Biblia: Kitabu cha Mkanganyiko au Neno la Mungu?

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,213
Reaction score
2,938
Hivi kweli akili zenu zimefungwa na kufuli la Wazungu mpaka mmeshindwa kuona ukweli ulio wazi? Yaani hapa duniani hakuna kitu kinachochanganya na kuvuruga akili za watu kama hiki kitabu cha Wazungu!,
Yaani Biblia!.

Inakuwaje Mungu aliyeumba mbingu na ardhi, mwenye akili na mamlaka, aandike kitabu halafu ATUCHANGANYE kiasi hiki? Hivi mnamfanya Mungu ni mwandishi wa hadithi za abunuasi au ni nini? Mnataka kutuambia Mungu ni mbabaishaji kiasi hicho?

Angalia huu upuuzi! Wasabato wamekomalia kuishika siku ya Jumamosi, wanakuambia ukigusa kazi siku hiyo wewe ni dhambi! Dakika hiyo hiyo, wengine wanakuambia, "Acheni ushamba, Jumamosi ilikuwa ya Wayahudi, sasa hivi ni Jumapili, siku ya kufufuka!" Halafu wanakuja wengine wajuaji zaidi wanakuambia, "Ah, Sabato haihitaji siku, Sabato iko moyoni!"

Hivi mnatufanya sisi ni watoto wadogo? Mungu gani huyo anayetoa maelekezo ya siku ya kuabudu halafu kila mtu anaelewa chake? Hiki kitabu cha Wazungu kimejaa mkanganyiko kiasi kwamba hata mkipewa miaka elfu moja, hamtakaa muelewane! Ni machafuko matupu!...

Hapa ndipo kichekesho kikubwa na cha kusikitisha kilipo! Ili uelewe hiki kitabu kinachojichanganya, unaambiwa mpaka umuite ROHO MTAKATIFU aje akueleweshe!....
Yaani Mungu atupe mwongozo wa maisha, halafu wakati huo huo tumuite Roho atueleweshe? Kwani hicho kitabu kimeandikwa kwa lugha ya majini?..

Huyo Roho anayewaambia Wasabato wasile nguruwe, ndiye huyo huyo anayewaambia wa Jumapili wale nguruwe. Huyo ni Roho Mtakatifu? au ni roho ya kuchanganyikiwa iliyopandikizwa na Wazungu ili kutuvuruga akili..

Biblia hiyo hiyo inatumika na watu wanaopiga marufuku kucheza kanisani, wakisema ni fujo.
Halafu Biblia hiyo hiyo ndiyo inayotumiwa na wengine kuruka sarakasi, kupiga ngoma na mayowe utadhani wako disko, wakisingizia Daudi alicheza mpaka nguo zikaanguka!.......

Hivi huu si ni uwendawazimu? Kitabu gani hicho ambacho hakina msimamo? Leo kinaruhusu, kesho kinakataza! Huu ni mtego wa Wazungu wa kutuvuruga akili ili tu.

Utasikia mchungaji anasema, Roho ameniambia ukitumia maji haya ya baraka, unakanyaga mapepo! Biblia hiyo hiyo inatumika kuhalalisha biashara ya maji, mafuta, na vitambaa vya upako utadhani mko sokoni! Hivi Mungu amekuwa muuza maduka ya jumla?..

Mwingine anakuja na mstari wake, anasema "Roho anasema panda mbegu ya milioni moja ndiyo ufunguliwe! Maskini anatoa mpaka senti ya mwisho akitegemea muujiza, huku mchungaji akinunua gari la kifahari kwa kutumia Biblia hiyo hiyo!

Huu ni uhuni! Inakuwaje Mungu aandike kitabu ambacho kinampa nafasi tapeli yeyote kujiita Mtumishi wa Mungu halafu anatumia ujanja wa maneno kuwapokonya watu haki zao? Huu mkanganyiko ndio unazalisha hawa manabii wa uongo wanaochipuka kila kona....

