Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

#wazee je kwa mfano me nikiwa na m1 ntaweza pata balo ngapi za kuanzia
 
Wakuu Kwanza kabisa poleni kwa changamoto za hapa na pale. Niende moja kwa moja kwenye Mada ninaplani ya kuuanzisha biashara ya nguo za mtumba.. Nipo mkoani lengo niufuate mzigo dar nije kuuza.

Mimi kiukweli Sio mzoefu Sana na biashara hii kama vile location kwa pale dar zinapatikana wapi, Bei zake usafiri nk. kwa hiyo kabla ya Kuja ibiwa Mwenye uzoefu wa biashara hii anielekeze nisije jutia pesa yangu! Wasalam!. Karibuni.
 
Mjomba wangu kesho kutwa hongera sana kwa wazo la biashara, kuna nyuzi kadhaa humu zimeongelea kwa upana sana kuhusu maduka ya nguo za mitumba kwa jumla hapa dar na jinsi watu wanavyopigwa, usiwe mvivu mjomba jaribu kuzitafuta utajifunza mengi.
 
Nashukuru Sana mkuu hizo nyuzi nimejaribu kuzisaka sijafanikisha
Mjomba wangu kesho kutwa hongera sana kwa wazo la biashara, kuna nyuzi kadhaa humu zimeongelea kwa upana sana kuhusu maduka ya nguo za mitumba kwa jumla hapa dar na jinsi watu wanavyopigwa, usiwe mvivu mjomba jaribu kuzitafuta utajifunza mengi.
 
Kuwa makini kwenye kujua size,sema kwenye balo ni ngumu kujua size,vingi ni oversize kulingana na nchi inapotoka.
 
Mkuu Sawa nimekupata vipi Bei zake kama unauzoefu
Dah bei sijui kwa wakati huu,maana nilishukag dar 2016 January kuchukua balo LA mashati,jamaa wangu alinipeleka kwenye maduka kuchagua haikufika laki tatu.

Baada ya kuchukua kesho yake nikasafirisha kuja kwetu mkoani nikapumzika kwa muda,nikaja nikakata balo na kuchagua Yale ya grade ,na zoazoa yalikuwa oversize saana mpaka nikauza jero jero.

Vile vile zingatia jinsia unayoilenga na rika husika.

Usiwe na haraka,tafuta mwenyeji&mzoefu mabeli yanahitaji umakini
 
Dah bei sijui kwa wakati huu,maana nilishukag dar 2016 January kuchukua balo LA mashati,jamaa wangu alinipeleka kwenye maduka kuchagua haikufika laki tatu.

Baada ya kuchukua kesho yake nikasafirisha kuja kwetu mkoani nikapumzika kwa muda, nikaja nikakata balo na kuchagua Yale ya grade ,na zoazoa yalikuwa oversize saana mpaka nikauza jero jero.

Vile vile zingatia jinsia unayoilenga na rika husika.

Usiwe na haraka,tafuta mwenyeji&mzoefu mabeli yanahitaji umakini
Nashuruku mkuu
 
Habari za wakati huu ndugu zangu natumaini amani ipo ya kutosha huko mliko

Nimekuwa nikijipanga kwa muda sasa ili lengo langu la kufanya biashara ya duka la nguo huku mikoani lifaninikiwe naona bado nahitaji kujifunza mambo kutoka kwa wazoefu wa biashara hii
Nachohitaji kukifahamu zaidi ni haya yafuatayo:

👉MTAJI KAMILI WA KUANZA NAO
👉NAMNA YA KUSAJILI BIASHARA YANGU
👉UJUZI MWINGINE UTAKAOSAIDIA KUSUKUMA BIASHARA HII MBELENA IWE YENYE FAIDA
👉AINA YA NGUO ZINAZOUZIKA KIRAHISI MFANO NGUO ZA WATOTO,ZA WADADA AMA VIJANA

NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWENU NYOTE
 
Mtafute jamaa anaitwa usiendekariakoo huko insta ndo naona ana maduka ya nguo mengi mkoani akupe ujuzi.
 
Habarini wakuu,

Kwa wiki ya pili sasa nimekuwa nikitafuta taarifa kuhusu biashara hii hasa hasa ni nguo, bag, viatu, ila watu wengi wananiambia ukinunua balo huwa zinakata mtaji na ni vizur ununue nguo moja moja maeneo kama ilalana tandika kisha uje kuweka dukani.

Wakuu naomba kwa yeyote mzoefu wa buashara hii atupe mawili matatu, hata kama ulikuwa unafanya now umeacha, maana nimeuliza ile lobota grade A kg 45 wameniambia 370 000/ nami hii biashara ipo miongoni mwa biashara nazotaka kuzifanya kuanzia mwakani,
 
Back
Top Bottom