watu wanasema inalipa ila sijapata taarifa za kutosha kuhusu hii biashara.Mambo yakienda sawa nafikiria kuanza kununua belo moja kwa kuagiza dar au nitaenda mwenyewe.
Naombeni ushauri wenu hasa kwa wale wenye uzoefu wa biashara hii na wale ambao pia wanaweza kunisaidia kupata taarifa sahihi kuhusu biashara hii.
Nina maswali machache ambayo labda yatanipa mwanga namna ninavyoweza kuingia katika biashara hii.
1. Nguo za daraja gani zinafaa kuanzia hasa kwa mtu mwenye mtaji mdogo chini ya shilingi 500000/=
2. Nguo za jinsia ipi zinatoka kwa urahisi
3. Nguo zinazotoka nchi gani n inzuri zaidi zinauzika Zaidi yaani kutoka ulaya au Asia?
4. Nitajuaje kuwa balo hili lina nguo nzuri kwa sababu nasikia kuwa kuna wasambazaji tofauti huko nje hivyo baadhi ya brand zao zinauzika Zaidi,kuna ukweli wowote juu ya hilo.je naweza kujua hizo brand zao?
Ninashukuru sana kwa wote watakaotoa muda wao kunisaidia kwa hili,kwani utakuwa msaada mkubwa sana.
MUNGU AWABARIKI SANA.
Asante