Hebu niulizeni Inakuwaje Mungu aliye mmoja, mwenye akili timamu, aandike kitabu ambacho kinashindwa kutoa msimamo mmoja kuhusu mambo ya msingi?
Huyu anasema kusuka nywele ni chukizo, yule anasema ni urembo wa uumbaji..

Hivi huyo ni Mungu au ni mchezo wa kuigiza wa Wazungu? Huwezi kuwa na kitabu ambacho kinasema NDIYO na HAPANA kwa wakati mmoja! Huku ni kutuona sisi kama hatuna akili!..

Geukia upande wa pili uone wenzenu walivyojipanga. Kurani haina hizi sarakasi za kijinga!.
Kwenye kitabu cha Waarabu, sheria ni msumeno inakata pande zote! Hakuna cha tajiri, hakuna cha maskini, hakuna cha nabii wa uongo wa kujitungia tafsiri.
Kimepangika, kimeeleweka, na hakihitaji upako wa ziada kuelewa kuwa dhambi ni dhambi!..

Kama kitabu chako kinakufanya ubishane na jirani yako kila siku badala ya kukuleta kwenye toba ya kweli, basi hicho ni kitabu cha kuvuruga watu! Amkeni! Mungu hawezi kuwa mwandishi wa machafuko. Acheni kufuata hadithi za Wazungu zinazohitaji sarakasi za kiroho kueleweka.

Tafuteni neno lililonyooka ambalo halitupi nafasi ya kutoroka dhambi kwa kutumia visingizio vya kijinga!

Hebu tuchambue huu upuuzi mliolishwa, mnaambiwa ni "Neno la Mungu" wakati limejaa sarakasi ambazo hata mtoto wa chekechea anaziona.

Kule Mambo ya Walawi 11:7, Biblia hiyo hiyo inasema: "Na nguruwe... huyu ni najisi kwenu." Msimamo uko wazi, sivyo?

Lakini ruka mpaka Matendo 10:15, utamsikia huyo huyo "Mungu" wa Wazungu akimwambia Petro: "Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi!" Sasa hapa ndipo mnapopigwa changa la macho! Wasabato wanashikilia Mambo ya Walawi, Walokole wanashikilia Matendo. Hivi Mungu alisahau alichokiandika mwanzo au alibadilisha gia angani? Hii ni vurugu!

Mithali 20:1 inasema: "Mvinyo ni mshihaki, kileo ni fujo!" Inakemea ulevi mazima.
Lakini nenda 1 Timotheo 5:23, Paulo anakuambia "Usinywe maji tu, bali tumia mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lako!"..

Yaani hapa ndipo mtego wa Wazungu uliponasa akili zenu mazima. Mungu anageuka kuwa kinyonga asubuhi anasema hivi, jioni anageuka kule, halafu ninyi mnasimama madhabahuni na kusema Bwana asifiwe! Asifiwe kwa lipi? Kwa kuwavuruga akili?...

Hebu tazameni huu usanii mwingine Biblia inakuambia kwenye Wagalatia 2:16 kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali ni kwa imani tu.
Yaani, hata uwe jambazi vipi, ukiamini tu basi milango ya mbinguni iko wazi!.....

Lakini kabla hujakaa sawa, mwandishi mwingine anakuja juu kwenye Yakobo 2:24 anasema, "Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa haki kwa matendo, wala si kwa imani peke yake."

Sasa mnataka kutuambia nini? Huyo Mungu wenu ana matatizo ya kusahau au alikuwa anajikata kauli mwenyewe? Huku mnaambiwa "fanya kazi upate thawabu," huku mnaambiwa "kazi ni bure, amini tu.

Mtu anajiishi anavyotaka akitegemea "neema," huku mwingine anajitesa kwa sheria akitegemea "matendo," na wote wanatumia kitabu kimoja! Huu ni uwendawazimu wa hali ya juu! Yani hapa Wazungu walipokuwa wakiandika hiki kitabu walituvuruga sana, hawakwenda direct kama Waarabu..

