Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Ushauri wangu, lete hiyo mitumba tz 70% iwe ya kiume na 60% ya kike! na kwakua unaanza lete grade 1, ili ujenge good will na wateja! wahindi wanacho kifanya wanaleta grade tofauti kisha wanachanganya ili kupata super profit! Uzuri mmoja ni kuwa, ukileta mali nzuri. Mteja mmoja akifungua na kuona ni mzuri, huwaambia wenzake na wote huja kwako.

Kizuri kingine ni kuwa, kuna watu wana hela zao chini..Wao wanasubiri wasikie fulani kafungua mali nzuri na inakimbia, yeye anakufuata, kisha anakupa hela ya belo zote ulizonazo store kisha yeye anauza rejareja kama wewe ila anakuwa kaongeza elfu kumi au ishirini kwa belo! kwenye hii biashara, umakini mkubwa ni ubora wa hizo nguo na jinzi sio jinzi tu ziwe za kisasa, sio chupa (juu pana, chini inabana, hutouza)! nilishwahi kuingiza nguo frm tz zamani from usa via charlestone port via s.carolina, zilinikata kwakweli!

Hakikisha kwenye huo mtumba, hakuna sox wala chupi. TBS watakupa shida bandarini!

Kama unaweza, mkuu badala ya nguo za mitumba weka mitumba ya viatu vya kiume, au changanya nguo za mtumba na viatu vya mtumba ili upime biashara! open shoes, canvas, mukasin, sendoz raba n.k! Kikweli biashara ya viatu vya mtumba inakimbia kupita maelezo.

Huna haja ya kuwa na duka au stoo kariakoo...wewe ukitangaza tu una viatu vya mtumba hasa vya kiume na kama utaweka kidogo vya kike visiwe kokoko, watu wananunua mali yote kwa siku moja! Ukiwa mvivu, utawauzia kontena lote, faida utaiona lakini ni kidogo sana ukilinganisha na watakachoenda kupata wao!

Kila siku asubuhi saa kumi uwe ushafika kariaokoo (mchikichini) na baloo tatu au nne hivi na kuhakikishia mpaka inafika kwenye saa moja asubuhi, unakuwa umemaliza mali yoote na unarudi home na furushi la kimango! Kule unakodisha meza kwa huo muda ni shilingi 5,000/- na vijana waaminifu wapo wa kukusaidia kulinda na kupiga debe, wewe kazi yako ni kupokea hela!

Kinachofanyika ni kuwa a day before upeleke hizo balo za viatu kariaokoo, unaita vijana wanatenganisha viatu vya kushoto na kulia, kwahiyo ukifika mchikichini asbuh unamwaga eiza vya kulia unabaki na vya kushoto and vice vser! Akikipenda kiatu unamtajia bei, bkoz kila kiatu kina bei yake, anakupa hela huku ameshika kimoja alicholipia! wakati wakufunga biashara, unampa mguu uliobakia.

Ofkoz, hadi mida hiyo lazima kuna pea kadhaa zinakuwa hazijapata wanunuzi, good news ni kuwa pembeni kuna watu kibao wanasubiri muhesabiane in a flat rate vyote vilivyobaki...ana ku'cash wewe unarudi na hela home saa moja asbh, na kuandaa mazingira ya kesho!

You can send mtu wako pale mchikichini, mida hiyo asbuhi akathibitishe nilio kwambia!

Kaka yangu anafanya hiyo busnss, uko sahihi kabisa.
 
Habari zenu wadau,

Mimi ni mwanamke wa kitanzania,mwenye familia ya mtoto mmoja,kutokana na hali halisi ya maisha kwa sasa ninatamani sana kufanya biashara ya mitumba hususani nguo za watoto maana katika utafiti wangu nimegundua watoto ndio wanaonunuliwa sana nguo katika familia nyingi maana wao ndio wanaongoza kwa kuchakaza nguo kutokana na kuwa na michezo mingi na pia nyingine zinawaruka au kuwabana kutokana na hali ya ukuaji.

