Biashara ya samaki

Me niliuza nikaambia laki moja kilo moja tena lubichi kuna wachina wanafanya bei inaenda juu sana
Ni kweli miss chagga inaweza kufika mimi nimesemea kwa bei ya zamani make hawa Chinese ndo wamefanya soko liwe juu.Siku ukija Mwanza nenda soko kuu kuna soko la samaki la jioni unaweza nunua sangara 40000 but bondo si mali yako unaliacha kwa muuzaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa mpaka Mali asili WameingilIa kati hawatoi vibali vya kuexport ..
 
Kabisa mpaka Mali asili WameingilIa kati hawatoi vibali vya kuexport ..
Hii ni habari njema sana wavuvi coz wavuvi walikuwa wanapata pesa kidogo sana halafu jamaa wamepiga pesa ndefu kupitia migogo yao.Yaani ziwa lina fursa nyingi za pesa ajabu. Imagine Wanyarwanda wanaenda mpk visiwani kipindi cha msimu wa dagaa wananunua dagaa karibu zote wanapeleka Rwanda wakifika Rwanda wanazipeleka kiwandani wanaziosha wanazitengeza vizuri na kuzifanyia lepackage safi wanaweka lebal na kuziuza ndani ya Rwanda na nje Rwanda kwa pesa ndefu wakati huku wamechukua kwa bei ya chini sana,Jaman serikali ingeweka jisho huko tungelikuwa na wavuvi matajiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tamaa na uelewa mdogo wa biashara kwa wavuvi .kidogo wameanza kuelewa
 
Tamaa na uelewa mdogo wa biashara kwa wavuvi .kidogo wameanza kuelewa
Hapana mpendwa,tatizo ni watendaji ambao wanashindwa kusaidia ktk hili,imagine km tungelikuwa na factories zetu za kuweza kununua dagaa na kufanya lepackage wenyewe km wanavofanya korosho,kahawa nk mbona ingelikuwa poa.Zamani tulizoea kuona mtu akila dagaa unaonekana maskini!Dhubutu!!!Mwanza si hivo tena dagaa ipo juu kinoma kisa soko la Rwanda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mkuu
 
Maliasili waingilie tuu lakini yanavushwa kwa magendo kwenda uganda na kilo moja uganda ni dola 320 kwa sasa na ni cash haina longo longo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu JF,

Habari zenu, hongereni na mihangaiko. Nataka kujua biashara ya samaki imekaaje, kuanzia kivukoni, bagamoyo, kanda ya ziwa kwa ujumla wake, kigoma.

Aina za samaki kama dagaa, vibua n.k

Kwa anaejua lolote kuhusu biashara hii, kwa maana ya upatikanaji wake/uvuaji wake kulingana na majira, ununuaji, uuzaji, usafirishaji, leseni/kibali, uhifadhi wake na changamoto zake. Naomba kwa anaejua atoe mchango wake hapa.

Karibuni!
 
Kama una mtaji wa kutosha fungua mashamba ya Samaki.

Make hii ya kuvua nayo ina mashariti kibao ya Serikali.

Ukiwekeza kwenye mabwawa makubwa ya Samaki hakika utatoka.
 
Kama una mtaji wa kutosha fungua mashamba ya Samaki.

Make hii ya kuvua nayo ina mashariti kibao ya Serikali.

Ukiwekeza kwenye mabwawa makubwa ya Samaki hakika utatoka.
Yeah ni kweli. Ina maana mwenye mtaji mdogo hana nafac ya kuchangamkia fursa kwenye hii biashara ya samaki? Kwa mfano ukitaka uwe unanunua na kuuza, vp uzoefu wako khs eneo hilo?
 
Yeah ni kweli. Ina maana mwenye mtaji mdogo hana nafac ya kuchangamkia fursa kwenye hii biashara ya samaki? Kwa mfano ukitaka uwe unanunua na kuuza, vp uzoefu wako khs eneo hilo?
Hiyo unafanya ila kumbuka unafanyanl uchuuzi. Unaziwa Samaki sh elfu 5 unamuuza sh elfu 7.

Unaweza fanya tu.
 
Kama una mtaji wa kutosha fungua mashamba ya Samaki.

Make hii ya kuvua nayo ina mashariti kibao ya Serikali.

Ukiwekeza kwenye mabwawa makubwa ya Samaki hakika utatoka.
Tena ufanye upesi nkuandikie business plan yako...utayopatia mtaji...uzoefu ninao
 
Kwa waenyeji wote wa mikoa ya.SHINYANGA
SINGIDA
DODOMA
MOROGORO
DAR ES SLA
Ambao wana uzoefu au wanatamani kuanza kufanya biashara ya Samaki katika mikoa yao
Na hawajui wapi wanaweza kupata mzingo wa Samaki...habari njema Samaki wanapatikana kwa wingi na kwa bei nzuri itakayo kuletea faida nzuri weka odder yako sasa na mzigo utakufikia mkoa wako husika...

Kwa maelewano zaidi piga ..0745703651 kwa walioko dar es saam....
Na mikoa mingine piga namba 0758255256 au 0688644047 Asanteni sana
 
bei nzuri ni ipi?
Mi huwa nakereka na hawa wafanyabiasha ambao wanasema nauza kitu bei nafuu au bei nzuri halafu hawaweki bei,huu ni ubabaishaji,hatujifunzi kwa wenzetu?!mfano,angalia makampuni yanayofanya biashara mitandaoni wanaweka bei ya bidhaa zao,halafu wewe ukiiona utajipanga kulingana na mfuko wako,bei nzuri kwako kwa mwingini ni mbaya,bei nafuu kwako kwa mwingine ni ghali.Tupia bei mtu aamue mwnyw!
 
Ndo maana nimeweka namba ndugu sio kirabiashara lazima BEI uweke hadharani..ndo misingi ya biashara yetu iyo BEI zinatofautiana MKOA kwa MKOA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…