Bible Vs Science: Je ulimwengu una umri gani?

Bible Vs Science: Je ulimwengu una umri gani?

Ungeonyesha utofauti wa Kalenda ya Kiyahudi kule Babiloni na Baaada ya kurudi na Je Uliathili Mfumo wa Siku sita fanya kazi siku ya saba Pumzika kama walivyoishi kule jangwani?
Je unakubaliana na mimi hawakwenda utumwani taifa lote kabisa kuna masalia walibaki?
Lkin licha ya kalenda kubadilika Mfano Mwezi Habib kuitwa Nissan, unakubaliana kuwa kwa sababu walikaa miaka 70 tu huko na walikuwepo wacha Mungu huko na manabii pia kama Ezekiel, Daniel na wakina ezra kumbukumbu hazikupotezwa hasa kwa maana ya week days seven?

Ndio maana tunasema ni makadilio ila makadilio hayo hayawezi kuturudisha katika miaka milioni.
Ukokotozi wa miaka hiyo unabase katika uzao wa Adam wa kitabu cha mwazo sio Ibrahim. Kama Adam aliishi miaka 900 mfano, Mwaka moja wake utaanza siku aliyoumbwa, dunia ikiwa na umri wa siku tano.
Ungejenga hoja kuanziq hapo sio Ibrahim.

Kuhusu Matendo na Mwanzo nq ukanganyaji wa Umri.
1: Ikiwa kweli kuna huo mkanganyiko, Bado creationist wako sahihi maana hauna range ya malaki au mamilioni bali makumi.
2:Lkn matendo sioni kama imekosea maana imetaja vituo Viwili. Alipotoka kwa wakaldayo (ur ya wakaldayo) hakwenda kaananinmoja kwa Moja, Alienda Harani, Baadae akatoka harani akaenda Kaanani.
Sasa Yeye hasemi alipotoka kwa baba Yake kule Ur (75Years), Bali aalitoka harani sio kwa wakaldayo baada ya kufa kwa baba Yake. Umejumlisha miaka ambayo haina uhusiano, labda kama kuna sehemu hatujelewana mkuu wangu.
Mkuu naamini Wote tunafahamu kwamba kalenda ya kiebrania ilikuwa na siku 354 ama pungufu ilihali calendar ya gregory ina siku 365 hivyo tunapishana takribani wiki mbili na miaka ya sasa hivyo basi ukichomoa wiki 2 kwa kila miaka 6000 je huoni utapata miaka pungufu zaidi kulingana na Gregorian calendar ambayo ndio inahesabu full mzunguko wa dunia kwa jua ? Mpaka hapo huoni hakuna accuracy kwenye hiyo calendar aliyotumia Usshe na YEC???

2. Nimejenga hoja kuhusu Abraham sababu genealogy yake imehesabiwa kwenye kukotoa miaka ili kupata family tree ya kuanzia Adam mpaka Yesu hivyo miscalculation ya umri wake itaaffect general result haijalishi kwa makumi au mamia maana mistakes kwa abraham ikijirudia kwa family tree nzima itabadilisha kabisa number ya jibu la mwisho so tusipuuze.

Hapo Biblia iko wazi kuwa Aliondoka Haran akiwa na 75 ila kitabu cha matendo kinadai by 135 ndio alitoka Haran Sasa huoni hapo kuna errors za calculation?? Kama zipo huoni ussher methodology tayari haina credibility??

Tuanzia hapo
 
Hapana nachomaanisha je Dunia hii ina umri gani na sio VIUMBE vina umri gani maana obvious Dunia lazima iliumbwa kwanza kabla ya mwanadamu hivyo natamani nifahamu upi ni umri sahihi wa Dunia ni ipi maana Ussher alichosema ni kwamba Dunia iliumbwa siku sita kabla ya Adam kuletwa duniani na ndio maana nikaona nilete hii mada humu tusaidiane kujua nani mkweli kuhusu suala hili.
Mkuu zitto junior,
Kutokana na nadharia nyingi sana zilizopo hadi leo kuhusiana na UMRI wa dunia, zikiwepo hizo ulizozielezea; ni ukweli usiopingika kuwa SI VYEPESI hata kidogo kujua umri wake sahihi.
Ila kwa msingi wa Biblia, INAWEZEKANA dunia ina mamilioni elfu au mabilioni ya miaka kwa sababu ya lile neno linalosema "Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji" (Mwanzo 1:2) ambapo uwepo wa nchi/ dunia ulidumu kwa muda fulani usiotajwa kabla ya Uumbaji wa vitu vingine kuanza.
Na dunia yote, yaani lile DUARA linaloitwa DUNIA lilikuwa limezama kabisa kabisa ndani ya maji kwa mamilioni ya miaka KABLA Mungu hajaamua kuliibua duara hili na kulifanyia modifications ambazo zilipelekea viumbe kuingizwa.