Sasa nakuja kwenu wadau mnishauri

i- Kwa Dar es Salaam ni wapi naweza pata mitumba mizuri ya watoto na kwa bei nafuu zaidi,ukinitajia na bei utakuwa umenisaidia sana

ii- Ni maeneo gani ambayo naweza kuuzia bila usumbufu,yaani kupata meza ya kuuzia ya kudumu kulingana na hali yangu ya kipato cha chini,kwa sasa naishi ndani ya wilaya ya temeke.

iii- Kwa wale waliowahi kuuza mitumba je faida zake huwa zikoje kwa furushi au bello moja ukilinganisha na bei ya kuchukulia

iv- Je, kulingana na kipato changu cha chini naweza kuanza na mtaji wa shilingi ngapi?ili nijue namna ya kujipanga.

Natanguliza shukrani kwa wote mtakaopitia uzi huu kwa kuchangia na hata kusoma tu.
 
Habari wadau,

Kama mjuavyo, hapa ndio nyumbani. kuna mtu ameniomba ushauri wa wapi anaweza kupata mitumba kwa bei ya jumla, amesikia kuwa pengine bei inakuwa nafuu kenya, mara zbar, mara hapa hapa kko Dar es Salaam. Ameniomba ushaauri. tafadhali wenye uzoefu. yeye yupo Dar es Salaam. Pia kama mnamfahamu mtu anayeuza kwa jumla, naomba mni-PM namba yake. hususani nguo za akina mama/dada.
 
Dada ulifanya hii biashara? Mimi nina mawazo tofauti kama uliifanya. Nitakupa ushauri na labda ujaribu. Nitumie private message. Ila sidhani au labda sijui kama ni muhimu kusema una mtoto, au huna au una mume au ndugu wakati lengo lako ni biashara tu.

Mungu atakujalia
 
Dada ulifanya hii biashara? Mimi nina mawazo tofauti kama uliifanya. Nitakupa ushauri na labda ujaribu. Nitumie private message. Ila sidhani au labda sijui kama ni muhimu kusema una mtoto, au huna au una mume au ndugu wakati lengo lako ni biashara tu.

Mungu atakujalia

Kwa maswali hayo ni dhahiri hana uzoefu kabisaa na hiyo biashara. Na kama una msaada ni vizuri zaido uandike hapa ili na wengine wajifunze pamoja na kuongezea uzoefu ktk ushauri wako. Huko Private mimi huwa naona ni kama utapeli. Kipi cha siri? Tuamke kwa kweli.
 
Habar wadau, VP braa za kinadada Na mama grade nzuri zapatikana? Ni shiling ngapi kwa bale?
 
Mkuu hua unachukulia wapi kwa bei hii? Na pia za aina gan? Za watoto, kike au kiume au hiyo bei ni constant kwa mabaro ya nguo ya aina yeyote?
Huku arusha mabaro ya watoto ya grade one mixture ni kuanzoa 700,000/=
 
Jamani mie nko mtwara na nataka nifanya hyo biashara hususani nipate mitumba ya kuchagua kwa bei ya jumla nina mtaji wangu kama 700,000 maana nimeuza samak ila saiv nimeona hawanilipi,naombeni ushauri wapi nitazipata hzo nguo za mitumba mizuri kwa bei nafuu? Naombeni mawazo yenu.
 
Mie ni mkazi wa mtwara nina kiasi cha mtaji wa 700,000 nilikuwa nauza samaki lakini tatzo kubwa hawanilipi kwahyo nataka niuze mitumba, kwahyo naomba ushauri wenu wapi nitapata mitumba mizuri kwa bei ya jumla yaani ya kuchagua kwa bei nafuu na je, inaweza nilipa? Mawazo yenu tafadhali naombeni.
 
Wakuu habarini, naombeni ushauri nataka nianze kuuza mitumba ya nguo za kiume naombeni ushauri na uzoefu we nu.
 
