Bibi harusi mtarajiwa, mama yake wafa ajalini wakielekea Kilimanjaro kwenye maandilizi ya harusi yake

Bibi harusi mtarajiwa, mama yake wafa ajalini wakielekea Kilimanjaro kwenye maandilizi ya harusi yake

Dah! Msiba mzito sana huu. Badala ya harusi, unakua msiba!! 🙁 All in all mashimo siyo kuyakwepa hata kidogo uwapo barabarani. Ni bora ufukie tu au upunguze mwendo.
Hii kwangu ni best comment kwa huu uzi. Ukiwa speed ukakwepa shimo inakutaka uwe na hesabu za haraka sana tofauti na hapo unaingia Lane ingine unakutana nacho
 
Pole sana kwa familia sema bibi harusi hakutakiwa kuendesha gari umbali mrefu huo bora wangekodi dereva tu kwa ajali nazokutana nazo bara barani hasa hii ya Dodoma kwenda Iringa wengi ni wale madereva wa nyumbani mjini harafu wanataka kuvuka mkoa bila hata ABC za Road...
 
Ajali hiyo iliyotokea baada ya Rehema aliyekuwa dereva wa gari hilo kukwepa shimo na kugongana na lori, pia imesababisha kifo cha mfanyakazi wa ndani wa mdogo wake, Irene Shija (15), huku wanafamilia wengine wawili wakijeruhiwa.
Kazi ya kuziba mashimo barabarani ni ya nani? Kodi si zinalipwa hili mashimo yazibwe? Je, ujenzi wa barabara ni wa viwango?
Kwa kifupi, mashimo barabarani na kusababisha vifo ni huduma mbovu anayopatiwa mwananchi.
Madereva, bora shimo kuliko lori.
 
Pole sana kwa familia sema bibi harusi hakutakiwa kuendesha gari umbali mrefu huo bora wangekodi dereva tu kwa ajali nazokutana nazo bara barani hasa hii ya Dodoma kwenda Iringa wengi ni wale madereva wa nyumbani mjini harafu wanataka kuvuka mkoa bila hata ABC za Road...
Ni kweli, kuna utamaduni wa kuendesha mjini, ambao ni tofauti na ule wa highway. Ukute hata hakumuwashia taa dereva wa lori na inaonekana alikuwa mwendo mkali sana, ingawaje yawezekana lori ndio lilikuwa kibati.
 
Ni kweli, kuna utamaduni wa kuendesha mjini, ambao ni tofauti na ule wa highway. Ukute hata hakumuwashia taa dereva wa lori na inaonekana alikuwa mwendo mkali sana, ingawaje yawezekana lori ndio lilikuwa kibati.
Kila unapopishana na gari iwe kubwa au ndogo inatakiwa kupunguza mwendo pindi ikitokea ajali isiwe na impact kubwa na kila unapolipita gari kubwa unatakiwa umsumtue kwa honi nae pia atakuruhusu kwa honi sio anaona gari limepita tu kama kicheche harafu mazingira mengine ni ya hatarishi ukiwa na abc za safari labda gari kubwa lije upande wako likugonge lakini kwa mazingira ya kawaida utakua salama sana...huwa naogopa sana kuwaona hawa madereva wa mjini wapo na Subaru harafu mwendo bati huku wamefunga vioo aisee...
 
Wakati wa bwana ufikapoo .....RIP

Mara nyingi shughuli za sendoff /harusi zikaribiapo wanashauri wahusika wasisafiri safiri ama kuendesha vyombo vya motooo
Apumzike kwa amani, ni Mungu tu anaetulinda mwaka jana nlisafiri toka nilipo hadi Songea 716Km kuhudhuria send off ya mamiloo.

Yeye alitangulia mimi nikatumia usafiri binafsi, alitangulia na usafiri wa public nakumbuka nilimwambia kwa nini tusiende wote akasema hapana anawahi kuweka mambo sawa nilihisi hofu ndani ya jibu lake.

Wakati wa kurudi tulirudi wote na wanafamilia kadhaa Mungu ni mwema tulifika salama na harusi ilifanyika, naunga mkono ushauri wa wadau hakutakiwa kuendesha.
 
Ingekuwa nchi za wanaojielewa, hilo shimo barabarani lingeinyoosha serikali. Kwa Tz matatizo, kadhia ndio maisha ya WaTz na yanapelekea mauti yao, na tumekubaliana nayo!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
Mashimo kwenye barabara zetu ni changamoto wiki mbili zilizopita Almanusra Toyota wish igongane na lorry maeneo ya dakawa kutoka Morogoro kwenda Dodoma.

Mvua inanyesha uono unakua hafifu ghafla unaona shimo ndio kilichomtokea dereva wa wish cha kushukuru alilikwepa na kwa haraka akarudi kwenye lane yake kuepusha ajali ya uso kwa uso, pona yangu ni umbali kati yangu na wish. Barabara zetu hasa kuu zinachangamoto madereva wanaopita kila mara walau wanaelewa mahali penye changamoto.
 
Salamu za pole kwa wanafamilia...

Wito:
Madereva wasio wazoefu wa safari ndefu za mkoa hadi mkoa si vyema kusafiri kwa kuendesha gari mwenyewe...

Hizi safari ndefu huwa zinahitaji umakini sana na muda wote akili inapiga kila aina ya hesabu uwapo barabarani kuepukana na majanga...

Kudance na mashimo barabarani kama sio mzoefu unaweza hata ukapindua gari au ukachochora...
Sahihi highway ajali ni kufumba na kufumbua ni hatari sana usipokuwa timamu Yani ukizembea kidogo tu hukawii kukutana na dhahama.
 
Back
Top Bottom