Wazungu wanawaimbisha kila siku "Mungu ni upendo," "Mungu ni mwema." Haya, fungueni hiyo Biblia yenu muone ukatili uliopindukia!

Kwenye 1 Samweli 15:3, huyo anayeitwa Mungu anatoa amri ya kikatili: "Nenda ukawapige Waamaleki... uwaue mwanamume na mwanamke, mtoto mchanga na anyoyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda."

Hivi huyu ndiye Mungu mnavyotuaminisha ana huruma? Mtoto mchanga anayeuawa ana kosa gani? Halafu dakika mbili mbele, anawaambia "Usiue." Huu ni ulingo wa machafuko! Leo anasema penda adui yako, kesho anasema fyeka hata watoto wachanga. Kama huu siyo mkanganyiko wa akili, basi ni nini?...

Mababu zetu walijua kuna Muumba mmoja, na huyo Muumba hakuleta vitabu vya kuwafanya watu wapigane mapanga eti kwa sababu huyu amekula nguruwe au yule amesali Jumamosi.

Kwetu, Mungu alionekana kwenye matendo, kwenye mvua, kwenye ardhi, na kwenye uhai hakuwa mungu wa nadharia zinazopingana!....
 
Nimesoma HOJA zako zote juu ya MUNGU wakristo wanamuabudu.

Lakini nazipinga HOJA zako kwasababu tu, KITABU BIBLIA kimeandikwa na watu wenye UPEO mkubwa mno WA AKILI.

Uwezo mdogo na usomaji wetu mbovu unapelekea kuwepo makundi mbali mbali ya waamini katika mafundisho yake.

Wala MUNGU hakutaka kutengeneza makundi haya yenye mkanganyiko,MUNGU ni WA wote.

Sasa kumekuwepo na wanaojiita walimu wa NENO ambao hao wanataka kufaidi kupitia udanganyifu wa mafundisho ya uongo kupitia Neno la MUNGU. Hawa ni wengi na wanazidi kuongezeka ili kututoa mm na wewe katika Imani juu ya Neno la MUNGU.

SASA suluhusho si kuwasikiliza Hawa wenye agenda mbovu. Bali Kaa chini uisome BIBLIA peke yako USITAKE kuadisiwa.

Bila shaka hata ww mwenyew hujaisoma Bali umebeba vifungu Kwa lengo la kuikosoa.

Usichukue vifungu vidogo vidogo ikiwa hukusoma sura nzima kujua Nini hasa kilitaka kuwasilishwa.

Hatusomi Biblia kama hadithi au gazeti au novels.

Inahitaji utulivu sana kuisoma na kuielewa
 
Sawa
 
Attachments

  • FB_IMG_1780315494134.jpg
    FB_IMG_1780315494134.jpg
    87.4 KB · Views: 26
Je Hayo yote yanabadilisha kuwa mwanamume aitwaye YESU:

aliishi karne ya kwanza,
alifanya miujiza,
aliteswa,
akauawa na wasiomuamini,
akafufuka siku ya tatu,
akatokea mamia kwa siku 40?

Bila kusahau kulikuwa na unabii wa matukio zaidi ya 300 ambayo angefanya kwenye maisha yake, ambayo yaliandikwa mamia ya miaka kabla hajazaliwa?

Post in thread 'Hivi Kuna ushahidi wowote Yesu alikuja duniani or it's just a conspiracy theory ya watunga stori?' Hivi Kuna ushahidi wowote Yesu alikuja duniani or it's just a conspiracy theory ya watunga stori?
 
