Biashara ya Uchawi Tanzania

Biashara ya Uchawi Tanzania

Juzi tarehe 26/07/2011 msichana mmoja anayeishi mjini Morogoro (kwa sasa nahifadhi jina lake kwa usalama wake) alipata ugeni wa ajabu na wa kushitua sana. Yalifika mabundi wawili mchana kweupe akiwa chumbani kwake Morogoro, kilichomshitua zaidi huyo dada bundi wale walianza kuongea naye, wakamwambia tumekuja kukuchukua (kumuuwa) na yametumwa na baba yake mzazi, lakini kwa sababu tarehe yako ya kuchukuliwa bado unaweza kuendelea na shughuli zako, lakini siku hiyo ikifika tutakuchukuwa bila wewe kujua.

Yule dada baada ya kupewa hilo tangazo la kifo, aliondoka haraka kwenda Tanga kwa wataalamu (mafundi au wachawi), kumbe mdada alikuwa na mganga wake, baada ya kumweleza mkasa huo, yule mganga akamwuliza kama anaweza kumsafirisha kwenda eneo la tukio, kwani huyo dada alipoondoka mabundi bado walikuwa ndani ya chumba chake. Dada alikubali na safari ya kwenda Morogoro ikaanza asubuhi

Mganga na binti walipofika Morogoro wakakuta mabundi yameshaondoka. Mganga akapiga manyaga yake, akawambia binti kuwa mama yake aliyekufa miezi michache iliyopita yuko nyumbani kwao Njombe. Hivyo wakaanza tena safari ya kwenda Njombe, walipofika nyumbani kwa baba yake anayeishi mtaa wa Matarawe, Njombe walipokelewa na baba yao na binti akamtambulisha mganga kuwa huyo ndiye baba yake mzazi.

Mganga bila ajizi akamwambia huyo baba kuwa kilichomleta pale ni kumchukua mama na mdogo wake binti ambao walishakufa na kuzikwa siku nyingi, mzee akakataa katakata kutokujuwa jambo lolote. Mganga akamwambia kama hatawatoa kwa hiari yake basi ataaibika atakapowatoa yeye. Mganga akafanya mambo yake, akatoka mtu wa kwanza, baadaye akatoka mtu wa pili ambaye ni mzungu, wa tatu akatoka mama na wa nne akatoka mdogo wake, wakafuatia wengine sita, jumla yao wote walikuwepo watu kumi ndani ya nyumba ya huyo mzee, wawili kati ya hao kumi walikuwa ni wazungu na taarifa zinasema wazungu hao walipata ajali miaka kumi iliyopita. Walikuwa ni wafanyakazi wa mashamba ya Mitiki ya Tanwat ambapo pia huyo mzee alikuwa anafanya kazi.

Mganga alimuliza huyo mzee sababu ya kuwa na wale wazungu, akasema anawakomesha kwa sababu walikuwa wanamnyanyasa sana wakati akifanya nao kazi Tanwat.

Ndani ya nyumba ya huyo mzee limekutwa jeneza, sanda na mashada yaliyotumika kumzikia mkewe, ambaye alizikwa kijijini kwao Lupembe.

Mganga na binti waliwachukuwa mama yao na ndogo wake na kuelekea kusipojulikana, mzee alibakia na ile misukule mingine minane. Taarifa hizi zilipoanza kusambaa katika mji wa Njombe na vitongoji vyake, watu walianza kujazana kwa wingi nyumbani kwa huyo mzee, wakitaka atoke ndani wakiwa wamenuia kumuua, ikabidi mwenyekiti wa mtaa awaite polisi wakaja na kuondoka na huyo mzee. Wananchi waliokuwa na hasira walipojaribu kuvunja mlango wa nyumba yalitokea majoka ya kutisha na wananchi wakatawanyika.

Nyumba ya huyo mzee jana na leo bado iko chini ya ulinzi wa polisi, na mapolisi wanajaribu kuzuia habari hizi zisitoke nje ya eneo hilo.

