Ndugu yangu
Udochi idea yako ni nzuri tu wala haina mashaka na kwa vile tayari umeshapanga fremu hapo ndio tunasema maji umeshayavulia nguo. Biashara hii kwa kweli ina siri kubwa (mimi sifanyi) kwanza kabisa unatakiwa kujua kwamba sisi wa Tz ni price sensitive sana, tunajali sana bei ya kitu husika. Mtu anaweza acha kununua kitu Gongolamboto akaenda kununua kariakoo kwa tofauti ya elfu moja tu. Gongolamboto kinauzwa elfu 6 kariakoo elfu 5. sasa weka picha vifaa vya pikipiki na kwa jinsi hao watu wanavyozurura dar yote. Kwa hio first approach tafuta mchina bei chee na utauza zaidi na kwa hio pesa uliyonayo unaweza kupata mzigo kidogo mkubwa, halafu tafuta vifaa ambavyo ni hot cake ambavyo vinauzika fasta kwa mfano plagi, wazo la kuwa na fundi pembeni sio baya lakini mimi kwa kuanzia nisingependa ufanye hivyo, unamleta fundi hapo wakati tayari umeweka mzigo kwenye frame umetuila, ila cha kufanya mtafute tu fundi akupe idea (fundi na sio dereva) ikiwezekana mlipe kidogo kwa information atakaokupa. Kwa kukusaidia mtafute mtu anaitwa
gkileo wa hapa hapa JF namba yake ya simu ni 0658131333. atakusaidia