Been learning about Islam lately
:2Head:

1) Jesus is just a Messenger 😂

View: https://youtube.com/shorts/7YYzgMQj3OM?si=5sQsZ2Yqy-07mTq4

2) Jesus spoke of Muhammad 😂

View: https://youtube.com/shorts/A7F3_AytauI?si=I5CQfxBtYMrtm_cb

3) Islam is a religion on peace 😂

View: https://youtube.com/shorts/5yVfDAn5hlE?si=EGImSQ_Q8LRZi_17

4) Muhammad is the first Muslim 😂

View: https://youtube.com/shorts/sWlP1X78b3w?si=9s3QoAINUDcCP07c

5) The Quran is a clear book 😂

View: https://youtube.com/shorts/cswsidQf9vY?si=fD1b87xExQuV1_4f

6) The Quran is Confirming the scriptures 😂

View: https://youtube.com/shorts/4pHRYWZviAc?si=wehIdCNlg8O9ivHU

7) Islam respects women the most 😂

View: https://youtube.com/shorts/HcIDNzfX4sY?si=1ZGnNqPoa3zSL

8) The Quran came to correct the Torah and the Bible 😂

View: https://youtube.com/shorts/51YXg0F91I0?si=dnBwHL2OXGLd2Xol

9) The Heavens and Earth were created in how many days? 😂

View: https://youtube.com/shorts/7JvVVxg5wG0?si=5Up3wcZWLRS3JB5w

10) Is JESUS the Truth, The First and The Last? 😂

View: https://youtube.com/shorts/B3nwkIRXY3k?si=RUX_knmOGTNwStl7

11) Who is coming with angels on Judgment Day? 😂

View: https://youtube.com/shorts/VOPfYgKY90I?si=Dwq66s1JUu7rACLA

12) Are we mistakenly comparing the Bible to the Quran? Who is going to raise the dead? 😂

View: https://youtube.com/shorts/emybUPY7994?si=U5ophOG1WlsBd_6E
 
Hivi kweli akili zenu zimefungwa na kufuli la Wazungu mpaka mmeshindwa kuona ukweli ulio wazi? Yaani hapa duniani hakuna kitu kinachochanganya na kuvuruga akili za watu kama hiki kitabu cha Wazungu!,
Yaani Biblia!.

Inakuwaje Mungu aliyeumba mbingu na ardhi, mwenye akili na mamlaka, aandike kitabu halafu ATUCHANGANYE kiasi hiki? Hivi mnamfanya Mungu ni mwandishi wa hadithi za abunuasi au ni nini? Mnataka kutuambia Mungu ni mbabaishaji kiasi hicho?

Angalia huu upuuzi! Wasabato wamekomalia kuishika siku ya Jumamosi, wanakuambia ukigusa kazi siku hiyo wewe ni dhambi! Dakika hiyo hiyo, wengine wanakuambia, "Acheni ushamba, Jumamosi ilikuwa ya Wayahudi, sasa hivi ni Jumapili, siku ya kufufuka!" Halafu wanakuja wengine wajuaji zaidi wanakuambia, "Ah, Sabato haihitaji siku, Sabato iko moyoni!"

Hivi mnatufanya sisi ni watoto wadogo? Mungu gani huyo anayetoa maelekezo ya siku ya kuabudu halafu kila mtu anaelewa chake? Hiki kitabu cha Wazungu kimejaa mkanganyiko kiasi kwamba hata mkipewa miaka elfu moja, hamtakaa muelewane! Ni machafuko matupu!...

Hapa ndipo kichekesho kikubwa na cha kusikitisha kilipo! Ili uelewe hiki kitabu kinachojichanganya, unaambiwa mpaka umuite ROHO MTAKATIFU aje akueleweshe!....
Yaani Mungu atupe mwongozo wa maisha, halafu wakati huo huo tumuite Roho atueleweshe? Kwani hicho kitabu kimeandikwa kwa lugha ya majini?..

Huyo Roho anayewaambia Wasabato wasile nguruwe, ndiye huyo huyo anayewaambia wa Jumapili wale nguruwe. Huyo ni Roho Mtakatifu? au ni roho ya kuchanganyikiwa iliyopandikizwa na Wazungu ili kutuvuruga akili..

