Aliyekuwa mchawi mkuu wa serikali ya Tanganyika na baadaye kubadilishwa jina na kuitwa Tanzania Yahaya Huseini amefariki dunia leo tarehe 20 Mai 2011.
Yahya aliingizwa kwenye system ya nchi na Waziri mkuu wa kwanza wa serikali ya Tanganyika marehemu Julius Kambarage Nyerere, baada ya kushauriwa na waganga wa kishenzi wa Bagamoyo, kabla ya kupata uhuru wa Tanganyika. Siku hiyo Nyerere alizuru lango kuu la kuzimu la Zazuni, Bagamoyo alipokwenda kufanyiwa uganga. Yahaya alikuwa bado kijana mdogo aliyependwa sana na viongozi wake, na alikuwa na kipaji kikubwa cha mambo ya unajimu na ulozi. Yahaya akiwa ndani ya ikulu ya Dar es Salaam, alitengeneza jini aliloligeuza umbo na kuwa fimbo, Yahaya kwa msaada ya lango la kuzimu la Mustallah waliomba watengenezewe saa ya kijini pia ambayo, kama kuna jambo lisilokuwa la kawaida saa ilikuwa inabadilika rangi kwa ndani na kuwa nyekundu.
Nyerere ambaye kwa asili yake ya kabila la Kizanaki, ushirikina ni jambo la kawaida na mara nyingi alikuwa akihudhuria matambiko yote yaliyokuwa yakifanyika kijijini kwake. Jina la Kambarage ni jina la mzimu wa mvua, marehemu ndiye alikuwa kiongozi wa mzimu huo, na ndiyo maana aliamua aitwe jina la muzimu huo wa mvua, KAMBARAGE.
Yahaya akitumia ujuzi wake wa unajimu wa kuchukuwa kichawi nyota za watu zenye vipawa vikubwa, alimsaidia sana Nyerere, baada ya kumpatia nyota ya utawala, kuongea kwa ufasaha na mvuto. Kwa kawaida kipawa chochote kutoka kwa Mwenyezi Mungu hasa kwa kiongozi, mtu unakuwa umekamilika kila idara, ndiyo maana leo hii ukisikiliza hotuba za Nyerere, unabaki kushangaa, kama mtu huyu na mawazo kama haya alishindwa vipi kuyatekeleza kwa vitendo, wakati serikali yote ilikuwa chini yake na maamuzi yake mbona hayakuwa yanatekelezwa. Binadamu tunazaliwa na vinasaba vinavyofanana kifamilia kutoka mababu wa zamani na vinasaba hivyo huendelea kuridhiwa na watoto na wajukuu, ndiyo maana kwa bahati mbaya vinasaba hivyo havisikiki kwa watoto wake wala wajukuu.
Yahaya aliendelea na nafasi yake ya mchawi mkuu wa taifa baada ya uongozi wa nchi kuwa chini ya Ali Hasani Mwinyi, majukumu makubwa ya wachawi ni kudidimiza na kuharibu maisha ya watu, hivyo kwa kutumia lango la kuzimu la mustallah la upanga, siku zote mipango yao ilikuwa ni ya uharibifu, ndiyo maana mzee Mwinyi kila akijitahidi kubadilisha hali ya maisha ya wananchi, alikuwa akiishia kubomoa misingi ya uchumi wa taifa.
Yahaya baada ya kumudu kuwadhibiti watawala hawa, kuzimu walimpandisha cheo, na kuwa mkuu wa lango la kuzimu la mustallah. Nyumbani kwake Mkwajuni Kinondoni alichimba bwawa la kuogelea, lakini hiyo ni geresha, siyo bwawa la kuogelea, bali ni lango kuu la kuingilia kuzimu, ndiye mchawi pekee, kama anavyosifiwa wa Afrika Mashariki na Kati kuwa na lango binafsi la kuingilia kuzimu. Usiku alikuwa akiingia ndani ya bwawa lake na kutambaa chini kwa chini ya ardhi hadi anaibukia juu ya lango la kuzimu la mustallah, upanga. Wachawi karibu wote hupaa angani kwa ungo, lakini mkongwe wa ulozi alikuwa anapasua udongo na miamba chini ya ardhi na njia inatokea.
Awamu ya tatu ya Benjamin, aliendelea na cheo chake kile kile cha mchawi mkuu wa taifa, jukumu kubwa likiwa ni uharibu wa maisha ya wanadamu, kipindi hiki yalijitokeza mambo makubwa ya uharibifu huko kuzimu, na kafara kubwa kubwa zilitakiwa, kafara kubwa mara zote zinatakiwa damu za binadamu kunyamazisha kuzimu. Kumbuka ajali ya meli ziwa victoria, kumbuka ajali kubwa kubwa zilizomaliza maisha ya Watanzania barabarani, kumbuka ajali za treni za abiria kila wakati kipindi chote cha utawala wa Mkapa. Mpango mkubwa ulioshindikana ni wa kuangusha ndege ya abiria ya precisios iliyokuwa inatoka Mwanza kuelekea Dar, kuzimu walishapanga mwezi, tarehe, siku na saa ya kuiangusha ndege hiyo juu ya soko kuu la kariakoo. Ilikuwa ni bahati mbaya sijui, ilikuwa ni bahati nzuri sijui lakini waliingia abiria wawili ndani ya hiyo ndege, abiria hao kuingia kwao ni baada ya abiria wengine wawili kuahirisha safari yao ya kwenda Dar hivyo tiketi zao zikapatiwa ruhusa ya kusafiri na ndege hiyo, watu hao walijulikana kama walokole, ndege ilipofika katika anga na eneo la maafa, mitego ya kichawi iliteketezwa, kwenye ulimwengu usioonekana moto ulilamba wachawi waliokuwa wamejipanga na madumu ya kuchukulia damu, misingi ya kuzimu ilipasuka, tangu siku hiyo makafara yaliyohitaji damu yalipugua sana.
Awamu ya sasa ndiyo aliwathibitishia Watanzania kuwa yeye ndiye mchawi mkuu wa taifa, anayetoa ulinzi usioonekana. Kumbuka mwaka 2005 nyota ya kilozi ilivyokuwa iking'aa kwa kiongozi wetu, inashangaza nyota imefifia kwa kasi ya ajabu, haijulikani kesho itakuwaje. Uchumi wa taifa upo kitandani Muhimbili, wananchi wamekosa matumaini makubwa baada ya ahadi kubwa kubwa walizopewa.
Ni lini taifa litapata viongozi wanaomuogopa na kumtegemea Mwenyenzi Mungu na kuzivunja laana hizi za kichawi zinazolitafuna taifa tangu mwaka 1961 ?
Je nafasi ya mkuu wa wachawi wa taifa itafutika, au ipo wazi kwa muda?