Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Ulicho eleza ni 100% ukweli mtupu, kuna braza angu anauza METRESS COVER (nyumba za godoro) Tandika. huwa anavunja ma ballore, show huwa ina anza mida 4 mpaka saa 6 anakua amemaliza ballore zake5 ballore kipindi chanyuma lilikua linanunuliwa bei chee kidogo ila kwa sasa halikamatiki linauzwa laki mbili na 80 alafu bei zilizopo mnadani ni zilezile 3,500, 4000,5000,6000,7000,8000,9000, 10000 N.k,

Unakutaa ballore moja lina metress cover 38-44
alafu zinakua mchanganyiko nzuri na mbaya kwa sasa biashara ina changamoto sanaa sababu bei za ballore zimekua juu alafu wanao daka bei zao ni za miaka ile ile kwaio faida haionekani lakini kipindi cha nyuma watu wamepiga pesaaa hatareeeee

Ukilipia meza elfu5 then uwalipe watu wanao nadi huwa wanakua wawil 8000 au 10000 itategemea na faida ya siku iyo
kwa sasa hii buzz inakata sanaa ila ilikua bonge la biashara wanao daka ndo wanao pata faida kwa sasa akinunua mfano elfu kumi theni analichana vipande viwili plus kulipinda kwa fundi then kuliuza si chini ya 25000 elfu

Nenda tandika mtaa wa masoko utakuta watoto wa masasi (mtwara) wanejaa wanafanya izo bizz
 
Habari za saizi ndugu zangu mimi natakuanza biashara ya nguo viatu na sandozi vya mtumba ila sjajua wanauza au (mastoo) yanapatikana wap kama kuna mtu anajua sehem hiyo naomba ani direct ili nije kujirdhisha bizaa zilizopo bila kusha na viatu vya michezo mtumba nina posema mtu siyo yale yalio siyo na quality hapana nataka qualit mtumba[emoji109][emoji109]
 
Mwenye kujua chimbo la mikoba ya mitumba ya wadada kwa hapa dar,yenye bei rahis tuelekezane wadau. Shukrani
 
Habari zenu wanajamvi wote humu nawasalimu, heshima zenu nyote pia mnaostahili heshima hii.

Kama kichwa kinavyoeleza,mimi nimekuwa nikijihusisha na vibiashara vidogo vidogo kutokana na mtaji wangu niliokuwa nao na walau umeongezeka kufikia kiasi fulani. Nafikiria kuingia kwenye biashara ya kuuza nguo za mitumba,maana baadhi ya watu wanasema inalipa ila sijapata taarifa za kutosha kuhusu hii biashara. Mambo yakienda sawa nafikiria kuanza kununua belo moja kwa kuagiza dar au nitaenda mwenyewe.

Naombeni ushauri wenu hasa kwa wale wenye uzoefu wa biashara hii na wale ambao pia wanaweza kunisaidia kupata taarifa sahihi kuhusu biashara hii.

Nina maswali machache ambayo labda yatanipa mwanga namna ninavyoweza kuingia katika biashara hii.

1. Nguo za daraja gani zinafaa kuanzia hasa kwa mtu mwenye mtaji mdogo chini ya shilingi 500000/=
2. Nguo za jinsia ipi zinatoka kwa urahisi
3. Nguo zinazotoka nchi gani n inzuri zaidi zinauzika Zaidi yaani kutoka ulaya au Asia?
4. Nitajuaje kuwa balo hili lina nguo nzuri kwa sababu nasikia kuwa kuna wasambazaji tofauti huko nje hivyo baadhi ya brand zao zinauzika Zaidi,kuna ukweli wowote juu ya hilo. Je, naweza kujua hizo brand zao?

Ninashukuru sana kwa wote watakaotoa muda wao kunisaidia kwa hili,kwani utakuwa msaada mkubwa sana.

MUNGU AWABARIKI SANA.
Asante
 
Tatizo muhindi amepandisha bei ya balo

Ila siyo mbaya, Faida ipo binafsi nafahamu Kwenye upande wa shuka, nguo za watoto na za wanawake.

Changamoto ni kukosa wateja wa aina fulani ya nguo

Kukuta ballo bovu na nyuki kibao
Issue siyo brand issue ni kueleweka kwa muhindi akupe mzigo mzuri
 
Asante sana mkuu kwa ushauri mzuri,nitafanyia kazi ushauri wako.
 
Niliwahi kuskia mtumba marufuku ifikapo 2018 katika nchi za east Africa.
Upo maeneo gani Ili uelekezwe mahali unapoweza kupata bidhaa unazozihitaji palipo karibu na wewe.
 
VP ulifanikuwa kuanza hii biashara ,naomba unipe experience yko coz na Mimi nataka kuifanya hiyo hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…