Biashara ya Uchawi Tanzania


Majimoto Tanzania inaongoza kwa uchawi Africa ni kweli au umekosea mimi nadhani ni Nigeria?! Tuambie vyema hapa
 

JE UNAJUA MSUKULE NI NINI?

MSUKULE
Msukule ni mtu ambaye anahesabiwa amekufa, lakini ukweli ni kuwa mtu huyo huwa amechukuliwa na Mchawi ili amtumie katika kazi zake maalum au amtumie katika mambo yake mengine anayoyataka.

Mchawi humfanya mtu huyo awe maiti au kama kitu kinachojiendesha chenyewe kikiwa kimekufa lakini hakijaoza wala hakiozi.

Mchawi kabla ya kumchukua mtu Msukule hufanya Mkataba Maalum na Jini anayeitwa “BAKAS” ili amsaidie katika kazi hiyo, na kuna Sadaka maalum ambayo hutoa kumlipa Jini huyo kama malipo ya kazi yake. Huyu Bakas ni Jini anayetawala siku ya Jumamosi.

Baada ya kukubaliana na Jini Bakas Mchawi huchagua mtu ambaye anataka kumchukua na akishampata huenda nyumbani kwa mtu huyo kinyume nyume mpaka anafika mlango wa mbele.

Anapofika mlangoni hunyonya roho ya mtu anayemtaka kwa kupitia tundu ya ufunguo na kama tundu hiyo haipo hutoboa tundu ndogo ambayo huiziba akimaliza kazi yake.

Baada ya kuipata roho anayoitaka huitia ndani ya chupa na kuziba chupa hiyo na kuondoka. Kazi hiyo hufanyika usiku wa manane kati ya saa nane na saa tisa usiku.

Siku inayofuata yule aliyechukuliwa roho yake huanza kuugua na hufa ghafla.

Baada ya Mazishi yule Mchawi huenda kaburini akiongozana na yule Jini Bakas ambaye hujigeuza kama babu kizee mwenye ndevu nyingi nyeupe ili kuuchukua ule mwili wa Marehemu.

Wanapofika makaburini yule Jini hukaa upande wa kichwani kwa maiti na mchawi hukaa upande wa miguuni na kila mmoja wao akifanya uchawi wake lakini kazi kubwa ya kumtoa maiti ndani ya kaburi kufanya na Jini.

Jini huomba kwa bidii na kunuiza Uchawi na husema maneno ya kichawi huku akimwaga juu ya kaburi majani ya Mkakaya (Acacia)

Mchawi yeye kwa upande wake husema maneno haya yafuatayo akirudia rudia “Mortoo tombo Mivi” maana yake ni kwamba “aliye ndani ya kaburi ni wangu”

Kwa nguvu za Uchawi mwili hutoka kaburini bila ya kaburi kuchimbwa na kusimama mbele yao na yule mchawi hukabidhiwa maiti huyo.

Baada ya kukabidhiwa kitu cha kwanza ambacho hufanya ni kwenda nyumbani na kumuonesha huyo ndugu zake kuona kama atawakumbuka.

Maiti huyo asipozinduka na kuwagundua ndugu zake au kutambua nyumbani kwao basi Mchawi hujua kwamba kazi imekuwa nzuri na hupelekwa nyumbani kwa mchawi.

Wakifika nyumbani Mchawi humrudishia yule Maiti roho ambayo aliiweka ndani ya chupa na kumnywesha dawa kali ambayo itamfanya asahau kabisa maisha yake yote ya nyuma yaliyopita na baada ya hapo maiti huyo atazinduka na kuwa Msukule.

Msukule ni binaadamu anayeishi lakini hana uhuru na anatumiwa kama mtumwa huku ndugu zake au jamaa zake wakijua kwamba amekufa.

Uchawi huu wa kuchukua Msukule ulianza miaka 500 na 1500 A.D. huko nchini Congo na Haiti na kuenea sehemu nyingi za Dunia
 
Majimoto Tanzania inaongoza kwa uchawi Africa ni kweli au umekosea mimi nadhani ni Nigeria?! Tuambie vyema hapa

Mfalme Fahd, Gaddafi, Khomein, Suddam, Osama n.k ni sehemu ya watu waliokuwa/wanaoingia shimoni Mustallah kuongeza nguvu za uchawi, Nigeria ni ya pili, Cameroon ya tatu na ya nne ni Congo
 

MziziMkavu, asante kwa maelezo yako, naongezea kidogo hapo kwenye rangi nyekundu.

