PatriceLumumba
JF-Expert Member
- Mar 9, 2016
- 426
- 581
Asante kwa ufafanuzi wako mzuri, naamini mleta mada atakuwa amepata mwanga kwa kiasi flani juu ya biashara hii. Mimi binafsi nimenufaika sana. Kuna jambo ninaomba ufafanuzi wa kina mkuu juu ya idadi ya copy ambazo mashine imeishatoa. Swali langu ni kuna ukomo wa copy ambazo photocopy mashine ikizifikia ndio unakuwa mwisho wake wa kutumika?
THEO,
Asante kwa kushukuru mungu akubariki kwa kutambua msaada wangu,Nami sitasita kutoa msaada wa ushauri kwa kila mtu kama mada iko ndani ya uwezo wangu.
Photocopy haina kikoma cha kutoa copy,Kuna nyingnne zinatoa mpaka copy laki 4 illa bado iko vizuri iinafanya kazi kuna nyingine imeto copy laki 2 unakuta imekufa kabisa.
Na hii isikusumbue kichwa kwasababu hivi ni vifaa vya eletronics havina warranty kuubwa.Na pia inatokana kama ilikuwa inafanyiwa service mara kwa mara,Pia inaweza ikawa imetoa copy nyingi kwa muda mrefu inakuwa safi sana ila kama imeto copy nyingi kwa muda mchache ni rahis kufa mapema.
Nadhani umenipata hapo Theo
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRICA
PATRICE LUMUMBA