Biashara ya Uchawi Tanzania

Hilo la namba 10 lina uhusiano wowote na jina la mabasi ya Sumry?
 
SERIKALI YA MAJINI
Majini wana Utawala wao ambao ni Majini Wakuu na Majini wa Kawaida wanaopewa Kazi za kufanya na Wakuu wao, Katika Serikali yao kuna Wakuu wa Serikali, Wakuu wa Majeshi, Wakuu wa Mahakama na wengineo wengi.

Utawala katika Serikali yao umegawanyika katika sehemu Kuu mbili (2);
  1. Utawala katika Ulimwengu wa Kijini.
  2. Utawala katika Ulimwengu huu wetu wa Kibinadamu.
Majini Wakuu kabisa wapo Watatu (3) ambao Majina yao ni;
  1. Lucifer.................ambae ndio Mfalme wao (Emperor),
  2. Beelzebuth.......... ambae ni Mtoto wa Mfalme (Prince),
  3. Astaroth ..............ambae ni Mtawala Mkuu wa Majimbo (Grand Duke).
Hawa Watawala Wakuu kabisa watatu, iwapo Binadamu anataka kuwaita na kuwatumia inambidi atumie njia Maalum;
Mtu anayewaita anatakiwa achore alama zao kwa kutumia Damu yake mwenyewe, au anaweza pia kutumia Damu ya Kobe wa Baharini (Kasa) katika kuandikia.

Iwapo atashindwa haya yote basi anaweza pia kuwaita kwa kuchora alama za Majini hao kwenye Kito cha Ruby au Emarald; kwani vito hivi vinaendana sana na Majini hasa wale wa Ukoo wa Jua, ambao huwa na Busara, wazuri na Marafiki zaidi kuliko aina nyingine ya Majini.

Alama hizi za Majini zinatakiwa zivaliwe na Mtu ambae anataka kuwaita. Ikiwa muitaji ni Mwanamme, anatakiwa aiweke kwenye Mfuko wake

wa Kulia na iwapo ni Mwanamke, anatakiwa aiweke katikati ya Matiti yake ikielekea upande wa Kushoto.

Alama hizi zinatakiwa ziandikwe katika siku ya Jumanne saa Kumi na mbili (12) mpaka saa moja asubuhi au saa saba mchana mpaka saa nane kwa majini wote.

Majini hawa watatu wana uwezo wa kufanya mambo yote, na kwa Mtu ambae anawaita hawa anatakiwa aheshimu wale tu ambao watamheshimu kwani Majini hawa Wakuu wanawaheshimu wale tu ambao ni Marafiki wao Wakuu na wa karibu, hivyo mtu anaeamua kuwaita anatakiwa ajihadhari kwa lolote ambalo linaweza kutokea.


Utawala wa hawa umegawanyika baina yao wote kwani kila mmoja ana Wasaidizi wake wakuu Wawili ambao nao huwa wanawatuma Majini wengine kuhusu mambo ambayo Mfalme wao Lucifa ameagiza yafanyike Duniani kote.


Wasaidizi walio chini ya Lucifa ni;

Put Satanachia na
Agaliarept;.............Ambao wanaishi Bara la ULAYA na ASIA.
Wasaidizi walio chini ya Beelzebuth ni;
Tarchimache na
Fleurety...................Ambao wanaishi Bara la AFRIKA.
Wasaidizi walio chini ya Astaroth ni;
Sargatanas na
Nebiros.............Ambao wanaishi Bara la AMERIKA.

8. SIRCHADE: Ana uwezo wa kukuonyesha wewe aina zote zile za wanyama katika umbo lolote lile walilonalo.

9. SEGAL: Ana uwezo wa kukuonyesha dhahiri miujiza yeyote iwe ya kawaida au ya kimazingaombwe.


10. HIEPATCH: Ana uwezo wa kukuletea mtu aliye mbali papo hapo.


11. HUMOTS: Ana uwezo wa kusafirisha aina zote za vitabu kwa starehe yake.


12. FRUCIESSEIERE: Ana uwezo wa kuwafufua wafu.


13. GULAND: Ana uwezo wa kusababisha aina yote ya maradhi.


14. SURGAT: Ana uwezo wa kufungua aina zote za Loki.


15. MORAIL: Ana uwezo wa kufanya vitu vyote Duniani visionekane.


16. FRUTIMIERE: Ana uwezo wa kukupa kila aina ya sherehe.


17. HUICTIIGARA: Ana uwezo wa kusababisha kutembea usingizini na kwa wengine kuwakosesha usingizi kabisa.

Satanachia na Satanisie wanawatawala majini 45 au 50 wanne katika hao ni Surgutthy, Heramael, Trimasel na Sustugriel. Wawili wa hawa ni machifu na waliosalia hawana umuhimu wowote.

Hawa ni Majini watumikao kwa binadamu kwa urahisi na haraka lau ikiwa wanaelewana na anaemuita,

Serguthy ana uwezo juu ya wake za watu na wanawali
Heramael anafundisha elimu ya madawa na anatoa na ujuzi kamili wa magonjwa yote, tiba zake sahihi, anafundisha aina ya mimea yote,

sehemu mimea hiyo inapatikana, nyakati nzuri ya kuipata, umuhimu wa mimea hiyo na namna ya kuchanganya mimea hiyo ili kupata dawa sahihi kwa maradhi ya aina yeyote ile.

Trimasel na Sustugriel hawa wawili ni Machifu na wanatoa elimu ya kichawi kwa wale wanaowapenda.

