Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Habari,

Mwenye kufahamu nguo za mtumba kwa akina dada zinapatikana wapi kwa ulanguzi ili nami nikauze na malengo yangu makubwa ni kuwauzia wanafunzi wa chuo. Na hali ilivyokuwa ngumu kutegemea kazi moja, hatuwezi kufanikisha.
Kazini natoka saa 4:00 jioni, kwa hiyo huo mda nataka niutumie kufanya biashra hiyo.

Mawazo yenu tafadhali.
 
Habari yenu wanajamvi,

Twende kwenye mada
Kwa yoyote anayefahamu biashara hii ipoje. Mimi nipo chuo DODOMA sasa nauliza.

Je, kuchukua nguo Dar na kuleta DODOMA ili niuze kwa wanachuo inakuwa nguo moja nauziwa kwa Tsh ngapi Dar na naweza pata faida kiasi gani kwa nguo moja.

Nguo ninazotaka nianze nazo ni form six izi za sasaivi zinazo trend yaani kiufupi sina ufahamu kuusu hii biashara anayefahamu tuhabarishane nina pesa 200,000/= adi 250,000/= mtaji
 
Kama form 6 unanunua jumla kwa elfu 10 tshirt 20, ambapo ni sawa na 200000. Wewe unauza nguo hyo 15 na kupata faida ya 100,000 kwenye nguo 20. Unatoa na elfu 10 ya kutuma kipasel unabaki na 90 na mtaji wako bado upo palepale wa laki mbili so unakuwa na 290,000.
 
Kama form 6 unanunua jumla kwa elfu 10 tshirt 20, ambapo ni sawa na 200000. Wewe unauza nguo hyo 15 na kupata faida ya 100,000 kwenye nguo 20 unatoa na elfu 10 ya kutuma kipasel unabaki na 90 na mtaji wako bado upo palepale wa laki mbili so unakuwa na 290,000
Wanavyuo hawanunui Mashati zaidi ya Tsh 5,000 ( Zile za kutembeza Hostel ). Bei za wanavyuo ukitaka kuuza Mashati bila shida ni Tsh 3,000 - Tsh 5,000. Anyway mimi nataka kujua wananua wapi hizo shati za form 6?
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naomba kujuzwa kuhusu biashara ya mitumba kwa dar iko vipi? Na upi ushauri wako?
 
Habari, jamani nahitaji kuanza biashara ya kuuza mavazi ya wanawake, yeyote mwenye uzoefu na biashara hiyo naomba mwongozo wake.
 
Ungefafanua mkuu

Madela, kanga, vyupi, sketi, au....
 
Wakubwa naomba mwongozi wa kupata mitumba bora kwa Dar ! Nineshauriwa nisinunue bales Bali nikachague
 
Back
Top Bottom