Kwa kawaida mwili wa mtu bila roho hauwezi kuishi, wachawi wanapochukua roho ya mtu ndani ya mwili wake, hupulizia jini ndani ya mwili wa huyo mtu, jini hilo likishaingia ndani ya mwili huanza matatizo ya kuumwa magonjwa ya ajabu ajabu, ndugu zake wanapompeleka hospitali vipimo vinakuwa havionyeshi tatizo lolote kwa mtu huyo. Madaktari hujaribu vipimo vya kila aina na vya bei kubwa. Kawaida mtu wa aina hiyo ni lazima afe ndani ya siku saba, lakini wachawi wanaweza kuongeza muda wa kifo chake hadi wiki mbili au tatu ili ndugu zake wapoteze pesa zao nyingi wakilitibu jini. Mtu huyo anapokufa anatakiwa azikwe siku hiyo hiyo, kama kafa jioni hutokea pilikapilika za ajabu ambazo ndugu wanatoa uamuzi wa kumzika ndugu yao usiku huo huo.

Aina ya pili ni roho ya mtu kuchukuliwa kichawi, kisha wachawi kupulizia jini ndani ya huo mwili, mtu huyo ataendelea kuishi maisha ya kawaida wakati roho yake ilishachukuliwa na wachawi. Maisha ya mtu huyo yanakuwa ni ya kupoteza kumbukumbu na wakati mwingine jini lililoko ndani yake linakuwa na tabia ya kuibua magonjwa ya mara kwa mara ya aina moja kama kifafa au kisukari. Roho ya mtu huyo hutumiwa na wachawi kwenye shughuli zao za ulozi, au huziuza kwa watu wenye kuhitaji wafanyakazi kama ilivyo sasa hivi mashamba na viwanda vingi sana vinanunua roho za hawa watu, hutumikishwa kazi ngumu sana kila siku chakula chao kikiwa ni uji wa makapi ya nafaka.

Aina hii ya pili ndiyo maarufu sana hapa nchi Tanzania, kiasi kwamba sasa hivi kiasi cha asilimia 75% ya Watanzania hawapo au ni misukule lakini wapo barabarani wanatembea na kazini wanaenda. Mbaya zaidi ziko familia yote baba, mama na watoto wote roho zao zimechukuliwa, kurudisha roho hizi zilizochukuliwa kichawi zirudi na kuivaa miili yao inawezekana, tena ni rahisi sana.
 

Majimoto utafanyaje ili roho hizo zirudi na kuivaa miili yao? Naomba unielimishe. Ni vipi pia unaweza kuzuia haya yasitokee?
 
Majimoto utafanyaje ili roho hizo zirudi na kuivaa miili yao? Naomba unielimishe. Ni vipi pia unaweza kuzuia haya yasitokee?

Hapo anataka umpigie goti Majimoto ndo atoe jibu. Majimoto bwana! hahaaaaaaaaaaaaa
 
maji moto
je wachungaji wa makanisa kama kakobe,mwingira na mama rwakatare na lusekelo

je wote ni wachungaji kweli?
kwa nini hawapatani?
 
Tuwe wakweli, tusiwe wanafiki; hivi Pengo na Mwingira wanapatana?!, Walutheri na Waanglikana wanapatana?!, Wasabato na Wayehova wanapatana?!, Wasabato na Wakatoliki wanapatana?!. Kama wooote hawa wanapatana, kwanini wasiwe wamoja?. Tusijenge unafiki au chuki, kama hao [Kakobe, Mwingira, Rwakatare na Lusekelo] wameonesha wazi kuwa hawapatani hiyo ndiyo hali halisi ya yooote yanayojiita makanisa. Kila dhehebu linalojiita la ki-Kristo halitakaa lipatane na dhehebu lingine, hii ni kwa sababu ya msingi wa mafundisho yao. Ni wewe mwenyewe mwananchi kuamua yupo anawapeleka watu mbinguni, kwa sababu msingi wa yote ni utakatifu... Asante.

maji moto
je wachungaji wa makanisa kama kakobe,mwingira na mama rwakatare na lusekelo

je wote ni wachungaji kweli?
kwa nini hawapatani?
 
Shindwa pepo!! Tunamwamini MUNGU mmoja aliyeumba mbingu na nchi bila ya ku2mia hata nguzo moja. Shindwa pepo.!
 
Majimoto asante kwa information nimegundua mambo mengi sana.....wow!

with God all things are possible.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…