Bible Vs Science: Je ulimwengu una umri gani?

mpendwa mitale na midimu ahsante na hongera kwa maelezo yako nimekupata uzuri sana. lakini kadili ya maelezo yako binafsi ninamaswali kama mawili tu ivi:

1: kuna mahali umedai kuwa biblia toka mwanzo mpaka ufunuo ina kila kitu na kila fomula (kwa maana kwamba imejibu kila kitu ikiwemo na sayansi yenyewe kwa jinsi nilivokuelewa mimi). swali langu ni hil: ni nini lengo la biblia kwa mwanadamu, ni nini kusudi la biblia kwa mwanadamu, Mungu alikusudia biblia iwe na kazi gani kwa mwanadamu, au kwa nini biblia ???

mpendwa mitale na midimu kama jibu la swali hilo hapo juu kuhusu lengo la biblia kwa mwanadamu ni tofauti kabisa na sayansi na haikukusudiwa kufundisha sayansi, unafikiri ni sahihi au ni haki tunapongangania kutafuta sayansi/ kujifunza sayansi toka kwenye kitabu ambacho hakikukusudiwa kwa kazi hiyo ?.

sikitai kwamba kuna sayansi mbaya na wanasayansi wapinga Mungu/wakana Mungu uwepo wa hao hauifanyi sayansi yote kuwa ni dhambi au kuwalaumu wapinga Mungu kwa kila jambo kwa Mgongo wa sayansi sidhani kama ni sahihi. ninachojua mimi ni kuwa sayansi ni pato la AKILI na MAARIFA tuliopewa na Mungu kama zawadi itusaidie kumpenda, kujua zaidi nk katika maisha yetu ya kila siku. ndio maana imeandikwa usimwache elimu aende zake na pia mpende bwana Mungu wako kwa AKILI zako zote. sasa sayansi ndio moja ya mapato ya izo AKILI au tunaweza kusema ndo AKILI zenyewe. tulipewa mikono na miguu kwa ajili ya kazi njema ya kumtumikia Mungu na jirani lakini kuna watu wanaitumia iyo mikono na miguu kwa kuvunja amri za Mungu kama kuiba, kuumiza, kupigana nk sasa hapo sidhani kama kosa ni mikono au miguu ndivo ilivo kwenye sayansi pia.
 

https://www.cfa.harvard.edu/news/2011-15P

Quran na science ipi ina spuculatations zaidi?
 
Labda niulize je ni wakati gani unajua Biblia iko lateral au figurative

Mkuu,watu wasipokubali kuisoma Biblia kama Kitabu chenye Vitabu vingi, waandishi wengi,chenye Lugha mbili, kila kitabu kikiandikwa kwa wakati wake na kwa watu mbalimbali na kwa staili tofauti tofauti, watu wataishia kupotoka na kupotosha wanaowasikiliza. Jambo hili ndilo limepelekea kuwepo madhehebu kibao ya Kikristu.

Kadri ya Roho Mtakatifu atakavyotujalia,sisi wengine tutazidi kupanda mbegu mpya kwamba baadhi ya mambo yanavyochukuliwa na watu haiko hivyo. Wenye kuhitaji kujifunza watafanya utafiti na Wahafidhina watadumu katika upotofu wao huo huo.
 
kwahiyo dunia iliumbwa kwa siku ngapi,au haikuumbwa,au ilijiumba,au mungu aliikuta

Kaka Swali lako ni zuri, lakini kama ungenifuata tangu mwanzo ungeuona msimamo wangu kadiri ya mimi nilivyoelewa,
kifupi
1. Dunia imeumbwa na Mungu
2. iliumbwa kwa zaidi ya siku sita (Mwanzo 1:1-2)
3. ilikuwa transformed na kuwareshaped ndani ya siku sita (Mwanzo 1:3-)
 
Bibles imeeleza wazi kuwa kwa Mungu siku moja ni Kama Mika 1000 na mikia 1000 ni Kama siku moja !
 
