Kaka Hakuna mtu anayekataa kuwa Mungu hakuumba vitu vyote, unajua Kitabu cha Mwanzo ukikisoma vizuri kina kila kitu unachokiitaji kwenye hii Dunia, Kuna sayansi kubwa sana pale, kuna elimu nzito kabisa
sasa twende polepole
Mwanzo 1:1-2 Mungu alifanya nini?
1. Aliumba mbingu na nchi (Ardhi)
2.Nchi ilikuwa Giza, ukiwa na utupu
3. kulikuwa pia na vilindi vya maji
so hivyo vyote viliumbwa nje ya zile siku sita, je baada ya kuumbwa hivi vilikaa siku ngapi kabla ya zile siku sita ?
umetoa andiko la Kutoka 20:11, ni kweli ndani ya siku SITA mUNGU ALIUMBA BAHARI kwa kutenganisha maji na ardhi, Mwanzo 1:6 Mungu akasema na liwe anga katikati ya maji LIKAYATENGE MAJI NA MAJI, Mwanzo 1:9 naMaji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja ili pakavu paonekane.........
Kaka
mitale na midimu ,
maandiko yote ya kuanzia Mwanzo 1.3-10 kitu kipya alichokiumba mungu kutoka vile vilivyokuwa awali Mwanzo 1:1-2 ni NURU pekee, lakini vingine kama Maji , Nchi, Giza alishaviumba kabla
Baada ya Mungu kukamilisha kuitransform Dunia iwe na mazingira ya kusupport uhai ndio kuanzia Mwanzo 1:11 na kuendelea anaanza kuweka Mimea na viumbe hai
MIMI NINACHOAMINI MUNGU ALIIUMBA DUNIA MIAMBA NA MAJI NA ILIKUWEPO KWA MUDA MREFU SANA, KISHA AKAPANGA MIPANGO YA KUWEKA VIUMBE HAI, LAKINI ILIBIDI LAZIMA AANDAE MAZINGIRA YA KUWAWEZESHA HAO VIUMBE HAI NA MIMEA IWEZE KUKUA NA KUSTAWI KWA UZURI, NDIO SASA MUNGU NDANI YA SIKU SITA ANAITRANSFORM DUNIA NA KUIPA MAZINGIRA YA KUWEZA KUTUNZA VITU HIVYO VYOTE
KITABU CHA MWANZO NI KITABU KIZURI SANA, NDIO MWANZO WA DUNIA NA NDIO MWANZO WA SAYANSI