So, logically, dunia ina miaka mingi sana kuliko hata hiyo 4.5 bilioni!

Kwa nadharia nyingine, tunaweza kusema KAMA SHETANI alitupwa huku duniani kabla ya Adam (na ndivyo inavyosadikika) basi ni wazi kulikuwepo na viumbe wengine waitwao WATU lakini si kama tulivyo sisi na inawezekana 'watu' hao walifutika duniani na ndipo dunia ikazamishwa kabisa ndani ya maji kwa kipindi kisiweza kujulikana, lakini kirefu sana kwa mabilioni ya miaka. Ni hadi pale Mungu alipoiibua dunia na kufanya uumbaji upya ambapo huyu aitwaye Adam aliumbwa kwenye namna fulani ya mfanano na Mungu!

Najaribu tu kutafakari kwa kuunganisha facts za kisayansi na maandiko ya Biblia.

Ahsante.
 
Hapana nachomaanisha je Dunia hii ina umri gani na sio VIUMBE vina umri gani maana obvious Dunia lazima iliumbwa kwanza kabla ya mwanadamu hivyo natamani nifahamu upi ni umri sahihi wa Dunia ni ipi maana Ussher alichosema ni kwamba Dunia iliumbwa siku sita kabla ya Adam kuletwa duniani na ndio maana nikaona nilete hii mada humu tusaidiane kujua nani mkweli kuhusu suala hili.

Kwanza hapa nataka kutia neno,nataka nijue kwanza aliposema dunia iliumbwa siku sita alimaanisha nini ? Yaani kwake yeye dunia ni nini ?

Maana kuna dunia (Earth),kuna mbingu na kuna vyote vilivyomo baina ya dunia na mbingu.
 
Mkuu mitale na midimu post yako #93 umekataa kuwa hakuna codes labda nikupe case ya Daniel

Daniel 12:4

4 Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho.

Hapa anaambiwa ayafunge mpaka wakati sahihi wa kufunuliwa ukifika!! Upi huo?? Twende pamoja Daniel alipouliza

8 Nami nikasikia, lakini sikuelewa; ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, mwisho wa mambo haya utakuwaje?
9 Akasema, Enenda zako, Danieli; maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho

Sasa kama hata Daniel mwenyewe kuna codes aliandika haelewi maana yake na hata ufafanuzi hakupewa je kwanini usiamini Biblia imejaa codes??

2. Isaya 29:11
11 Na maono yote yamekuwa kwenu kama maneno ya chuo kilichotiwa muhuri, ambacho watu humpa mtu aliye na maarifa, wakisema, Tafadhali ukisome hiki; akasema, Siwezi, kwa kuwa kimetiwa muhuri

Hapa pia twaona kuna maneno ya Biblia yako sealed hivyo watu hawawezi kuyaelewa hata wangekuwa na maarifa kiasi gani sasa kama Isaya alitambua hili linawezekana kwa kuwa Biblia iko sealed sasa kwanini unakataa kuwa Biblia haina codes??

Hapo bado Yesu naye alitumia parables ambayo hakueleweka kabisa hta kwa wanafunzi wake je vipi kwetu sisi huoni hta hayo mafumbo tunaweza kushindwa kudadavua hata??

Karibu
 
Kwanza hapa nataka kutia neno,nataka nijue kwanza aliposema dunia iliumbwa siku sita alimaanisha nini ? Yaani kwake yeye dunia ni nini ?

Maana kuna dunia (Earth),kuna mbingu na kuna vyote vilivyomo baina ya dunia na mbingu.
Dunia alimaanisha EARTH tunayoishi hakuzungumzia pluto wala hizo sayari zingine alijikita kuwa dunia imeumbwa siku 6 tu hivyo dunia sasa ipo na umri wa 6022??
 
Wamepima kuanzia Adam alipoumbwa!
Mbona tunasoma humu ndani Kuwa Dunia ilikuwa ina watu kabla ya Ujio wa Adamu?

Samahani kama nitakuwa sijaeleweka maana sipo vizuri kwenye hizi mambo.
Watu??? Sio kweli.
 
Dunia alimaanisha EARTH tunayoishi hakuzungumzia pluto wala hizo sayari zingine alijikita kuwa dunia imeumbwa siku 6 tu hivyo dunia sasa ipo na umri wa 6022??