Agalierept na Tarihimal wanamtawala Elelogap, ambae nguvu zake zipo juu ya Maji.

Nebirots Wawili wawatawala Hael na Sergulath.
Hael anatoa maelezo juu ya Usanii wa kuandika kila aina ya Barua, anampa Mtu uwezo wa kuongea mara moja kila aina ya Lugha na anaelezea na kufumbua vitu vyote vya siri.
Sergulath ana uwezo wa Kufundisha Mtu njia mbalimbali za kuvunja pande ambazo hazielewani.

Hawa wana Wasaidizi wao Wanane (8) wenye nguvu


1. Proculo ambae ana uwezo wa kumpatia Mtu usingizi kwa muda wa masaa manane huku akiwa anafahamu yanayotokea usingizini.


2. Haristum ambae anampa Mtu uwezo wa Kupita kwenye Moto bila ya kuungua.


3. Brulefer, ambae ana uwezo wa Kumfanya Mtu apendwe na Wanawake.

4. Pentagnony, ambae anawapa Watu uwezo wa Kutokuonekana (Invisible), pia anapendwa sana na Watawala Wakuu
5. Aglasis, ana uwezo wa Kumsafirisha Mtu kwenda sehemu yeyote ile Duniani.
6. Sidragrosam, anawafanya Wanawake wacheze Uchi.
7. Minoson, ana uwezo wa Kumhakikishia Mtu kushinda katika Michezo yeyote ukiwepo wa Kamari.
8. Bucon ambae ana Uwezo wa kuanzisha Chuki na Wivu kati ya Jinsia mbili (Wanaume na Wanawake).


 
Hivi mwenge wa uhuru unaokimbizwa nchi nzima hauna uhusiano wowote na uchawi? Naomba kufahamishwa.
 
mambo Majimoto daah hebu niambie hizo dvd za ushuhuda wa mwisilamu (mchawi) aliyeokoka na za Malango makuu ya kuzimu nitazipata wapi? Na mimi nipate kujua mabo ya dunia.
 

Majimoto kwa mambo haya dunia naanza kuiogopa.
 
majimoto tuambie nguvu za hawa akina lwakatare na lusekelo ni uweza wa kimungu au ni wa majini?
 
Mheshimiwa Majimoto tafadhali nitumie contacts zako nahitaji kuongea na wewe kirefu kuhusu masuala ya dunia/uchawi/dunia isiyoonekana inaelekea kuna vitu vingi sana ambavyo sijui na ningependa kujua.
 

Mheshimiwa Majimoto kama yote ulioandika hapa ni kweli na yamefanyika huogopi watakuchukua????? Na binadamu anasafiri vipi na kijiko???????? Jamani Majimoto please reply.
 
Mheshimiwa Majimoto kama yote ulioandika hapa ni kweli na yamefanyika huogopi watakuchukua????? Na binadamu anasafiri vipi na kijiko???????? Jamani Majimoto please reply.

Priya. Binadamu wengi hawajui nguvu na uweza wa kutenda mambo makubwa walio nao. Tenda wema, simama kwenye kweli, fanya ibada bila ya kuchoka utaona matokeo yake, shetani na wasaidizi wake ni LAZIMA ni lazima wakimbie. Mtaani kwangu walikuwepo wachawi/waganga wa kishenzi watatu, viongozi wengi wa serikali walikuwa wakiingia na kutoka tangu asubuhi hadi jioni. Kwa msaada wa Mungu wote wamekimbia mtaa. Mwezi uliopita alifika kijana mmoja akiniomba msaada, nimwelekeze mganga wangu anakopatikana. Mwanzo sikumwelewa, nilimkaribisha ndani, ndipo alinieleza mambo ya kichawi ninayofanyiwa na wakazi wa mtaa wetu ya kuniangamiza, lakini siku zote wanashangaa siku zote nimesimama bila kufikwa na jambo lolote baya. Anasema waliamua kutafuta nguvu maeneo mengine, wakachangishana nauli na walituma ujumbe wa watu wawili kwenda Sumbawanga, ajabu walirudi Dar wakanikuta bado nipo, jambo hilo liliwashangaza sana ndiyo sababu huyu kijana akaamua kunitafuta.

Huyo kijana ninaye na anaendelea vizuri na masomo. Kosa kubwa linalowasumbua watu wengi ni WOGA, woga ni kifo mara moja.

Kusafiri kwa ungo, kusafiri kwa kijiko, kusafiri kwa fagio, ni usafiri wa kutumia majini, nimeeleza kwa kirefu kwenye topic za nyuma.
 
Ndiyo ni uchawi kwa asilimia 100 (%)
Mwenge naweza sema si uchawi bali matokeo yake ni mabaya kupita kiasi sifa za mwenge ni mbaya kwa kila sehemu unapolala kwani kuna maasi mengi mno hutokea kama ulevi uasherati uwizi na ugomvi na kila aina ya mabaya ni bora uachwe ila dhana ya mwenge wa uhuru unamurika bara la africa tuache tufate mazuri na kukimbiza mwenge ni upuuzi tushapata uhuru wetu bandia tosha tuondolewe upuuzi wa mwenge

tufanye kazi tuendelee japo mianya mingi ipo wazi na haina sheria watu wanaiba na kuturudisha nyuma lakini tusikate tamaa tutafika tu tuwe kama ulaya na america
 
majimoto tuambie basi juu ya makanisa kama haya ya akina kakobe,lwakatare,lusekelo, na wengine kama hawa maana tutashindwa hata sehemu ya kwenda kuombewa du!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…