=> Nguo za watoto miaka 0-4, NDO ZITAKUTOA HASA WAKIUME BUKTA ZA JEANS, VIGAUNI YA WAKIKE PIA VINALIPA kumbuka watoto huvalishwa nguo zaidi ya nne kwa siku, hujikojolea kujichafua kwahiyo wanahitaji nguo nyingi kuliko rika lingne

=>NGUO za watoto utakayo muuzia MWANAUME ni bei ya juu kuliko MWANAMKE sababu ni kwa kuwa wanaume wengi hawajui bei za nguo kama akina mama

=> NGUO ZA WANAWAKE HASA WADADA ZINALIPA kumbuka wanaume hawana tabia za kununua nguo kama wanawake

=>BELO MOJA LA NGUO ZA WATOTO LINA NGUO 300 au 400 na kuendelea linauzwa GRADE Three 220,000/= GRADE TWO 350,000/=

GRADE ONE 600,000/= nyingne ni 800,000/=

Bei ni za Mnazi Mmoja DAR ES SALAM

=> UKICHAMBUA KARUME FANYA KUWAHI ASUBUHI SANA SAA 10 ASUBUHI UKACHAGUE

=>TAHADHARI: ufunguapo BELO ni sawa na nazi hujui kama ni nzima au mbovu ndani, UNAWEZA NUNUA UKAPATA NGUO NZURI MPAKA RAHA siku nyingne ukanunua zote mbovu haziuziki hata moja NDO BIASHARA ILIVYO
 
NGUO ZA KIUME ZINAZOLIPA NI JEANS ZIWE MODEL kwa vijana ukichukua zile pana itakula kwako
=> KOMBAT nazo zinalipa
 
Habari,

Nimejaribu kufatilia Mwenge na Sinza yaani asilimia zaidi ya 80 biashara iliyopo ni ya maduka ya nguo.

Ukienda Kariakoo mtaa unaongoza kwa kuwa na watu wengi ni mtaa wa Kongo na huo kwa zaidi ya asilimia 80 biashara inayofanyika ni biashara ya nguo.

Nilikuwa najiuliza, inamaana watanzania tunapenda sana kuvaa nguo? Je, biashara hii inalipa sana?

Baada ya kutafakari kwa kina na kuona michango yenu namimi nitafungua duka la nguo, wanasema usifungue biashara kwa kuwa fulani anafanya namimi nitafungua baada ya kuona wafanyabiashara wa Sinza na Kariakoo wanauza nguo kwa bei mara mbili ya waliyonunua hivyo kama eneo lina wateja wanapata faida kubwa sana.

Yaani tisheti au shati wananunua elfu 17 wakishaliweka kwenye frem zao za vioo bei zao wanaanzia elfu 35 na kama we ni mbishi basi utanaunua kwa elfu 30.

Heri ya mwaka mpya.
 
Ndugu, ungesema maduka ya mavazi, maana hata viatu wananunua 18000 wanauza 40000
 
=> nguo za watoto miaka 0-4, NDO ZITAKUTOA HASA WAKIUME BUKTA ZA JEANS, VIGAUNI YA WAKIKE PIA VINALIPA kumbuka watoto huvalishwa nguo zaidi ya nne kwa siku, hujikojolea kujichafua kwahiyo wanahitaji nguo nyingi kuliko rika lingne
=>NGUO za watoto utakayo muuzia MWANAUME ni bei ya juu kuliko MWANAMKE sababu ni kwa kuwa wanaume wengi hawajui bei za nguo kama akina mama
=> NGUO ZA WANAWAKE HASA WADADA ZINALIPA kumbuka wanaume hawana tabia za kununua nguo kama wanawake
=>BELO MOJA LA NGUO ZA WATOTO LINA NGUO 300 au 400 na kuendelea linauzwa GRADE Three 220,000/= GRADE TWO 350,000/=
GRADE ONE 600,000/= nyingne ni 800,000/=
bei ni ZA mnazi mmoja DAR ES SALAM
=> UKICHAMBUA KARUME FANYA KUWAHI ASUBUHI SANA SAA 10 ASUBUHI UKACHAGUE

=>TAHADHARI: ufunguapo BELO ni sawa na nazi hujui kama ni nzima au mbovu ndani, UNAWEZA NUNUA UKAPATA NGUO NZURI MPAKA RAHA siku nyingne ukanunua zote mbovu haziuziki hata moja NDO BIASHARA ILIVYO

Mkuu hivi nikuulize mara nyingi upatikanaji wa BELO unaweza pata nchi gani?
 
Je, mi nataka kununua BELO halafu kuuza kwa bei za jumla. Bei zake zikoje na soko lake lipo wapi?
 
Back
Top Bottom