Biashara ya Vifaa vya Ujenzi (Hardware Store): Ushauri wa Mtaji, Uendeshaji, Changamoto na Faida

Kwanini msichukue mkopo bank kama tayari mmeshapewa distributorship ? .... au
 
Ni kwel ukiangalia kwa benki hizo asilimia hua wanazitoa miezi 3 na kuendelea kwa hiyo kama ni mwezi 1 ni faida kubwa
 
Pia kama utaongeza mtaji hela pia itaongezeka lakini je kuna ukwel juu ya hili ?
 



Elimu nzuri sana.
 
Tukiacha za biashara, uimara wa tofali unatakiwa kuchanganya kiwango gani cha cement na mchanga?

Nahitaji kupiga tofali zangu binafsi za kujengea maana naamini zinazouzwa kunakuwa na uchakachuaji ili kutengeneza faida kubwa zaidi.
Hapa nilipo tofali moja ya inch 5 ni sh.1500.

Nikinunua mashine yangu binafsi ya kupigia tofali naamini naweza kuikodisha kwa watu na ikanirudishia faida pia.
 

Tofari 40 kwa mfuko 1
 
uimara wa matofali unategemea na aina ya mchanga, aina ya maji unayotumia, aina ya cement, machine inayotumika kuyatengeneza na umwagiliaji wa maji baada ya kufyatua hasa hasa siku sita za kwanza tokea kufyatua. Mchanga wa kolongoni au unaopatikana kwa kuuuzoa mitaani ni tofauti sana na ule unaochukuliwa kule bagamoyo au maeneo ya kibaha kule, nimeona maeneo ya boko dsm watu wanachukua mchanga wa bagamoyo wanauchanganya na ule wa kolongoni kwa ratio ya 2:3 kupata tofari nzuri na kafaida. nadhani ule wa bagamoyo ni mzuri zaidi. Maji yakiwa na acid au salt sana sio mazuri kwa kufyatulia matofali, wataalam wa cement wanalijua hili chumvi ni adui mkubwa wa cement kwenye quality ya kukamata udongo (binding effect), aina ya cement na zenyewe ni sababu nyingine sio kila cement inafaa ukiwaona wataalam wa cement watakushauri kwa ubora zaidi juu ya hili, Twiga, rhino na ile ya pakistan nadhani ni bora sana. suala la machine pia ni muhimu nadhani kwenye uimara tofari la machine ya mkono ni tofauti sana na aliyetumia machine ya umeme yenye vibration na hii pia inachangiwa na uchanganyaji wa cemet na mchanga kupata equal distribution(mchanganyiko ulio sawa). tofali ukiwa mzembe kuzimwagilia maji tegemea asara ya tofali kupasuka, tofali baada ya siku moja tokea ufyatue lazima ulimwagilie maji ya kutosha asubuhi na jioni kwa muda walau siku tano. huo ndio mchango wangu ahsante.
 
Nashkuru ndg REHEMA ZA MUNGU kwa ufafanuzi mzuri. Be blessed.
 

hii kiboko aisee yaani mfuko mmoja wa saruji utoe tofali 55 hadi 60 !!![emoji2][emoji2]
hii nyumba ikinyeshewa na mvua inamong'onyoka aisee...kwavile ni nyumba ya mchanga hii
 
Hii ilikua ni mwaka 2012 kipindi ambacho hata ungefungua duka la kope ungefaidika.

Kwa kipindi hiki biashara ya uhakika ni kuuza chakula tu.

Maana hata toilet paper siku hizi haziuziki tena. Sasa sijui ndiyo kusema watu wakitoka msalani wavuta kyupi juu na kusepa au wamerudi kwenye maji hata sielewi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…