Maoni yake hayo ninayapinga kwa mtazamo wa imani yangu.

Kwenye imani yangu kuna dunia,kuna mbingu na kuna vilivyomo. Dunia iliumbwa kwa siku mbili,mbingu kwa siku mbili na vilivyomo vililetwa kwa siku mbili pia,yaani kwa muda sawa. Sababu Mola wetu mlezi akisema jambo kuwa na linakuwa.

Kwa mapokezi ya uislamu yamekuja kusema hiyo siku moja kwa Mola wetu muumba kwetu ni miaka elfu moja na kwa mapokezi mengine husemwa sawa na miaka elfu hamisini.
 
Mkuu unaweza ukawa sahihi bado kama dunia imejengwa kwa siku 6 ila swali langu je toka hizo siku sita mpaka leo je miaka mingapi imepita?? Maana nataka kujua umri wa dunia ni miaka mingapi
 
Mkuu unaweza ukawa sahihi bado kama dunia imejengwa kwa siku 6 ila swali langu je toka hizo siku sita mpaka leo je miaka mingapi imepita?? Maana nataka kujua umri wa dunia ni miaka mingapi

Hapa namaanisha ya kwamba hatuwezi kujua usahihi wa umri wa dunia.

Kielimu kuna kuangalia mambo ya faida na yasiyo na faida kuyapuuzia au kuyaacha kabisa. Kwa maana kujua umri wa dunia si jambo la msingi si kwangu wala si kwako wala si kwa wale. Tunatakiwa kutosheka tu na kujua ya kuwa dunia,ardhi na vilivyomo vimeumbwa ndani ya siku sita. Kwahiyo basi kujua umri wa dunia na kutokujua hakuna faida yoyote wala hasara,na elimu imejengeka katika hakika na si kubahatisha na dhana.

Nakuja ....
 
"History is the key to the future.." by knowing the history and the beggining earth we might as well predict its end and prevent the end from happening..mkuu kama binadamu wangekua na mtazamo kama wako binadamu tungekuwa bado primitive
 
Kutokuwa na mtazamo kama wangu kumefanya ukweli usahaulike.

Kama unajishughulisha na elimu na misingi yake utakubaliana na mimi.

Kwanza mtazamo huu ni miongoni mwa adabu za kutafuta elimu,pili mtazamo huu unakuepusha na kubahatisha,kadhalika mtazamo huu unazindua kujua lipi linawezekana na lipi haliwezekani na kuifanya akili kuwa imara zaidi.
 
Lakini kama ukiitaka historia bila kuwa na misingi imara ya kuitunza historia hiyo ni kazi bure.
 
Kutokuwa na mtazamo kama wangu kumefanya ukweli usahaulike.

Kama unajishughulisha na elimu na misingi yake utakubaliana na mimi.

Kwanza mtazamo huu ni miongoni mwa adabu za kutafuta elimu,pili mtazamo huu unakuepusha na kubahatisha,kadhalika mtazamo huu unazindua kujua lipi linawezekana na lipi haliwezekani na kuifanya akili kuwa imara zaidi.
Mkuu hakuna knowledge isiyo na benefit... unajua kwamba moja kati ya vitu vya msingi katika establishment of a mine ni kujua history na origin ya miamba katika eneo husika??

Na unajua kwamba Universal gtavitation law was published in 1680's even before the first visit in space 1900's?? kwa huo mtazamo wako ungemuona newton ni mwendawazimu na anapoteza muda.... Hii ni kukuonyesha tu kwamba the only limit is ur mind knowledge has no limit..
 
Ziko elimu kibao zisizokuwa na manufaa.

Elimu ina mipaka yake na vijenzi vyake.

Unazungumzia space ipi ?

Msingi wa elimu ni kuepukana na kukosea. Sasa kama elimu imejikita kwenye kukosea kosea na kuzua,manufaaa yanapatikana wapi hapo ?

Mfano uchawi una faida gani ?
 
Uzi unahusu biblical and scientific knowledge sasa uchawi sioni kama unaingia hapo..
Mtazamo wangu ni kwamba the Bible dont provide the math kuonyesha exactly dunia ina umri gani (hesabu zinazofanyika hapa ni fake guesses tu) lakini the same bible haijatoa limitations za kutafuta ukweli kwa kutumia njia za kisayansi, na sayansi inaprovide proven facts (unless proven wrong by another scientific fact)ambayo ni miaka 4.6b..
Everthing is knowledge acha kukaza ubongo
 
Back
Top Bottom