Mkoa mpya wa Njombe unatisha kwa ushirikina.

Juzi tarehe 26/07/2011 msichana mmoja anayeishi mjini Morogoro (kwa sasa nahifadhi jina lake kwa usalama wake) alipata ugeni wa ajabu na wa kushitua sana. Yalifika mabundi wawili mchana kweupe akiwa chumbani kwake Morogoro, kilichomshitua zaidi huyo dada bundi wale walianza kuongea naye, wakamwambia tumekuja kukuchukua (kumuuwa) na yametumwa na baba yake mzazi, lakini kwa sababu tarehe yako ya kuchukuliwa bado unaweza kuendelea na shughuli zako, lakini siku hiyo ikifika tutakuchukuwa bila wewe kujua.

Yule dada baada ya kupewa hilo tangazo la kifo, aliondoka haraka kwenda Tanga kwa wataalamu (mafundi au wachawi), kumbe mdada alikuwa na mganga wake, baada ya kumweleza mkasa huo, yule mganga akamwuliza kama anaweza kumsafirisha kwenda eneo la tukio, kwani huyo dada alipoondoka mabundi bado walikuwa ndani ya chumba chake. Dada alikubali na safari ya kwenda Morogoro ikaanza asubuhi

Mganga na binti walipofika Morogoro wakakuta mabundi yameshaondoka. Mganga akapi

Wapi Majimoto??? Tumekumiss mkuu.

Majimoto,heshima mkuu,swali langu moja: Ni nani aliyerithi mikoba ya mchawi mkuu wa taifa iliyoachwa wazi na mkongwe Yahaya Hussein.

Very interesting,nilifikiri wazungu hawagusiki na uchawi wa kiafrika?

Majimoto unajua lolote kuhusu uchawi katika jamii ya wamarekani weusi??????

majimoto kwa nini jk namuona anakalia kiti kile kile kila siku ?

Shindwa pepo! Shindwa shindwa! Huna mamlaka ktk mji ya watakatifu! Nenda kuzimu ukachomwe moto pepo mchafu,Shindwa shindwa na ULEGEE! Ameeen!!

Very interesting,nilifikiri wazungu hawagusiki na uchawi wa kiafrika?

Majimoto unajua lolote kuhusu uchawi katika jamii ya wamarekani weusi??????

Shetani ndiye mtawala wa dunia, ametapakaa kila kona ya dunia, angani yupo, nchi kavu yupo, ndani ya bahari na maziwani yupo. Kila mahali shetani yupo. Shetani kama mtawala wa dunia, anao wasaidizi wake na ana vikosi vya majeshi ya kupigana vita. Madhalani shetani anamtegemea sana shetani anayemiliki anga, huyu ni mwanamke anayejulikana kama malkia wa anga, ni mbaya na katili kwelikweli kuliko wasaidizi wote wa shetani. Malkia wa anga huwa hakai sehemu mmoja huwa anasafiri kuzungukiwa anga yote ya ulimwengu kuanzia dunia yetu sayari zote, nyota zote, hadi mwezini. Huyu malkia ana njia zake kabisa angani anazopita na anatembea kwa kuteleza kwenye ulimwengu usioonekana, huteleza kama wanamichezo wanavyoteleza kwenye michezo ya barafu.

Majanga yote makubwa yanayoikumba dunia husababishwa na malikia wa anga, kama vimbunga, matetemeko ya ardhi n.k.

Shetani anao wasaidizi wengine kama majini na mapepo, na yote yametapakaa dunia yote. Majini yanatumiwa sana na ulimwengu wa Kiaarabu, mapepo nayo yapo kwa wingi sana, kiasi kwamba hapo ulipo sasa hivi umezungukwa na mapepo kati ya 500 hadi 1000 au zaidi kutegemea na hali ya eneo, kama eneo hilo wanateketezwa kwa wingi wa sala ndivyo idadi kubwa ya mapepo hutumwa eneo hilo, kuzuia maombi na sala.

