uimara wa matofali unategemea na aina ya mchanga, aina ya maji unayotumia, aina ya cement, machine inayotumika kuyatengeneza na umwagiliaji wa maji baada ya kufyatua hasa hasa siku sita za kwanza tokea kufyatua. Mchanga wa kolongoni au unaopatikana kwa kuuuzoa mitaani ni tofauti sana na ule unaochukuliwa kule bagamoyo au maeneo ya kibaha kule, nimeona maeneo ya boko dsm watu wanachukua mchanga wa bagamoyo wanauchanganya na ule wa kolongoni kwa ratio ya 2:3 kupata tofari nzuri na kafaida. nadhani ule wa bagamoyo ni mzuri zaidi. Maji yakiwa na acid au salt sana sio mazuri kwa kufyatulia matofali, wataalam wa cement wanalijua hili chumvi ni adui mkubwa wa cement kwenye quality ya kukamata udongo (binding effect), aina ya cement na zenyewe ni sababu nyingine sio kila cement inafaa ukiwaona wataalam wa cement watakushauri kwa ubora zaidi juu ya hili, Twiga, rhino na ile ya pakistan nadhani ni bora sana. suala la machine pia ni muhimu nadhani kwenye uimara tofari la machine ya mkono ni tofauti sana na aliyetumia machine ya umeme yenye vibration na hii pia inachangiwa na uchanganyaji wa cemet na mchanga kupata equal distribution(mchanganyiko ulio sawa). tofali ukiwa mzembe kuzimwagilia maji tegemea asara ya tofali kupasuka, tofali baada ya siku moja tokea ufyatue lazima ulimwagilie maji ya kutosha asubuhi na jioni kwa muda walau siku tano. huo ndio mchango wangu ahsante.