Biashara ya Night Club Dar imekufa?

Biashara ya Night Club Dar imekufa?

Time really flies aisee. Miaka Ile Bills, Mambo Club hatari na nusu. Sio kwamba hizi open bar hazikuwepo. Weekend imefika jioni unajongea Jolly pale au Qbar unaanza mdogo mdogo moja moja hadi saa 6 unazama bills hadi alfajiri. Dah maisha yake hawawezi kujirudia. Watu wastaarabu wanajua muziki mzuri. Enzi hizo ukitaka oldies unazama Blue Palms unakula oldies balaa hadi kiu inakata unasuuzika moyo kabisa.
Sio sasa hivi ujinga mtupu, open bar lounge ni amapiano tu. Yan unaweza kukaa masaa 5 hujasikia oldies hata moja ni maujinga ya amapiano tu watu wako kama kuku anakata roho ndo styles za kucheza eti.
Mpaka mtu unaona it’s better ukae nyumbani ufungulie zako ngoma unazozitaka😂kuku anakata roho
 
Naona wabongo wanashindwa kutofautisha Night clubs na pub/bars, Night clubs ni special kwa kudance na kunywa, bar ni kunywa tu na kudance ni kuforce , maana hamna dance floor. Nadhani starehe za bongo zinarudi nyuma hamna kabisa night clubs ila kuna mabars tu. Sisi ma mtoni bado kuna ma night clubs ya nguvu ya kumwaga na yote uwa yanakua downtown tu. huko vitongojini ni pubs tu na mwisho ni saa 6, ila night clubs ni all night long.
 
Nikaona kinywaji cha Tequila nikasema duh so mishahara yangu 5 ndiyo nanunua hii chupa 1.

Nashuka nakuta kuna mzigo wa 4M.

Roho imeniuma. Kwasababu naamini kuna watu wanamudu huu mzigo, swali kuu ni 'How did they do it?' acha hawa generational wealth
Kuna Wanaijeria niliwakuta Kidimbwi one day. Nikasema sitakaa nikaenda sehemu za kishua kama zile. Yale ni matumizi mabaya ya pesa.

Wananunua chupa za 1.5M hafu sio moja wala mbili, nyingi tu.
 
Siasa za Awamu ya Tano na RC wa zamani.....nani angeenda Night Club?

Pia kulikuwa na wimbi la wasiojulikana ambao hadi leo hawajajulikana ilihatarisha usalama wa wala bata usiku.
Ndio maana sijawahi kumpenda shujaa wa Afrika. Ni mtu ambaye hakupenda watu wawe na furaha.Alikuwa na roho mbaya sana. Na alinikera sana alivyovyunja Bilicanas
 
Binafsi kizazi cha sasa naona kama haki-enjoy kabisa. Watu wanakaa tu pub wanatandaza beers na pombe kali nyiiiingi, no dancing ni kutikisa vichwa tu na kushikashika warembo.

What a lazy life!?

Kipindi hicho unakula bia mtaani ikifika saa sita mnahamia club huko hata ukitaka kuongea labda upaza sauti maana ni sound la kufa mtu, mwendo wa ku-dance.

The only time muziki unasimama labda kuwe na show baaas. Zaidi ya hapo ni kucheza.

Sifa kuu za night club
1. Ni indoor
2. Privacy ya kutosha, kulikuwa hadi na VIP rooms
3. Well sound proofed
4. Dance floor ya maana
5. Nyimbo mchanganyiko....inafikia mahali mnajua kabisa kuwa muda flani ni muda wa bongo fleva na dj fulani ndio anapiga, muda fulani ni oldies na mnajua mkali wa oldies ni nani ukicheck kwa dj chamber unakuta kweli ni yeye.

No talks ni muziki kwa kwenda mbele.

Siku hizi sioni kama kuna starehe. Watu wamejikita kwenye mashindano ya kunywa na kupost kwenye oage zao.
Good old Days.
Siku hizi starehe ni kunywa mipombe mingi tu. Tunataka zama za disco life zirudi asee.
 
Summary ya Menu ya vinywaji hii hapa: Aione na RRONDO View attachment 2934372
Putin.jpg
 

Attachments

  • Putin.jpg
    Putin.jpg
    3.4 KB · Views: 5
Uholela wa biashara bila vibali. Bar na pubs zinatakiwa kufungwa saa sita usiku. Then club zinakesha. Watu wakitoka bar wanaingia club mpaka asubuhi.
Sasa bar,pub,liquor stores zote zinakesha nani ataenda club?
Hata ndio matokeo ya kutosimamia sheria ndio maana hata mitaani watu hawalali kisa bar inapiga muziki hadi asubuhi.
Kweli kabisa, Samaki samaki au Terminal Pub Morogoro yaani ni mpaka majogoo...
 
Back
Top Bottom