Biblia hiyo hiyo inatumika na watu wanaopiga marufuku kucheza kanisani, wakisema ni fujo.
Halafu Biblia hiyo hiyo ndiyo inayotumiwa na wengine kuruka sarakasi, kupiga ngoma na mayowe utadhani wako disko, wakisingizia Daudi alicheza mpaka nguo zikaanguka!.......

Hivi huu si ni uwendawazimu? Kitabu gani hicho ambacho hakina msimamo? Leo kinaruhusu, kesho kinakataza! Huu ni mtego wa Wazungu wa kutuvuruga akili ili tu.

Utasikia mchungaji anasema, Roho ameniambia ukitumia maji haya ya baraka, unakanyaga mapepo! Biblia hiyo hiyo inatumika kuhalalisha biashara ya maji, mafuta, na vitambaa vya upako utadhani mko sokoni! Hivi Mungu amekuwa muuza maduka ya jumla?..

Mwingine anakuja na mstari wake, anasema "Roho anasema panda mbegu ya milioni moja ndiyo ufunguliwe! Maskini anatoa mpaka senti ya mwisho akitegemea muujiza, huku mchungaji akinunua gari la kifahari kwa kutumia Biblia hiyo hiyo!

Huu ni uhuni! Inakuwaje Mungu aandike kitabu ambacho kinampa nafasi tapeli yeyote kujiita Mtumishi wa Mungu halafu anatumia ujanja wa maneno kuwapokonya watu haki zao? Huu mkanganyiko ndio unazalisha hawa manabii wa uongo wanaochipuka kila kona....

Hebu niulizeni Inakuwaje Mungu aliye mmoja, mwenye akili timamu, aandike kitabu ambacho kinashindwa kutoa msimamo mmoja kuhusu mambo ya msingi?
Huyu anasema kusuka nywele ni chukizo, yule anasema ni urembo wa uumbaji..

Hivi huyo ni Mungu au ni mchezo wa kuigiza wa Wazungu? Huwezi kuwa na kitabu ambacho kinasema NDIYO na HAPANA kwa wakati mmoja! Huku ni kutuona sisi kama hatuna akili!..

Geukia upande wa pili uone wenzenu walivyojipanga. Kurani haina hizi sarakasi za kijinga!.
Kwenye kitabu cha Waarabu, sheria ni msumeno inakata pande zote! Hakuna cha tajiri, hakuna cha maskini, hakuna cha nabii wa uongo wa kujitungia tafsiri.
Kimepangika, kimeeleweka, na hakihitaji upako wa ziada kuelewa kuwa dhambi ni dhambi!..

Kama kitabu chako kinakufanya ubishane na jirani yako kila siku badala ya kukuleta kwenye toba ya kweli, basi hicho ni kitabu cha kuvuruga watu! Amkeni! Mungu hawezi kuwa mwandishi wa machafuko. Acheni kufuata hadithi za Wazungu zinazohitaji sarakasi za kiroho kueleweka.

Tafuteni neno lililonyooka ambalo halitupi nafasi ya kutoroka dhambi kwa kutumia visingizio vya kijinga!

Hebu tuchambue huu upuuzi mliolishwa, mnaambiwa ni "Neno la Mungu" wakati limejaa sarakasi ambazo hata mtoto wa chekechea anaziona.

Kule Mambo ya Walawi 11:7, Biblia hiyo hiyo inasema: "Na nguruwe... huyu ni najisi kwenu." Msimamo uko wazi, sivyo?

Lakini ruka mpaka Matendo 10:15, utamsikia huyo huyo "Mungu" wa Wazungu akimwambia Petro: "Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi!" Sasa hapa ndipo mnapopigwa changa la macho! Wasabato wanashikilia Mambo ya Walawi, Walokole wanashikilia Matendo. Hivi Mungu alisahau alichokiandika mwanzo au alibadilisha gia angani? Hii ni vurugu!

Mithali 20:1 inasema: "Mvinyo ni mshihaki, kileo ni fujo!" Inakemea ulevi mazima.
Lakini nenda 1 Timotheo 5:23, Paulo anakuambia "Usinywe maji tu, bali tumia mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lako!"..

