Wazolee
JF-Expert Member
- Sep 1, 2018
- 3,183
- 3,660
UISLAM ILIKUWEPO KABLA YA MTUME MUHAMMADMAKELELE Mengi yamejaa UJINGA na uongo MTUPU.
Usihangaike na MAKELE
1. UISLAMU ULIANZA LINI NA MOHAMED ALIZALIWA LINI?????????......
Hadi nakuonea huruma.
Nje ya Quran ILIYOANDIKWA Mwaka 600 hakuna UISLAMU.
HAKUNA UISLAMU HAKUNA
NGUZO TANO ZA UISLAM NDANI YA BIBILIA
1) KUTOA SHAHADA /KUAMINI MUNGU NI MMOJA TU
Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Yesu alikuwa muislam ndio maana hapo anashuhudia kuwa Mungu ni mmoja na yeye ametumwa na huyo Mungu mmoja
2) KUSALI KWA KUSUJUDU / paji la uso kugusa aridhi
Mathayo 26:39
Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.
Yesu hapo anaomba huku paji lake la uso likiwa limegusa aridhi Yani amesujudu
2 Mambo ya Nyakati 7:3
]Wakatazama wana wa Israeli wote, uliposhuka ule moto, utukufu wa BWANA ulipokuwapo juu ya nyumba; wakasujudu kifulifuli hata nchi sakafuni, wakaabudu, wakamshukuru BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele.
3) KUTOA ZAKA
Hi Haina ubishi Kila mtu anaijua
4) KUFUNGA SAUMU
Yeremia 36:9
[9]Basi, ikawa katika mwaka wa tano wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kenda, watu wote waliokuwa katika Yerusalemu, na watu wote waliokuja Yerusalemu kutoka miji yote ya Yuda, wakapiga mbiu ya kufunga mbele za BWANA.
Yoeli 1:14
Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini,
Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi;
Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu,
Na kumlilia BWANA,
5) KUENDA HIJA / NA KUANGALIA KIBLA UNAPOSALI
Kwa Sasa kibla ni msikiti wa maka waislam wote duniani wanapofanya ibada wanatakiwa waangalie huko na wenye uwezo waende huko
Waislam wa zamani pia walikuwa wanaenda hija walipo chaguliwa na Mungu
Kumbukumbu la Torati 12: 5
Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika kabila zenu zote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe wende huko;
[6]pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na ya kondoo;
Kipi kipya hapo tunachofanya sisi ambacho waislam wa zamani hawakufanya?