Wamepima kuanzia Adam alipoumbwa!
Mbona tunasoma humu ndani Kuwa Dunia ilikuwa ina watu kabla ya Ujio wa Adamu?

Samahani kama nitakuwa sijaeleweka maana sipo vizuri kwenye hizi mambo.
A fool says in his heart there is no GOD!
 
Katika physics ya wenzetu walioendelea nimeona wakizungumzia kuhusu Time travel,,kwamba mtu Unaweza kurudi backward kwenye muda mwingi uliopita,,,au ukaenda mbele sana kwenye mda ujao...nafikiri kwa kutumia hio time machine tunaweza kujua mda gani umepita...

Kibiblia Kuna sehemu inaitwa ulimwengu wa roho,,huko kuna kila kitu muda iliopita na ule ujao wote upo na hata mtu akitaka kujua habari za Mambo yote yajayo tayari yameshaumbwa yote..Kwamba dunia ina miaka mingapi bado sijakubaliana na upande wowote na zidi kupitia nipate Maarifa,,,ya biblia ina tatizo maana mwandishi kashindwa kubainisha mwanzo sahihi ni upi
Kuhusu miamba shule nilifundishwa aina tatu za miamba geu,,moto na wa tatu siukumbuki,, swali langu ni kwamba je sampuli za hii miamba yote ,zilisoma miaka hio bilioni?
 
Hakuna anae weza jua umri halisi wa dunia mpaka awe na uhakika wa origin yake af sie wote tumefuata baada ya mazingira kuwepo Ko ni ngumu kujua vinginevyo mtaleta thesis Za uongo tu hapa
 
Kwanza neno tym lenyewe ni controversial.
Reference Chinese yrs, Gregorian calendar, Arabic yrs or Islamic yrs
Siku moja kwangu ni kama siku elfu moja na siku elfu moja ni Kama siku moja. Asema bwana @confusion of Confucius
 
Hakuna anae weza jua umri halisi wa dunia mpaka awe na uhakika wa origin yake af sie wote tumefuata baada ya mazingira kuwepo Ko ni ngumu kujua vinginevyo mtaleta thesis Za uongo tu hapa
Hapana mkuu unaweza kujua kama ukitumia experiments za kueleweka kwa mfano ukijua kwamba mwili wa binadamu ukifa una characteristics zipi kwa kila siku inayoisha kiasi ukiokota mzoga ni rahisi kujua amekufa lini sababu unapima zile characteristics za ile experiment yako.

Kwa kusema hayo kama kuna mwamba ambao uko proven kwamba kila baada ya miaka let's say 20 unaongezeka layer flani basi utatumia hio kufanya estimation ya total half lives ya hizo layers kupata origin ya hilo jiwe na matokeo yakiwa consistent kwenye experiment nyingi basi hiyo methodology inakubaliwa.

So hapa kikubwa ni kujua tabia ya miamba in different periods ndipo unatengeneza formula ya kugundua ni level ipi ilianza na ilichukua muda gani.... Simple and clear

Ndio maana leo hii unaweza ukafa tukaokota fuvu ila tutajua ulikuwa jinsia gani na ulizaliwa mwaka gani ingawa Hatujawahi kukuona ukiwa hai, hivyo kusema hakuna aliyekuwepo hivyo hatuwezi kujua si sahihi pale ni formulae tu.
 
Ndio mkuu walipopima sampuli za baadhi ya miamba karne iliyopita Wanajumlisha half-life (umri) wa kila layer ya huo mwamba ndio wakagundua ni 4.5 Billion. Mfano kama unajua kila baada ya miaka billion 1 ndio mwamba unatokea layer au element fulani si unafanya hesabu za jumlisha tu kwa zile layer unapata total duration ya huo mwamba.