Yaani hapa ndipo mtego wa Wazungu uliponasa akili zenu mazima. Mungu anageuka kuwa kinyonga asubuhi anasema hivi, jioni anageuka kule, halafu ninyi mnasimama madhabahuni na kusema Bwana asifiwe! Asifiwe kwa lipi? Kwa kuwavuruga akili?...

Hebu tazameni huu usanii mwingine Biblia inakuambia kwenye Wagalatia 2:16 kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali ni kwa imani tu.
Yaani, hata uwe jambazi vipi, ukiamini tu basi milango ya mbinguni iko wazi!.....

Lakini kabla hujakaa sawa, mwandishi mwingine anakuja juu kwenye Yakobo 2:24 anasema, "Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa haki kwa matendo, wala si kwa imani peke yake."

Sasa mnataka kutuambia nini? Huyo Mungu wenu ana matatizo ya kusahau au alikuwa anajikata kauli mwenyewe? Huku mnaambiwa "fanya kazi upate thawabu," huku mnaambiwa "kazi ni bure, amini tu.

Mtu anajiishi anavyotaka akitegemea "neema," huku mwingine anajitesa kwa sheria akitegemea "matendo," na wote wanatumia kitabu kimoja! Huu ni uwendawazimu wa hali ya juu! Yani hapa Wazungu walipokuwa wakiandika hiki kitabu walituvuruga sana, hawakwenda direct kama Waarabu..

Wazungu wanawaimbisha kila siku "Mungu ni upendo," "Mungu ni mwema." Haya, fungueni hiyo Biblia yenu muone ukatili uliopindukia!

Kwenye 1 Samweli 15:3, huyo anayeitwa Mungu anatoa amri ya kikatili: "Nenda ukawapige Waamaleki... uwaue mwanamume na mwanamke, mtoto mchanga na anyoyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda."

Hivi huyu ndiye Mungu mnavyotuaminisha ana huruma? Mtoto mchanga anayeuawa ana kosa gani? Halafu dakika mbili mbele, anawaambia "Usiue." Huu ni ulingo wa machafuko! Leo anasema penda adui yako, kesho anasema fyeka hata watoto wachanga. Kama huu siyo mkanganyiko wa akili, basi ni nini?...

Mababu zetu walijua kuna Muumba mmoja, na huyo Muumba hakuleta vitabu vya kuwafanya watu wapigane mapanga eti kwa sababu huyu amekula nguruwe au yule amesali Jumamosi.

Kwetu, Mungu alionekana kwenye matendo, kwenye mvua, kwenye ardhi, na kwenye uhai hakuwa mungu wa nadharia zinazopingana!....
Ni kitabu sawa na hekaya za Abunwas na Kurani. Vitabu vyote vya dini ni hadithi za watu wa kale ziliipewa uungu uchwara.
 
Maandiko yanayodaiwa kwamba ni ya Mungu ni mengi sana.

Kuna Biblia ya wakristo.

Kuna Quran ya waislamu.

Kuna Torah ya wayahudi.

Kuna Tripitaka ya wabudha.

Kuna The Vedas ya wahindu.

Kuna The Kojik ya washinto kule Japan.

Kuna The Guru Granth Sahib ya wasikhism.

Kuna Rastafar Bible ya Rastafarians.

Kila muumini wa vitabu hivi aamini kwamba KITABU chake pekee ndicho neno la Mungu. Na maandiko ya vitabu vingine sio ya Mungu.

Sasa Mungu mmoja hawezi kuwa na maandiko mengi yanayo tofautiana maelezo.

Mungu huyo angelikuwepo, kungelikuwa na KITABU kimoja tu, kwa watu wote ulimwenguni wote.

Mungu hayupo, Ni binadamu tu waliandika hadithi zao uchwara kwenye vitabu na kuanza kuita Neno la Mungu.

If human beings can build a house and call it, the house of God. They can also write a book 📖 and call it, the word of God.

Hakuna Mungu.

Hakuna Neno la Mungu.

Kuna vitabu vilivyoandikwa na wanadamu kama sisi, vinavyoitwa neno la Mungu. Ambavyo havina ukweli wowote ule. Ni hadithi na hekaya tu.
 
Yeyote anayetaka kuwa Mkuu kuliko YESU,

Yeyote anayetaka kuandika kitabu kikuu kuliko BIBLIA:

1)  Kwanza afe, na tuhakikishe amekufa kama walivyohalikisha YESU amekufa kwa kumchoma kwenye mapafu na maji kutoka.

2) Kisha Ufufuke baada ya kuzikwa huko chini baada ya siku tatu wakati ushaoza. Tuweke na walinzi kabisa maadui zako ambao hawakukubali kama waliowekwa kulinda kaburi la YESU. Tuje tufukue tukute mwili haupo. Tukuone live ikiwezekana na uthibitisho wa majeraha yaliyokuua yawepo.

3) Kuwe na unabii kukuhusu ulioandikwa kabla hujazaliwa wa matukio yasiyopungua 300 kukuhusu, kuanzia kutungwa kwa mimba yako, kama ilivyo kwa YESU.

4) Ufanye miujiza kama YESU : wenye magonjwa ya ajabu yasiyotibika wapone, vipofu waone, viwete watembee, wafu wafufuliwe.

5) Wanafunzi wako wa kwanza wakubali kuteswa na kuuawa ili kutoa ushuhuda kukuhusu, wakati hakuna faidia yoyote wanayopata hapa duniani sio utajri sio umaarufu sio wanawake, zaidi ya kudharauliwa, kama wanafunzi wa YESU.

6) Wanafunzi wako angalau watano waandike yote haya uliyofanya, kila mtu kivyake. Kisha wawarithishe wanafunzi wao masimulizi kukuhusu. Na wanafunzi wao wawarithishe wenzao. Tuwape miaka 300.

Kisha wataalam wa forensics kina J. Warner Wallace watuambie hawa jamaa wa hii dini wamejitungia story au ni historia ya kweli inapitishwa kama ile iliyopitishwa na wanafunzi wa YESU.

7) Mwisho kabisa ingepedeza kama ungepita rekodi hii: kitabu cha dini yako kiwe na

vitabu angalau 60,
vilivyoandikwa na watu angalau 40,
kwa miaka isiyopungua 1,500

wote wakikuongelea wewe tu kwa upatano na uelewano kama mtu mmoja,

kwa namna mbalimbali: masimulizi halisi ya historia, sheria, unabii, nyimbo, methali, mafumbo n.k

kama vile Biblia inavyomuongelea YESU.

So you have about 1500years to pull this of. Only that you're late. They have all been late. And all they are and you will be are false teachers.
 
1000055545.jpg

Ona picha hii kwenye hii video, ni Taswira ya Biblia kwa njia ya picha. Mtandao tata kabisa wa uhusiano uliopo ndani ya Biblia.

Kitabu kilichoandikwa kwa miaka zaidi ya 1500 na watu zaid ya 40, ndiyo kinafanana hivi!

Kushoto kwenda kulia ni chapter moja moja Kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo.

Hiyo mistari (arcs, upinde) ni mistari inayounganisha maandiko yake kwa kufuatilia marejeleo yake:

Yaani andiko hili lilinukuliwa hapa au kutimiza unabii uliotolewa katika kitabu au mstari huu wa awali. Zaidi ya marejereleo 63,700!

View: https://youtu.be/2VZLH35sPjo?si=Clg1ylcNwF9fWinR
 
NA BADO HUJASEMA
BADO KUNA VITU VILIONDOLEWA KWENYE BIBLIA AMBAVYO VITAWACHANGANYA WATU
WAKAPIGANA NA VITABU VINGINE VILICHOMWA MOTO
UKISOMA MWANZO UTAONA KUNA VITU
 
Back
Top Bottom