Hao ni baadhi ya wasaidizi wa shetani ambao wako katika ulimwengu usioonekana, kwenye ulimwengu unaoonekana shetani anawatumia wanadamu ndio hawa tunaowaida wachawi au waganga wa kienyeji. Hawa wachawi hutofautiana sana kutoka eneo moja hadi eneo lingine la ulimwengu wetu, tofauti yenyewe hutokea haswa kutokana na maendeleo na kiwango cha elimu ya eneo husika. Kwa mfano mchawi wa Tanzania wengi elimu hawana au ni ndogo sana, mchawi huyu ataloga kila kitu, hataki mtu ajenge nyumba ya bati, ataloga mkorosho, mbuzi, watoto wako yeye uchawi ni kuzuia maendeleo.

Wachawi wa uropa na marekani siyo rahisi kuwatambua, wamesoma na wana nafasi nzuri za biashara na utawala, wengi sasa hivi utawakuta wamening'iniza flash disk shingoni kumbe ni ungo wa kusafiria.

Yapo maeneo ambayo uchawi ni sehemu ya maisha ya kila siku ya watu wa eneo hilo, maeneo yanayoongoza duniani kwa uchawi ni:

a) Bara lote la Asia, Japan ikiwemo

b) Nchi zote za Kiarabu, Iran ikiongoza

c) Bara lote la Afrika, Tanzania ikiongoza

d) Marekani ya Kusini

e) Nchi za Uropa

majimoto nilikuwa nina interest na habari za mississippi na tenesee marekani
nimesiki sikia tu kwa juuu juuu

Ina maana Tanzania inaizidi Nigeria kwa uchawi?

Mkuu mhondo, Nigeria wapo wachawi waliobobea katika fani ya uchawi na wanaujua uchawi, lakini idadi yao ni ndogo kuliko idadi ya waliopo nchini Tanzania kwa sasa hivi ambao hawafahamiki sana. Nchini Nigeria mtu akiwa mchawi anakuwa mchawi kweli kweli, na mtu akiwa kiongozi wa dini anakuwa ni mtu mahiri kwelikweli kwenye dini, ndiyo maana watu wanasema watumishi wa Mungu nchini Nigeria wanatumia nguvu za giza, siyo kweli.

Majimoto,kweli Tanzania iko juu kwa uchawi kuliko nigeria? mbona tunasikia mara fulani kaenda nigeria kuchukua uchawi kwa nn wasichukue hapa hapa na je wapo wa naigeria wanaokuja kuchukua hayo maujanja hapa TZ?

Majimoto ni wakala wa shetani...........period!

Very interesting,nilifikiri wazungu hawagusiki na uchawi wa kiafrika?

Majimoto unajua lolote kuhusu uchawi katika jamii ya wamarekani weusi??????
Wengi wao wanaamini uchawi unaoitwa American VOODOO! YANI WANAABUDU ZAIDI MABABU ZAO WALIOKUFA.
FOR MORE INFO JUST GO TO "AMERICAN VOODOO"http://theoriginalpapabones.com/blog/
AND The American Voodoo Society/ Kimdubu Society.
It is very interesting for sure, coz tuna bad perception about this invisible physics.

Majimoto,kweli Tanzania iko juu kwa uchawi kuliko nigeria? mbona tunasikia mara fulani kaenda nigeria kuchukua uchawi kwa nn wasichukue hapa hapa na je wapo wa naigeria wanaokuja kuchukua hayo maujanja hapa TZ?

Tanzania yapo malango saba ya kuzimu (soma topic zangu za nyuma) na kila lango lina kiongozi wake na wasaidizi (majini) kumi na wawili yanayoratibu mbinu mbalimbali za ulozi hapa nchini. Nguvu zote za ulozi hupatikana kuzimu na kamwe siyo Nigeria.

Asante Majimoto kwa kujibu maswali yetu na tunakuomba usichoke,kwa hiyo Nigeria hakuna malango ya kuzimuni ama yapo machache ukilinganisha na Tanzania?

Back
Top Bottom