Muhimu hapa ujue tu characteristics za hiyo miamba kila baada ya muda fulani basi unatumia hayo maarifa kutambua umri wa mwamba mfano kama unajua mtu wa miaka 60 huwa anatoka let's say mvi za blue na akifika miaka 100 anatoka mvi za kijani sasa basi ukikutana na mzoga wenye mvi za kijani hutosema huyo mtu alikufa na miaka 100??

 
mkuu sio ussher ni Mungu ndie anasema aliumba dunia kwa siku sita.
Labda hapo ipaweke sawa kuwa Mungu alimaanisha nini? siku sita lateral days au mamilioni ya miaka kwa mujibu wa wanasayansi wasioamini uwepo wake na uumbaji wake huu tunaoujadili.
Dunia wala Ulimwengu kwa maana ya miamba haukuumbwa kwa siku sita, mnamtafsiri Mungu tofauti. Zile siku sita za Kimungu kwa sababu Gregory calendar tunayoifuata haikuwepo wakati huo Mungu aliumba vitu vya kuujaza Dunia. Mwanga siku ya kwanza na uumbaji mwingine siku zilizofuata. Tahadhari tu, Hizi siku sita ni za Kimungu na sio 24hrs za kwetu. Uumbaji wa kibiblia unaendana kabisa na ugunduzi wa kisayansi. Kulikuwepo kwanza na uumbaji wa miamba ambao haukuzungumziwa kwenye Biblia, ukafuata kuwepo kwa mfumo wa mwanga nk. Mwanzo 1 haikuenda mbali kuelezea uumbaji kwa sababu sio objective ya Bible. Kwa wale wasomaji watanielewa. Main objective ya Bible ni Salvation of Mankind baada ya anguko. Na ndio maana mimi sitaki kwenda deep kutumia Bible kwenye kuelezea mambo ya uumbaji
 
Wakati naanza shule mtaani kwetu hapa kuwa na makorongo Bali palikuwa na visima visivyoisha maji, kama dunia ina mika 4 bln basi mtaa wetu ungekuwa makorongo kila kona na visima nisingevikuta tena, sasa nawaambieni ukweli tu kwa ninavojua huyo wa miaka 6000 yuko sahihi kuliko wa 4bln, yaan kifaa kijue umri wa Uhai halafu hakipo hai[emoji23] [emoji23]

Wanasayansi tuacheni kidogo nasisi tuna Akili za asili eti.
 
Mkuu kinachopimwa ni TABIA sio umri as umri mfano nimetoa hapo ufanye utafiti ugundue let's say mzee wa miaka 60 ana mvi nyeupe then mzee wa miaka 80 ana mvi za blue na mzee wa miaka 100 ana mvi za kijani. Sasa basi ukiokota maiti ina mvi nyeupe huwezi kukadiria kuwa aliyekufa aliishi miaka 60??

Ndio hivyo hivyo kila layer/element kwenye mwamba inachukua muda fulani kubadilika tabia zake kama kuoza n.k hivyo basi kwa kuwa walishapima wakagundua inachukua let's say miaka 10 mwamba unabadilika tabia fulani sasa wakikuta mwamba una layer kama 1000 tofauti si watafanya tu 1000×10 watapata umri wa mwamba!!!

Sawa tu na mkojo unaweza pima umri wa mtu sababu licha ya kuwa hizo mashine za kupima hazikuwa hai kujua ulizaliwa lini na wapi ila zinafahamu tabia za vimelea vya baadhi ya tissues za mwili wao hivyo zikionekana ni rahisi kujua huyo mtu ana range ya umri gani duniani

Kwahiyo inapimwa TABIA za MABADILIKO na zinajumlishwa half lives zake wanapata makadirio ya umri wa mwamba husika
 
https://www.cfa.harvard.edu/news/2011-15P

Quran na science ipi ina spuculatations zaidi?

Nashukuru kwa kuthibitisha hoja zangu. Qur'an itabaki kuwa ni SI Unit ya Science. It is a divine book and a guidance to human being of all ages. Yet, not a scientific book.

