Biashara ya Stationery: Ushauri, Vifaa, Gharama na Mbinu za Uendeshaji

Biashara ya Stationery: Ushauri, Vifaa, Gharama na Mbinu za Uendeshaji

Vitu gani vinatakiwa kuzingatiwa unavyofungua ofisi ya stationery?

Naomba ufafanuzi wa faida, hasara na changamoto zake kwa ujumla.
 
Chagua location nzuri hasa vyuoni.

Kwenye maofisi japo siku hizi office nyingi zinamiliki vifaa karibia vyote ila si mbaya.
 
Tafuta tenda ofisi za watu, usisubiri waje wenyewe. Tengeneza bidhaa zenye jina na nembo ya biashara yako.

Kila kazi unayeweza kuweka sign weka mfano kwenye vitabu vya tickets, note books, invitation cards, nk.

Ubunifu na uchakachuaji wa products ni muhimu. Mfano unakuwa na pens unazipiga sign au nembo yako then unauza kwa bei ya ofa au kugawa bure kwa wateja wako ili kujitangaza nk
 
Namimi nahitaji hii kitu, wajuzi mje mtupe somo hasa kwa upande wa faida zake pamoja na changamoto zake!
 
Naomba ufafanuzi wa faida,hasara na changamoto zake kwa ujumla.

Umejipanga vizuri? Au ndo vile kuanza kigumu..kama hujajipanga vilivyo nichek Dm tubonge nikuuzie stationary pamoja na location.
 
Hii mashine naitafuta ni kariakoo sehemu gani?
Photocopy nzuri ni Canon Image Runner 2525 bei 1.5mil, zinapatika Kariakoo. Angalizo: kabla ya kufungua biashara ya stationery fanya utafiti wa eneo la biashara kwanza vinginevyo utaifunga au kugeuza banda la Miamala na Vocha tu.
 
Biashara hii ni nzuri sana ila inabidi kuangalia location kama chuo, kanisa au shule ili mambo yaende vizuri.

Kwenye upande wa huduma utapata wateja wa photocopy, printing, passport size na scanning. Pia inabidi uwe mbunifu mfano nyaraka ambazo kupata inamchukua mtu muda mrefu unakua nazo ofisini kwako. Unaweza kuwa na copy ya fomu ya NIDA, fomu ya maombi ya TIN (TRA) na huduma ya kuprint onlipe copy ya kitambulisho cha NIDA zote hizi zitaongeza kipato.

Kwa upande wa bidhaa weka bidhaa kama daftari, kalamu, notebook, riboni za kupambia, vifaa vingine vya mapambo, gundi, na vifaa vya shule vingi. Ukiwa na connection, uchangamfu na uchapakazi utauza sana.
Ongeza huduma kama Mpesa, Airtel, luku na malipo mengine.

Hakikisha mtu unayemweka ana ujuzi na biashara hii vinginevyo utapoteza wateja ( nmewahi kuifanya biashara hii).
Kama mtaji wako ni mdogo, fanya yale mambo ambayo unaweza kumudu vizuri usipende kubeba mambo mengi kuliko mtaji.

Hakikisha una computer, printer 3 in 1, photocopier (nashauri Canon) kama unaweza chukua na Camera kwa passport.
 
Mgeweka bei y vitu kma printer n je ukiwa n kiasi gni unaweza kufungua.

Sent using Jamii Forums mobile app

Printer Epson L850 (3 in 1)ni 1,100,000 bei inaweza kuwa chini au zaidi ya hapa kutegemea na mkoa uliopo,
Epson L805 ni 875,000/= print only (heavy duty)

Epson l382 (3 in 1) matumizi ya kawaida 495,000-550,000/=.

Ofisi nyingi wana L382 na L805 kuna ambao wana L850 pekee. L850 inasafisha picha kutoka kwenye memory card, pia inapata command kutoka kwenye PC. L805 inapata command kutoka kwenye PC na inaprint pekee. Ndiyo maana ukiwa na l805 inabidi uwe na l382 kwa ajili ya scanning na coloured copying.

Canon IR 2320 inauzwa 2,350,000/= inapiga copy na kuprint

Laminanion A3 inauzwa 120,000/=

Paper cuter A3 inauza 34,000/= A4 17,000/=

Kuna mashine ya binding ingawa sikumbuki bei yake

Camera sijawahi kuwa nayo ila kutoka hapo mengine unaweza kuongeza. Ila ili uanze kwa amani inabidi uwe na kama milioni 7 angalau.
 
Kwa hiyo unaweza kuanza na printer moja, copier na vifaa vichache pamoja na bidhaa utakazouza.
Kama uko location ambayo biashara ya 'secretarial service' inaenda sana mtaji mdogo unaweza kutosha ila kama ni eneo ambalo biashara inasuasua itabidi uchanganye kidogo bidhaa na huduma tofauti.
Kuna ambao mtaji wa 4M unawatosha kuendesha stationery.
Binafsi nilianza na 6M lakini mambo hayakwenda vizuri kwa sababu ya mzunguko mdogo wa biashara kwa eneo husika.
 
Mkuu huo mtaji wa 4m au 6m inajumuisha na kodi za fremu na TRA?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu asante kwa mchanganuo murua.niko kwenye mpango wa kuanzisha hii kitu.
Je hyo epson l850 sio heavy duty?
Printer Epson L850 (3 in 1)ni 1,100,000 bei inaweza kuwa chini au zaidi ya hapa kutegemea na mkoa uliopo,
Epson L805 ni 875,000/= print only (heavy duty),
Epson l382 (3 in 1) matumizi ya kawaida 495,000-550,000/=.
Ofisi nyingi wana L382 na L805 kuna ambao wana L850 pekee. L850 inasafisha picha kutoka kwenye memory card, pia inapata command kutoka kwenye PC. L805 inapata command kutoka kwenye PC na inaprint pekee. Ndiyo maana ukiwa na l805 inabidi uwe na l382 kwa ajili ya scanning na coloured copying.
Canon IR 2320 inauzwa 2,350,000/= inapiga copy na kuprint,
Laminanion A3 inauzwa 120,000/=
Paper cuter A3 inauza 34,000/= A4 17,000/=
Kuna mashine ya binding ingawa sikumbuki bei yake,
Camera sijawahi kuwa nayo ila kutoka hapo mengine unaweza kuongeza..ila ili uanze kwa amani inabidi uwe na kama milioni 7 angalau.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu asante kwa mchanganuo murua.niko kwenye mpango wa kuanzisha hii kitu.
Je hyo epson l850 sio heavy duty?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni heavy duty inatosha kwa shughuli za stationery...inapiga copy, inascan, inaprint kutoka kwenye pc au flash, insafisha picha, kadi za harusi, business card. Stationery nyingi ambazo wanatumia 850 wanatumia hiyo pekee bila printer nyingine.
 
Mkuu huo mtaji wa 4m au 6m inajumuisha na kodi za fremu na TRA?

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemea na bei ya fremu kwenye eneo husika na utakavyojieleza TRA. Ila kama utakua unafanya secretarial pekee inaweza kutosha vitu muhimu ni printer, photocopy machine na PC, baada ya hapo ni shelf na show case na lamination machine.
Vitu muhimu ni kama highlighter pen, correction pen, daftari, kalamu, penseli, vifutio rangi na bidhaa nyingine.
Kama unamtaji mdogo fanya secretarial na line ya mpesa ikuongezee mapato kidogo.
Secretarial inaweza kukuingizia hadi 20,000 kwa siku kama uko location nzuri.
 
Sawa nimekupata mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom