Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Habari wanajamii,

Kuondoa usumbufu wa kufungua thread nyingi kuhusu hii biashara nimeona niulize swali langu humu humu ingawa thread ni ya zamani, nataka nianze kufanya biashara ya viatu vya mtumba nimejulishwa kuna wahindi huwa wanauza mabelo ya viatu vya mtumba mazuri wanapatikana kariakoo mwenye ujuzi na hili anisaidie ndugu zangu.

Nawasilisha.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Nami pia nisaidieni katika hilo alilouliza blakafro. Msaada wanajamvi.
 
Habari wana Jukwaa.

Nimekusudia kuanza biashara ya kuuza mitumba ya nguo za akina dada na watoto, hivyo basi naomba masaada wa kujua kati ya Dar es Salaam na Mbeya wapi inapatikana kwa wingi, pia na unafuu wa bei ukoje?

Pia kama kuna mtu anajihusisha na uuzaji wa mitumba kwa jumla anaweza nisaidia mawasiliano yake au tuwasiliane PM.

Ahsante sana, naamini nitapata msaada wa haraka zaidi.
 
Kwa Dar nenda Mnazi Mmoja kwenye maduka ya wahindi,utaona maduka mengi sana ya mitumba.

(1) Belo grade A Kg 45-55 kwa nguo za kiume ni laki5-4,kila belo lina nguo 200-250..Grade B laki3-2.8
(2) Nguo za watoto. -Nguo nyepesi kuanzia umri 0-6yrs mpaka 2-12yrs grade A laki5-4.5

-Nguo za kawaida umri 0-6yrs na 2-12yrs grade A laki4-3.
Grad B nguo za watoto ni laki2.5

(3) Nguo za kike grade A laki3,grade B laki2-1.8
NB: Ila bhana sasa hivi nguo wanachakachua sana kama sio mzoefu unaweza kununua grade A ukaja kukutana na mafampa.

Ukitaka belo lenye nguo nzuri mpe cha juu mfanyakazi utakayekutana nae apo, lakini ukijifanya bandidu inakula kwako
 
Kwa dar nenda mnazi mmoja kwenye maduka ya wahindi,utaona maduka mengi sana ya mitumba.
(1) Belo grade A Kg 45-55 kwa nguo za kiume ni laki5-4,kila belo lina nguo 200-250..Grade B laki3-2.8
(2) Bguo za watoto. -Nguo nyepesi kuanzia umri 0-6yrs mpaka 2-12yrs grade A laki5-4.5
-Nguo za kawaida umri 0-6yrs na 2-12yrs grade A laki4-3.
Grad B nguo za watoto ni laki2.5
(3) Nguo za kike grade A laki3,grade B laki2-1.8

NB: Ila bhana sasa hivi nguo wanachakachua sana kama sio mzoefu unaweza kununua grade A ukaja kukutana na mafampa.

Ukitaka belo lenye nguo nzuri mpe cha juu mfanyakazi utakayekutana nae apo,lakini ukijifanya bandidu inakula kwako

Ahsante mkuu kwa ushauri
 
Habari zenu za Majukumu Ndugu zangu.

Bila shaka Muwazima, nami Nashukuru kama Ni ivyo ila Kama hauko vizuri basi usipoteze Matumaini yako Kwa Mwenyezi Mungu endelea kumuomba.

Nina hitaji kufanya biashara ya Nguo za Mitumba aina Ya Suluali Za Cadet.

Nimegundua ninapo ishi hizi nguo Zina Soko ila Shida Yangu kujua huko kwenye Soko la hizo Balo Kuna aina ngapi ya Dizain hiyo ya Nguo (Suluali Za Cadet) na Bei zake zikoje kama mtu unataka Balo.

Shukran kwa usikivu.
Nina shida ya ufafanuzi wa ilo tu.
 
Habari wadau,

Mwenye ufahamu wowote kuhusiana na zinapopatika nguo za mitumba kwa jumla, au njia za kupita ili kuweza kununua mitumba inayouzika.

Tupeana msaada wa maarifa hapa, Msaada sio lazima kumpa mtu mtaji au pesa pekee, hata kumuelewesha mtu njia za kupitia pia ni msaada mkubwa sana.

Ukizingatia hivi sasa hali ya uchumi imebana, hivyo kuna fursa kubwa sana hapa kwenye mitumba kwa kua ni bei nafuu ukilinganisha na first hand clothes.

Nahitaji msaada wenu wa maarifa na mawazo.

Ahsanteni
 
Back
Top Bottom