HOJA ZANGU MUHIMU:
1. Umri wa Dunia ndiyo umri wa Solar system (SUN) and universe kwa ujumla wake. Kwa sababu vyote vimepatikana baada ya Big Bang.
2. 13.8 Billion years of the Universe ni speculation and hypothesis based on standard model since Radiometric dating ya kupima miamba ndiyo so far actual experimental tool inayotumika kukadiria object zingine. Hatujapata particles zilizotoka kwenye Nebula tukatumia radiometric dating kupima umri wa Nebula. Na Wala mwanadamu hajafika kwenye Nebula (dark matter)

3. Pamoja na kuwa Dunia ina mazingira yanayo-support Maisha yawepo wanasayansi hawajui ni conditios zipi zinazofanya Maisha yawepo. NA HUU NI UTHIBITISHO WA KUWEPO MOLA MLEZI NA MWANZILISHI WA UHAI.

https://www.cfa.harvard.edu/news/2011-15P

Excerpts from the web:

Our Solar System

Although our Sun is an ordinary star, the Solar System is the only planetary system known to harbor life. Studying the Solar System enables us to learn how stable planetary systems form and how planets develop the conditions needed for life.

Stars, Planets and Origins
We think we know how stars live and die, but our picture of how stars form to begin with is incomplete. Although astronomers have discovered more than 1000 planets in other solar systems, we do not really know what conditions actually produce life.


Galaxies
Soon after the Big Bang, the Universe became a space filled with "stuff:" neutral gas, dark matter, and radiation. After several hundred million years, primitive structures began to form from the first chemical elements, creating the first massive stars and eventually the first galaxies.

Cosmology
Working from the standard model of the "Big Bang" some 14 billion years ago, we are investigating the early epoch of inflation and the nature and role of dark matter in the evolution of structure in the Universe. We also seek to understand the nature and properties of the "dark energy" that is speeding up the expansion of the Universe.


Laboratory Astrophysics
Science is successful because the physical laws we discover on Earth work everywhere and everywhen. We use laboratory experiments to expand our understanding of physical processes and then apply these results to processes throughout the Universe.


Extreme Astrophysics
The most violent and energetic phenomena in the Universe include gamma-ray bursts, supernova explosions, black holes, neutron stars, and the as yet unidentified cosmic accelerators which produce the highest energy photons and cosmic rays.
 
Mwenyez mungu ndie muumbaj wa dunia pia mwanadamu wa kwanza ni adam,mambo ya bing bang sijui evolution ni uzushi tu.
Je kama dunia ina miaka bilion kadhaa, virutubisho ardhini visingekuwepo kutokana na radiations.

"Wanamacho nao hawaoni,wana masikio nao hawasikii"

Mche mungu hakika utajua kilichofichwa ndani ya maandiko
 
Adamu mtu wa kwanza mkuu?? Au ni mtu wa kwanza kuchaguliwa na Mungu?? Maana akiwa mtu wa kwanza italeta utata hasa kwa wakazi wa zile nchi zilizotajwa kuwepo nje ya bustani ya Edeni kama Kush,Nod na kadhalika walitokea wapi

Anyway mada haipingi uumbaji wa Mungu ila inataka tu kufahamu je toka dunia iumbwe mpaka leo imepita miaka mingapi.... Kwa mujibu wa maandiko au kisayansi yupi unaona ni accurate na kwanini??

Ubarikiwe
 
Kwa Sababu Mungu Amesema ni siku sita na Ya Saba akapumzika.
Sing'ang'anii Bali nang'ngania alochosema Mungu.
Wakati anasema hayo alijua yeye alifanya hayo, na alijua kuwa hayukomlimited na space na time.
Kwa Sababu alichokisema kwa habari za Siku kulikuwa na practical reference na hata sasa uzao wa walioambiwa wanaendelea kukitekeleza practically sio njozi au hekaya. Siku sita wanafanya kazi siku ya Saba wana Pumzika sawasawa na maelezo manyoofu ya Muumbaji.

Nakusihi mkuu, Tuchague mkumsikiliza Mungu kwanza kabla ya rational human ideas.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…