Biashara ya Stationery: Ushauri, Vifaa, Gharama na Mbinu za Uendeshaji

Biashara ya Stationery: Ushauri, Vifaa, Gharama na Mbinu za Uendeshaji

Natumaini ni wazima,

Ndugu wapenda naomba kujuwa mwenye uzoefu wa biashara ya stationary kwenye maeneo ya chuo hasa wale wa mikoani, nimepanga kufanya hii biashara Ila naomba mwenye uzoefu anipe japo intro ya hii biashara. Ila napenda niwe natoa huduma ya copy,printing,scan na kuuza vitu vidogo vidogo na plan yangu ni mikoani.
 
Wakuu salaam,

Nataka kufungua stationery nina Milion Moja Tu Ya mtaji,kodi nishalipia tayari imebak kununua vifaa vya kazi.

Sina kitu chochote ndo nataka nikanunue.

Hebu nishaurini ninunue nini na nini kwa kuanzia na wapi nikannunue?

Wataalam wa hizi kaz naombeni ushauri wenu.

Asante
 
1. Computer (Desktop.
2. Printer (Multifunction)
3. UPS (Sio lazima)
4. Vinginevyo naimani unavijua ambavyo vitakaa kwenye mashelf kama yapo.
 
Kitu yenye kuingiza hela kwenye stationery ni printer na photocopy machine. Photocopy tu used ni 1.5 mil, printer yenye faida ni epson ya mitungi 6 ila unaeza anzia ya mitungi 4 ile ya nje. Inacost kati ya 1.2 hadi 1.5mil desktop nunua 1 tu inatosha zile za laki2 used, nunua rim zako5 yaan box moja na kadi kadhaa halafu anza
Amekwambia ana 1m, sasa wewe unampa hesabu milioni 3 na wadogo zake
 
Mkuu unalipaje frem kisha unakuja kutuomba ushauri!

Sina nia ya kukukatisha tamaa ila kiwango chako cha hela ni kidogo sana kiasi naogopa hata kukupa budget ya vitu. Ninachokushauri ni kwamba biashara inahitaji sana mentorship, ukikosa hiii jua ni rahisi kufail na bila shaka huna mshauri.
 
Jikusanye kwanza, hiyo haitoshi kwa iyo biashara.
Unatosha kuanzia. Usimkatishe tamaaa. Anaweza kuanza kwa kununua madaftari/makaunterbooks, kalamu, mabunda ya karatasi, chaki na vifaa vingine vidogo vidogo wakati anajipanga kununua machine mbalimbali hata used. Kinachofanya biashara sio mtaji bali ni determination na guts to start a first step.
 
Kuliko apoteze huo mtaji kwa hiyo biashara ya steshenari ..bora asubiri kwanza apate mtaji wa kutosha asiwe na haraka
 
Wakuu salaam,

Nataka kufungua stationery nina Milion Moja Tu Ya mtaji,kodi nishalipia tayari imebak kununua vifaa vya kazi.

Sina kitu chochote ndo nataka nikanunue.

Hebu nishaurini ninunue nini na nini kwa kuanzia na wapi nikannunue?

Wataalam wa hizi kaz naombeni ushauri wenu.

Asante
Hongera kwa hilo wazo. Inshort hiyo fedha sio kubwa na wala sio ndogo. Lakini kumbuka pia mtaji haijawahi kujaa na kukidhi kila kilichopo zaidi ya kuanza na ulichonacho.

KWA stationary kwa uzoefu wangu Mdogo lazima ujue ni eneo gani unaenda anzisha na kwa shughuli gani utajihusisha nazo kwa kuanzia. Maana yangu ni kujua printer ambayo utaanza nayo na kwa Kiasi ulichotaja bac printer aina ya Epson l 380 itakufaa ni laki nne kasoro Hadi laki nne na 20.

Tafuta desktop used unaweza pata kwa 250k Safi na itakayomudu mwanzo wako itakayobaki ndio uchukue vifaa vidogo vidogo vya kuanzia na nadhani itaosha kusheheni stationary yako.

Mitano tena mapambano yanaendelea. Kila kheri mkuu
 
Back
Top Bottom